Najutia kumruhusu kutoa mimba zangu mbili

Shozylin

JF-Expert Member
Jul 21, 2022
297
607
Wakuu nimeandika hapa si kwa lengo la kujivunia bali nikujutia kosa nililo fanya la kumruhusu kutoa mimba zangu mbili.

Ipo hivi, mwaka 2020 niliingia kwenye mahusiano mapya na binti mmoja ambaye sikumdhania kama atakuwa sehemu ya maisha yangu hadi leo kulingana na nilikomtoa. Huyu binti alikuwa akiishi na dada yake, uhuru kwake ulimzidi hadi kufikia hatua ya kuwa anatoka na marafiki zake usiku.

Nilivyoingia kwenye mahusiano naye nikaanza kumpa somo na kumtaka abadilike kwa tabia ambazo mimi sikuzihitaji awe nazo kama mpenzi wangu.

Kwanza nilimuuliza kuwa anatumia uzazi wa mpango akasema hatumii, na huwa anaumwa michango ya tumbo kwaiyo kubeba mimba kwake mpaka atumie dawa, nikasema poa.

Siku ya kwanza na kufanya mapenzi naye siku nne mbele akapata hedhi kama kawaida, baada ya siku zake kupita tukaendelea na mchezo wa kulana hatimaye hakuona tena hedhi yake. Tayari alikua na mimba.

Niwe mkweli kwa wakati huo nilimuweka wazi kuwa sikuwa tayari kuoa na nilimlaumu sana kwakua alinambia kuwa hawezi beba mimba mpaka atumie dawa.

Nikamwambia kama atazaa azaa mimi nitalea. Pia yeye hakua tayari kuwa mzazi pekee. Baada ya mgogoro huo akanipa wazo la kuitoa mimba kama sipo tayari kumuoa, nikamwambia hili la kutoa ni juu yako mie simo. Hatimaye tukaitoa.

Miez 9 mbele akapata ya pili hapa tena nilimlaumu kwa kumwambia hakujifunza kwa mimba iliyopita? Kwanini hakutumia uzazi wa mpango? Nikamwambia hii mimba unazaa ila mimi kuoa mpka 2022 ndiyo malengo yangu. Mwaka huu ulikua 2020, mwezi wa 11 mwishoni.

Mwaka 2021 mwezi 2 , nikakutana na msichana mmoja ambaye alikua pisi kali sana na nilikuwa namkubali kinyama, sasa siku hiyo akaomba tukajikumbushie maana ni miaka sasa imepita tangu tupotezane.

Wakati huo huyu mwanamke wangu nilisogeza geto akawa kila sku analala kwangu na kupika chakula cha usiku, ila mchana anarudi kwa dada yake. Sasa siku hiyo nimekutana na yule mshichana wa kitambo kidogo nikakosa mbinu ya kumuaga huyu mwanamke wangu nilichokifanya nikaamua kuzima simu nikaenda kwa yule msichana wa kitambo nikalala usiku mzima huko.

Asubuhi nimerudi nyumbani mwanamke wangu ananiuliza ulikua wapi, nikamjibu kuwa kama nimerudi salama shukuru Mungu wengine wanaondoka na hawarudi salama. Kikubwa niache nilale nitakwambia niliko kuwa. Nikalala. Asee hili tukio lilimuumiza sana sana, ikafika hatua na kunambia hawezi kuwa na damu yangu kama mimi baba naanza kumfanyia visa vya wazi namna ile, akaanza kuniambia kila siku atoe mimba.

Nilichoshwa na zile kelele zake asee nikaenda nunua dawa za kutoa, tukaitoa. Hapa niliumia na nilimuhurumia kwakua nilijua tuna hatarisha afya yake. Baada ya kufanya lile tukio nikaanza kujilaumu, hivi huyu mwanamke je, akiwa mgumba itakuwaje? Kwanini nimeruhusu tena hili litokee? Sasa hivi naishi naye ninawezaje kumkataa asiwe mke wangu na mpaka sasa kaanza kuwa sehemu ya maisha yangu?

Kuna muda nilitoka kiutafutaji kama miezi 7 nimerudi, ndani ya hii miezi 7 huyu mwanamke akapata bahati ya kujulikana nyumbani kwetu kama sasa mke wangu mtarajiwa/mke kabisa japo hatuna ndoa. Mama yangu akampenda sana huyu binti.

Baada ya miezi 7 nilirudi nyumbani, na hapa sasa nikawa natamani abebe mimba bila mafanikio sasa. Nikajikuta nakua na mawazo na hofu pengine labda tuliharibu uzazi wake wakati tunafanya utoaji mimba!

Nimemhesabia sana siku za hatari lakini wapi.

Ni kama vile baraka siku 5 nyuma huyu mwanamke wangu aliniombaa hela akanunue pedi nikampa, asee siku hiyo nilikuwa na hasira na majuto lakini hisia zangu za majuto na hasira huwa najitahidi asizione kabisa.

Usiku wa jana kanambia anahisi tumbo linamuua halafu akanambia siku niliyo mpa hela ya pedi alienda kununua kipimo cha mimba, akajipima kakuta ni mjamzito. Woooow! Kuanzia usiku saa 10 sijapata usingizi kwa furaha niliyokua nayo + mawazo namna ya kumlea mtoto wetu mtarajiwa.

Kiukweli ni kama Mungu ametupa nafasi nyingine ya kupata mtoto, nahisi ni kama baraka na neema kwangu mimi. Sasa mke wangu ana mimba changa. Kiukweli nashukuru Mungu kwa nafasi hii.

Kuna uzi mmoja humu JF japo nimesahau id ya mhusika, ila jamaa alikuja kuomba ushauri wa mke wake kutokua na uwezo wa kubeba mimba. Niliusoma huo uzi kiukweli wakati nasoma nilikua na huzuni sana na majuto, leo nimepata nguvu ya kuandika na mimi haya.

Napenda kumshauri jamaa kuwa kuna utofauti kati ya kuwa mgumba na kuwa tasa. Ugumba unatibika aombe Mungu na ajaribu kuonana na wataalamu kwa ushauri mzuri (usichoke).

NB: Kamwe asije mtu kwako anaomba ushauri wa kutoa mimba ukamruhusu. Majuto yake ni makubwa japo kuwa kuna njia salama za utoaji lakini sishauri jambo hilo.

Mungu wa mbinguni anisamehe na awasamehe wote tuliowahi kutenda dhambi ya aina hii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom