Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 34,637
- 38,017
Huyo Dada ni mjanja, alikuwa hamtaki jamaa na alipania kumchuna amkomoe halafu wasimuliane na mashoga zake.
Sasa wakasimuliane hayo yaliyowakuta
Huyo Dada ni mjanja, alikuwa hamtaki jamaa na alipania kumchuna amkomoe halafu wasimuliane na mashoga zake.
Sasa wakasimuliane hayo yaliyowakuta
We mwanamke mumeo ile kitu unampa SAA ngapi?
Wakuu habari za mida,
Jana jioni nilipotoka kazini nilipitia recreation place moja hivi nipate moja moto moja baridi wakati nikisubiri foleni iishe ingawa sina Gari ila kwa kawaida ikifika saa mbili usiku kidogo fujo za Dala dala Posta -Makumbusho zinakua zimepungua. Basi nikiwa hapo recreation nikampigia simu mrembo mmoja hivi staff mwenzangu kazini ambae nimekua nikimfuatilia sasa kwa wiki kadhaa nikamwomba apite nilipo tupate japo bia mbili mbili huku tukizungumza.
Cha kushangaza kaja na mashoga zake watatu na yeye wa nne, baada ya kuona nimeshtuka akajibalaguza kwa kusema eti amekutana nao hapo nje tu, wakaagiza Windhoek lager mmoja akaagiza Savana dry, nikasema moyoni kwa kijita lelo ni lelo walipofika bia ya tatu kila mmoja huku wakiongea stori zao za kina diamond na Ali kiba zisizo na kichwa wala miguu wawili wakainuka kwenda jikoni kutazama nyama choma nilisikia kama ganzi miguuni na ndipo hapo nilipoanza kufikiria escape from sobibo, wakati nimeanza kupanga escape plan warembo hao walikua bia ya sita kila mmoja.
Wadada wananyonya bia sijawahi ona, mimi nipo bia ya tatu tena safari nikinywa kwa kuichungulia. Yote tisa, kumi wakaagiza kongoro la kukatia pombe wakati wakisubiri nyama choma iive ambayo sikutaka hata kujua ni kiasi gani. Ilikua ni saa mbili na nusu usiku nilipojifanya nakwenda kuongea na simu nje nilipofika nje ya bar hiyo iliyokaribu na Billicanas Club nilipiga hatua ndefu kuelekea Posta Mpya huku nikitazama nyuma kwa hofu kama kuna mtu ananifuata.
Nikatokea NMB phonex house na Mungu si Athuman hili hapa Dala dala la Makumbusho Posta likiwa na abiria wachache nikadandia hill hilo na kupiga ishara ya msalaba kwa kufanikiwa kutoroka salama.Nikazima simu hadi saa sita usiku ndo nikaiwasha na kukutana sms kama 30 hivi za matusi kutoka kwa yule binti Wa kazini, akiniita majina yote mabaya kuanzia firauni na mengine mengi, kwamba wakiitwa wanaume nawe utatoka?
Kwamba jianaume suruali tu, kwamba aliniona wa maana kumbe sina lolote. Leo asubuhi amenikuta nimeshakaa kwa meza yangu amefika akasimama mbele yangu akaniangalia kwa macho makali sana na akavuta msonyo mrefu sana na kwenda kwenye idara yake, nahisi ndio nitakua nimekataliwa hivyo. Wakuu msichana anakuja kunikomoa hivyo huku anaujua kabisa mshahara wangu tupo ofisi moja anajua mimi ni Karani tu wa kawaida. Wote mimi na yeye net yetu inalingana.
Mabinti mjirekebishe sio vizuri kwa kweli
hahaha katarijasubhila kwikekakeka wamakagwata.
Una roho ndogo sana. Ukioa kuna siku anakuja mama mkwe hapo na wanae wawili kumuuguza. Si utaacha kununua chakula nyumbani kwako?
By the way kuna wadada wengi tu wanaolipa bill zao bila kutegemea 'shemeji'. Si ajabu walikucheka tu na kukuona mmasai