Ambae hujaoa/kuolewa usiikimbilie ndoa

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
9,667
12,238
Nimekaa nikawaza sana changamoto ambazo nakutana nazo maishani, changamoto hizi muda mwingine zinanifanya nakufuru, na huwa najuta sana, maisha ni magumu, kazi nazo siku hizi zimekuwa ngumu kiasi kwamba hakuna tofauti kati ya mwenye kazi na asie na kazi. siku hizi ukimpata mtu akakusaidia 1000 tu ya kula mshukuru sana na umthamini kama ndugu.

Miongozni mwa vitu vinavyo nifanya nijute sana mimi mwenzenu ni kuoa nikiwa na umri mdogo, niliingia kwenye maisha ya ndoa punde tu nilipo kuwa na miaka 24. na chanzo kikubwa cha mimi kuingia kwenye ndoa kichwa kichwa ni kwasababu ya ahadi niliyo jiahidi kuwa sitaki mtoto wangu alelewe na baba mwingine ingali nikiwa hai. hivyo katika kurukaruka na mabinti ikatokea huyu mke wangu akashika mimba. sikuwa na jinsi ikabidi tu nifanye uhalalishwaji ili nipate fursa ya kumlea mtoto wangu katika maadili ya wazazi wote wawili. ili mtoto asije kunilaumu hapo baadae. {hii ni kutokana na maisha ambayo nimewahi kuyapitia nikiwa mdogo hivyo sipendi sana mtoto wangu afuate njia yangu}

Kwenye hawa mabinti tunao papukia kuwaoa kuna wengine ni wachawi total, kuna wengine wana majini mabaya ya mikosi,

Kuna kipindi kwenye haya maisha yangu ya ndoa kwenye baadhi ya tarehe zikifika nyumba huwa naiona chungu sana, tunaweza tukanuniana bila sababu maalum, hii hali inaweza kudumu hadi siku nne nakuendelea, nikimuangalia mwanangu bado mdogo ndio kwanza yupo kwenye hatua za kujifunza kusoma.

Kuna muda ukimuamsha mwenzio ili ule tunda la usiku bila sababu za msingi aamki. unaamua tu kumuacha na kufanya mambo mengine ya kukupotezea mawazo. waliosema tumia muda mwingi kumpata mtu sahihi awakukosea.

Ukitaka kuoa kijana mwenzangu ambae hujao hakikisha unaoa mwanamke unae jua historia yake, hapa ni bora ukaangalia wale uliokua nao utotoni ni bora zaidi kuliko kukutana na mwanamke tu juu juu utakuja kujuta kama mimi ninavyojuta.

Waliosema ukitaka kufanikiwa jifunze kubalance ny.ege hawakukosea kabisa, mimi mwenzenu chanzo cha majuto haya yote ni kushindwa kudhidhibiti ny.ege zangu.

Huyu binti kwaajili ya mwanangu ninampenda ila nahisi kuna matatizo yao kwenye ukoo wao ajawahi kuniambia ila haki vile kuna vitimbi haviandikiki kabisa...nashindwa nianzie wapi kuviandika ili jamii inielewe ila kwakifupi usiinkimbilie ndoa...tumia muda miwngi sana kumschunguza mtu ulie nae kwenye mahusiano...usikosee kuoa utajuta sana​
 
Maisha hayana formula, huyo ni chaguo lako ni msalaba wako na lazima ufike golgota.

Wanaume tulishakubaliana dawa ya mwanamke ni mwanamke, turudie somo hili mara ngapi?

Hivi mnajuwa kama mama yetu Samia ni Rais wetu lakini yule mwamba first gentleman ana wake wengi?

Sasa mwamba kamtuliza Rais nyinyi mnasumbuliwa na hivi visecretary?
 
Unaeza laumu mwenzio anakosea, mara majini, sjui ukoo, kuuumbe sababu ya yooote hayo ni wewe!! Kuna shida zingine haziishi kama msipokaa chini wote mkajitathmini kila mmoja akatoa lake la moyoni kirafiki kuna baadhi ya mambo yatapungua
 
hakiandikiki kilicho nikuta ila tusikimbilie kuoa
Tatizo siyo kukimbilia kuoa, Bill Gates na Melinda Gates wamekubaliana kudivorce na kiroho safi tu na pesa siyo tatizo kwao.

Tatizo letu kubwa ndoa za Watanzania wengi kimsingi zilishakufa na wala hazipo ila watu wameamuwa kujiweka kifungoni uonekane na jamii una ndoa wakati kimsingi hiyo ndoa haipo na ilishakufa mnapaswa kuachana kila mtu aanze maisha mapya lakini mnagandana tu, hii ndio tofauti yetu na wazungu hawapo tayari kukaa kwenye ndio isiyokuwa na furaha.
 
kweli akili nyingi inahitajika...ila kuna mengine yanahitaji ujasiri...ivi ikitokea unamuona mkeo anafanya jambo ubnormal gizani mkiwa mmelala...mathalani amekukalia, ama bila sababu za msingi anaamka na kusimama chumbani usiku...ni akili gani itahitajika hapo....?
Anapenda mambo ya waganga? lazima pawe na sababu
 
Watu wengi huwa wanakosea sana kuoana kwa kujuana juu juu tu. Watu wanakutana bar miezi mitatu mbele ndoa.

Lazima ukitaka kuoa umchunguze mwanamke kiundani mpaka kizazi chake cha tatu kwenye ukoo wake uwajue nje ndani. La sivyo utajibebesha gunia la misumari.

Umenikumbusha mzee mmoja juzi tuko maskani tunapiga story za mambo ya ndoa akatuambia "Vijana ukitaka kuoa muoe mama mkwe wako" akafafanua akasema "yani kama unataka kumuoa binti yangu basi muoe mke wangu".

Kuna tulioelewa ila wengine hawakuelewa.
 
Hakunaga mwenye akili kwenye hayo mambo, ni uvumilivu tu na kubebeana mapungufu ndani mwenu na kumuomba Mungu....ukijifanya akili nyingi utaacha ndoa kila baada ya muda flani
kidogo upo upande wangu...je mtu akifanya yale makosa ambayo kwako ni makubwa unaweza kuendelea kumvumilia...?
 
Back
Top Bottom