Nimemwambia nibebee Mimba ili nikuoe hataki

Yani kwa kauli hiyo atakae kubali kuolewa na wewe nae apimwe akili. Hivi ikitokea ukapata ajali au ugonjwa ukaadhiri mifumo yako ya uzazi ushindwe kumpa mwanamke ujauzito utaweka wapi sura yako?
Tasa na wasio tasa wote wameumbwa na Mungu.
Wewe omba Mungu akupe mwenza sahihi na ndoa yenye Furaha baraka ya watoto itakuja tu,usimpangie Mungu.
Mwisho umemaliza vzuri ila ulivyoanza umebugi
 
Wanaanza hivi hivi, na mabinti wa siku hizi wasivyojielewa utaona mtu wa hivi ndio anamkubalia anampa mchezo bila shida na kumuacha awe ndio mwanaume wake, hapo akishatest mitambo anamwambia tena atoe ili amle hadi atapochoka kisha amuache.

Aiseee kuna watu ni takataka
Mwisho umemaliza hovyo
 
Umetumia lugha kali sana huku ukimtuhumu mama yake kwa kumpa elimu kuhusu kumbebea mimba mwanaume ambaye hajakuoa bado.

Mkuu kama umeshamtakia hivyo sahau kukubebea mimba, wanawake wanawekaga vitu moyoni haviwatoki kirahisi. Pole.
Kuwa na staha na adabu kwa wanawake uzuri mmoja kuna comment umesema wewe ni mtoto haramu. Nafasi bado unayo ya kubadilika na ukawa na maadili.
 
Duuuh bro hata ningekuwa mie ningekataa yaani unitumie then uni dump kisa sishiki mimba, we oa kama yaliyomo yamo utayakuta,

Kwenye ndoa kuna sehemu wanasema... Kwenye shida na raha...

Shida zenyewe ndokama hivoo kutopata mtoto.

I hope hio legacy yako ya kumpa ujauzito binti ndo aolewe, uitumie pia kwa mabinti zako.
 
Dah....mkuu hebu tupia kapasport size...isijekuwa unamlaumu bure...labda Ana wasiwasi na sura za watoto zitakavyokuwa
Hii kitu nimeshasikia baadhi ya mademu wakiapa kutokuzaa na waume zao kisa wana sura nzito, wako tayari watafute mchepuko handsome wambambikie mtoto mume
 
Wakuu habari

Huyu binti nahisi kaikosa ndoa, yaani ni zoezi simple lakini anashindwa kutekeleza, wakuu sikuizi watu tumeshtuka hatutaki kuoa matasa mwishowe wanaishia kujaza choo tuu, nahisi huyu binti anataka kuzeekea nyumbani.

Inabidi tushtuke wakuu ndoa nyingi zimekosa mvuto kutokana na kukurupuka kuowa mwanamke tasa mjaza choo matokeo yake inakua mzozo kwa ndugu na jamaa kwamba kwanini umeowa gumba.

Mabinti acheni kuchezea bahati wenzenu wanazisaka ndoa kwa waganga sasa endeleeni kushikwa akili na mama zenu.
amekujibu vzr sema ttz ni ww kutaka kumfanya mwenzio kiwanda cha majaribio
 
amekujibu vzr sema ttz ni ww kutaka kumfanya mwenzio kiwanda cha majaribio
Sina maana hiyo mkuu, kiukweli inatulazimu tufanye hivyo kwani mmekuwa hamueleweki, naweza kutoa posa na matakataka mengine lakini unaambulia mgumba

Ila kupitia maoni ya wadau kuna kitu nimekinyaka
 
Sina maana hiyo mkuu, kiukweli inatulazimu tufanye hivyo kwani mmekuwa hamueleweki, naweza kutoa posa na matakataka mengine lakini unaambulia mgumba

Ila kupitia maoni ya wadau kuna kitu nimekinyaka
kuzaa ni majaliwa mkuu..
je sio ww ndio mgumba
 
Back
Top Bottom