Nimemuongezea ulinzi mchumba wangu

Nimemuongezea ulinzi mchumba wangu

hatari...unamwekea mlinzi kabisaaaa??? pole...mwanamke halindwi,,,kama amekupenda anajicommit kwako na ana hofu ya mungu atakupenda tuu..kama hajakupenda nje atachovya kama kawaida??/
 
Fuso kazi yake kubeba mizigo tu sio kufanya mambo ya udukuzi. Inaonekana wewe ndio hujaelewa nini nimesema hapo. Nimesema kama nataka kuonana na huyo demu wako mimi namtumia sms shoga yake au ndugu yake ampigie simu kama waende shopping au atowe sababu yoyote ile ili atoke. Wewe utaona ametoka na shoga yake au ndugu yake kwa mihangaiko yao ya kawaida tu. Kumbe anakuja kwangu mimi hayo mambo nishafanya sana tu Mkuu acha kujifanya sungusungu wa papuchi mbululaz wewe.
hahahahahahhahah, hii nimeipenda ingawa na mimi nimedukua ila i need to reshuffle my tactic!
 
Ndugu wanajamvi,

Kama mnavyojua ulinzi ni kitu muhimu sana, hata nchi zinakuwa na jeshi ili kuhakikisha adui hapenyezi wa namna yoyote ile. Ulinzi huanzia ngazi ya taifa, kaya hadi mtu binafsi. Yote haya ni kumwepusha na figisu za vijana wa mjini ili tuweze kufunga pingu za maisha mwakani kwa usalama na amani.

Nilifikia uamuzi huu muhimu maana sitaki mwisho wa siku tushirikiane na watu ambao kazi yao ni kujaribu kudokoa matunda ya wenzao, yaani mimi nilime, ninyweshee maji kisha matunda tule wote - hilo ni BIG NO!

Sitaki kusikia ushauri ule wa Traditional wa eti mwanamke anajilinda mwenyewe, huu ni ushauri mfu ambao haupimiki kabisa hata kwenye mizani, abiria lazima uchunge mzigo wako kuanzia mwanzo wa safari hadi utakapofika stendi, upotevu wa mzigo wako hutaweza kumlaumu Konda, Dereva ama muhudumu yoyote wa kwenye gari sababu huo utauwa ni uzembe wako.

Sasa hatua nilizochukua kuimarisha ulinzi kwa my wife to be, kwa nia nzuri kabisa, na kwa kutumia mbinu za medani nimefanikisha yafuatayo:- kama nilivyowaeleza mwanzo kwamba ulinzi ni jukumu la kila raia ndani ya nchi yetu.

1. Kujiunga kwenye magroup yake yote ya WhatsApp bila yeye kujua - naona kila anachopost.
2. Nimehakikisha najua Username na Password zake zate za mitandano ya Kijamii, hata ID yake ya humu JF nimeshainyaka pia.
3. Napata copies za SMS zake zote za WhatsApp kila akipost, hii usiniulize kwa namna gani nimefanikisha hili.
4. Napata copy za calls zake anazopiga na kupigiwa na mtu yoyote yule, then nazifanyia kazi, zile nazoona zinataka kuleta hali hatarishi basi muhusika nahangaika nae.

Ya tano bado naifanyia kazi - hii nawasiliana ma mtalaam wangu ili tuone namna nzuri ya kuifanyia implementation bila kumtelea madhala makubwa sana mdokozi wa mali za watu kwa kutumia nguvu za giza!

Mwanaume usiye na wivu basi una mapungufu, ulinzi ni kitu muhimu usijidanganye uta-share na watu bila wewe kujijua, yawezekana hata marafiki zako wakawa wanakula mzigo na wanakusanifu tu, wanawake wameumbwa na siri nzito, kuweni makini. Mimi mimeshachukua hatua wewe je?

Mlinde mkeo, mlinde mchumba wako, mlinde mpenzi wako.

Nawatakia siku njemaaa.

BY Fuso!

MUNGU ASIPO ULINDA MJI, AULINDAE ANAULINDA BURE......Zaburi 127: 1
 
Acha uongo, 80% uliyoyasem hayawezekani kabisa, kama akitaka kuliwa analiwa tuu na hicho ki nokia tochi ambacho hujui hata kama kipo
 
Hujanielewa, nimekwambia calls zake zote zinakuwa recorded na kuwa fowarded kwangu bila yeye kujua; sms zote pamoja na zile za WhatApp nazo vile vile. , kwa hiyo nitakusikiliza na nitakukamata kama kuku kabla hata hujaliona paja, then utashuhudia kitakachokupata ili ukawasimulie na wezi wenzio!!

Nipe namba yake unikamate
 
Baada ya ndoa kinacho fuata ni kuaminiana na sio kulindana, huenda ukawa sawa kwa upande mmoja ktk mpango wako huo, lakini nini maamuzi yako ikiwa utagundua kachepuka? Mbinu ya 1 hadi ya 4 itakusaidia kugundua wanao mnyatia lakini hiyo mbinu ya 5 ndio itakayo kufanya ulete mrejesho hapa.
 
Hakuna kitu kigumu kama kumlinda binaadamu. Na jambo hilo linakuwa gumu zaidi kama mtu mwenyewe anayelengwa ni mwanamke.

Mkuu unajipa kazi ya ziada na stress za bure tu. Hiyo shughuli ni futile bro !!!

Lakini mkuu naomba unijibu maswali yangu manne (4) ya kijinga kama ifuatavyo:

1. Unauhakika gani kuwa hizo unazojua ndizo IDs pekee shemeji yangu alizonazo in all social networks?

2. Je kama ana kisimu cha tochi ambacho hukijui na hutakuja kukijua na labda ndo anachotumia kuwasiliana na vidumu vyake?

3. Je una codes zao za siri za mawasiliano wanazotumia ili kuwa-fool ninyi wapenzi wao?

4. Je umefanyaje ili kuzuia mawasiliano yake na wabaya wako yale ya ana kwa ana pale nyumbani huko njiani, sokoni, makazini, maeneo ya ibada etc etc?
 
Kanichekesha huyu anataka aje atulilie humu,naona wanaume sasa hivi wanalia tu humu MMU

Kisa wanamwogopa babu Ngabu😀😀.

Hivi inakuwaje lakini kibabu kama mimi niwakoseshe amani hawa watu? Tena vijana mashababi....au ndo chipsi mayai hizo?

Swagga zangu hazina mpinzani walah!
 
Kisa wanamwogopa babu Ngabu😀😀.

Hivi inakuwaje lakini kibabu kama mimi niwakoseshe amani hawa watu? Tena vijana mashababi....au ndo chipsi mayai hizo?

Swagga zangu hazina mpinzani walah!

We babu Ngabu wewe itakua huli chips yai nadhani,eti swaga zako hazina mpinzani
 
Maajabu ya kilindwacho, humwambia mwizi niibe haraka haraka nikalindwe. Hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha
 
Back
Top Bottom