Kwa iyo bia zko nani alilipa?!
lol nimecheka ungeuliza deni walilipaje kunogesha story
hahah hiyo ni ESCAPE FROM NOWHERE ungepiga bia na nyama choma sawa na wao ingekuwa Poa zaidi ila hujaniangusha bingwa!!
Huyo Dada ni mjanja, alikuwa hamtaki jamaa na alipania kumchuna amkomoe halafu wasimuliane na mashoga zake.
Ni tambia mbaya za wadada sasa kama hamtaki kwanini amlie hela zake? Ndio mana wanafanyiwa kitu mbaya
Una roho ndogo sana. Ukioa kuna siku anakuja mama mkwe hapo na wanae wawili kumuuguza. Si utaacha kununua chakula nyumbani kwako?
By the way kuna wadada wengi tu wanaolipa bill zao bila kutegemea 'shemeji'. Si ajabu walikucheka tu na kukuona mmasai
Nadhani amekusoma na kwa kuwa wapo sehemu moja kikazi itabidi akamuulize aje kumalizia huu mkasa.
jean phillipe beyun
Umenichekeshasana.mwombe tena outing,mwambie this time aje peke yake.kwa akili ya videm uchwara kama hakimtaki mtu huwa kinamtia gharama za style ya aina hiyo ya kuleta kundi ktk dates.
Ngoja ufunguliwe kesi ya unyanyasaji wa kijinsia..
Hii imenikumbusha siku moja nimemuahidi binti mmoja ambae kwa wakati huo nilikua bado sijachana bahasha kusoma barua,tukakubaliana aje,kumbe kapanga kuja na wadogo zake wa kiume wawili,yaani mmoja ni mdigo wake wa kiume na mwinhine ni rafiki ya huyo dogo walikua wanasona form six nadhani.
Basi wakatangulia kufika eneo la tukio ingawa yeye hajaniambia kaja na hao madogo,ile nakaribia kufika namuuliza uko upande gani ananielekeza na kuniambia yuko na wadogo zake,nikaishiwa nguvu gafla.
Nikamuuliza kwa nini kaja nao akadai wako likizo kaamua awatoe,nikamwambia mbona hukunijulisha akasema alijua sitajali,hapo nimerudi pembeni kufikiria niende au nisiende,mwishowe nikaamua kwenda,ingawa nilikua nishamaind sana.
Nkaamua tu kulipia bil zao zote ingawa bil ilikua kubwa maana madogo walkua na uchu na pombe sana ingawa dada yao hanyw.
Kisha wakajiongeza kwamba wanaondoka hvyo nkabak na dada yao ambae walmuona kesho yake