Mliozaa nje ya ndoa, wawezeshe mapema mlowazalisha ili damu zenu zisije kuteseka

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,385
98,853
Wakuu,
leo Naandika kwa uchungu Sana,
Hivi karibuni Nilikua Kwny msiba wa mfanyabiashara mwenzangu alifariki.
Baada ya msiba kimekaa kikao Cha mirathi.Kama marafiki na washirika wa karibu wa marehemu tulihudhuria.

Kuna mdada Kaja na mtoto mgongoni na kujitambulisha kua alizaa na marehemu enzi za uhai wake, mtoto Sasa ana miaka 2.

Baada ya kuskia vile mjane wa marehemu kawa mkali sn kua hamtambui huyo mtoto, anachojua huyo mdada Ni mpangaji tu kwenye nyumba yao mwaka wa 6 huu tangu 2016 kipindi hicho huyo mdada akiwa ni mwanachuo. Habari za Alikua ni hawara yake na alizaa nae Ndo anaziskia leo Hii pale msibani.

Kaka wawili wa marehemu wakamtetea binti kua wanamtambua na marehemu alishawatambulisha kwa uyo binti na huyo mtoto kabla hajafariki, japo kwenye wosia hajataja kazaa nje Wala kua na MKE mwngn tofauti na mkewe.

Kaka hao wakasisitiza busara itumike huyu mdada nae afikiriwe kwenye mirathi maana ana damu ya ukoo wao, kwamba ile nyumba ya kupanga anayoishi mdada, aachiwe iwe yake Moja kwa moja ili aweze kumlea huyu mtoto wake kwa kutumia Kodi za wapangaji maana BINTI alierithishwa hiyo nyumba. Tayari kesharithishiwa nyumba nyingine moja na shamba la miti mkoani.

Mjane wa marehemu pamoja na binti alierithishwa wakawa wakali sana kwamba hawamtambui mtoto Wala mdada. Mzozo ukawa mkubwa wazee wa familia wakaingilia Kati na kutoa msimamo wa familia kua, kwa mujibu wa uislamu marehemu alitakiwa amrithishe uyo mdada chake mapema kwa ajili ya mwanae kabla hajafariki.

Kwahyo msimamo wa familia ukawa ni wamemtambua mtoto Ni ukoo wao, ila suala la urithi hatopata Chochote kitu.
Na Siku 2 mbeleni tumekuja kuskia mjane na binti aluyerithishwa walienda kumfurusha kwenye ile nyumba kwa kumtupia vyombo vyake nje yule mdada aondoke kwenye mazingira yao. Hii kitu imeniacha mdomo wazi.

Story za hapa na pale,
Nikagundua mdada kwa sasa Ni jobless na alimtegemea marehemu kwa kila kitu, na mahusiano Yao yalianza binti akiwa mwaka wa 2 chuo baada ya kupanga pale.

Mdada kabadilika kutoka mpangaji,
kua hawara wa mwenye nyumba na kuacha kulipa kodi.Mwaka wa 3 kabeba mimba na kujifungua akiwa pale pale kwenye ile nyumba na kua Mchepuko wa kudumu wa marehemu bila MKE wa marehemu kujua.

Nnachoomba,
Ndugu zetu waislamu naombeni mlitolee ufafanuzi hili la mtoto au MKE wa nje ya ndoa kutoruhusiwa kurithi mali limekaaje?
Suala Ni Kweli au sio kweli?

Kama Ni kweli,
Nawasihi sana Wanaume mlioozaa na Michepuko, wawezesheni mapema kiuchumi michepuko yenu kwa ajili ya future ya damu zenu

NAWASILISHA
 
MWANZO 6:1-8

Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.

Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.

Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.

Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.

Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.

Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya.
 
Hii changamoto inawakumba wanawake wengi.

Tanzania kama mwanamke hajaolewa na amezaa na mwanaume tu au hata mume wa mtu ni ngumu sana mtoto kupata stahiki yake ikitokea mwanaume huyu kafariki.

Muhimu wanawake tusijisahau, tufanye kazi Kwa ajili ya kesho yetu na watoto wetu, kutegemea sana mwanaume mwisho huja kuwa maumivu makali sana.

Ni ngumu sana Kwa mwanamke ambaye hajishughulishi na chochote kuanza kujishughulisha Hadi akasimama akishafiwa na mume/mzazi mwenzie, ila ni rahisi kidogo (Kuna kanafuu) mwanamke kuendeleza biashara au kazi yake akishafiwa maana anakuwa kashazoea. Huyu ambae hajazoea anahisi Dunia imemgeuka, inamtesa ila kiuhalisia wala haimtesi ni maisha Sasa yanataka iwe hivyo.

Wanaume wafunzeni wanawake kujitafutia hata kama mnauwezo wa kuwapa Kila kitu, mjue Kuna Leo na kesho, sio kifo tu, Kuna kuugua muda mrefu, kukosa kazi, biashara kwenda vibaya n.k. acheni wake/wanawake zenu wajifunze kutafuta hata mia mia au waajiriwe, muhimu wajiheshimu na wawaheshimu.

Wanawake msikubali kukaa tu hata kama mnapewa Kila kitu, Mungu akileta mtihani haandiki barua.
 
Na kesi kama hizo zipo nyingi tu, ila wadada nao waache tamaa za kijinga mtu anajua kabisa jamaa anae date nae ana familia yake Na yeye anakubali tu kirahisi kuzaa nae bila ya makubaliano yoyote ila kwakuwa yuko vizuri kiuchumi mwisho wa siku ndo yanatokea Kama hayo halafu unatia huruma,
Wakati ulivyokua unatembea Na mume wa mtu kwa kificho ulikuwa unajiona mjanja
 
Na kesi kama izo zipo nyingi tu, ila wadada nao waache tamaa za kijinga mtu anajua kabisa jamaa anae date nae Ana familia yake Na yeye anakubali tu kirahisi kuzaa nae bila ya makubaliano yoyote ila kwakua yuko vizur kiuchumi mwisho wa siku ndo yanatokea Kama Ayo afu unatia huruma,
Wakati ulivokua unatembea Na mume wa mtu kwa kificho ulikua unajiona mjanja
Tusimlaumu binti,
Wanawake wakishapenda
Wana tabia ya kuamini na kijipa matumaini atakuwa nae daima, anaeteseka hapo Ni mtoto
 
Hii changamoto inawakumba wanawake wengi.

Tanzania kama mwanamke hajaolewa na amezaa na mwanaume tu au hata mume wa mtu ni ngumu sana mtoto kupata stahiki yake ikitokea mwanaume huyu kafariki.

Muhimu wanawake tusijisahau, tufanye kazi Kwa ajili ya kesho yetu na watoto wetu, kutegemea sana mwanaume mwisho huja kuwa maumivu makali sana.

Ni ngumu sana Kwa mwanamke ambaye hajishughulishi na chochote kuanza kujishughulisha Hadi akasimama akishafiwa na mume/mzazi mwenzie, ila ni rahisi kidogo (Kuna kanafuu) mwanamke kuendeleza biashara au kazi yake akishafiwa maana anakuwa kashazoea. Huyu ambae hajazoea anahisi Dunia imemgeuka, inamtesa ila kiuhalisia wala haimtesi ni maisha Sasa yanataka iwe hivyo.

Wanaume wafunzeni wanawake kujitafutia hata kama mnauwezo wa kuwapa Kila kitu, mjue Kuna Leo na kesho, sio kifo tu, Kuna kuugua muda mrefu, kukosa kazi, biashara kwenda vibaya n.k. acheni wake/wanawake zenu wajifunze kutafuta hata mia mia au waajiriwe, muhimu wajiheshimu na wawaheshimu.

Wanawake msikubali kukaa tu hata kama mnapewa Kila kitu, Mungu akileta mtihani haandiki barua.
Sahii kabisa,
Wanaume tuwajengee uwezo wa kujimudu kiuchumi tunaowazalisha kwa maslahi ya damu zetu
 
MWANZO 6:1-8

Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.

Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.

Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.

Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.

Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.

Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya.
Hapa panahitaji ufafanuzi, umeniacha Njia panda
 
Ukoo wana haki ya kukataa maana kama mwenye mtoto mwenyewe alishagawa na hakumkumbuka iweje waingilie? Na huyo mdada akome ajifunze aliona akizaa atachukua nafasi ya bi mkubwa, je ingekuwa ni kwa upande wake angekubali?

Michepuko wanajihesabiaga haki wakishazaa na waume za watu, swali la kujiuliza ingekuwa wao ndo wenye waume wangekubali?
 
Wakuu,
leo Naandika kwa uchungu Sana,
Hivi karibuni Nilikua Kwny msibani kwa mfanyabiashara mwenzangu.
DeepPond hilo suala ni kweli kwa mujibu wa mafundisho ya kiislamu kuwa mtoto wa nje ya ndoa harithi kitu ila ni vizuri baba mtu akamkatia chake mapema kabla ya kufariki.

Huyo rafiki yako ndio alifanya kosa hapo. Mke wa rafiki yako yupo sahihi kabisaaa wala asilaumiwe.

Yote haya yamewekewa sheria kwa kuwa Uzinzi ni jambo mno ila watu wanachukulia poa tu

#Uzinzi haujawahi kumuacha mtu Salama#
 
@DeepPond hilo suala ni kweli kwa mujibu wa mafundisho ya kiislamu kua mtoto wa nje ya ndoa harithi kitu ila ni vizuri baba mtu akamkatia chake mapema kabla ya kufariki

Huyo rafiki ako ndo alifanya kosa apo
Mke wa rafiki yako yupo sahihi kabisaaa wala asilaumiwe

Yote haya yamewekewa sheria kwa kua Uzinzi ni jambo mno ila watu wanachukulia poa tu

#Uzinzi haujawahi kumuacha mtu Salama#
Kwahyo mafundisho ya uislamu ndo yanamchukulia mtoto wa nje Kama mtoto haramu au vipi?

Huoni kama mtoto aliezaliwa nje anabebeshwa mzigo wa lawama na mateso usiomhusu?
 
Wakome watu kama hao hata sinaga tone la huruma, wakati akiamua kuzaa hakuzaa kwa ajili ya huyo mwanaume, alizaa kwa starehe zake tu alee mwanaye bila kutia huruma. Kama mwanaume akilea sawa, asipolea yote sawa wakubaliane na hali. Watu wa kuingilia ndoa za watu hawana huruma umbwa hizo
 
Back
Top Bottom