The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,503
- 2,046
Nimemsikiliza sana naibu katibu wa chama cha soka cha Burundi kuhusu mipango yao ya maendeleo, nikajaribu kuwaza kuhusu mwelekeo wa taifa letu kimichezo, nikaona bado tuna safari ndefu sana kufikia matamanio yetu kimichezo.
Alipoulizwa na mtangazaji wa chombo kimoja cha habari hapa nchini kuhusu siri ya mafanikio iliyonayo Burundi kimichezo hasa soka, alisema.
" Hii ni matokeo ya utashi wa serikali nzima kwani baada ya kumalizika vita tukawa na hukumu la kujenga amani. Baada ya kuona tumefanikiwa kujenga amani ikiwa zamu ya kujenga maendeleo.
Swali likawa tunajengaje maendeleo katika mazingira ambayo hatuna rasilimali watu ya kutosha kama mlivyo watanzania? Ndipo tukaja na wazo la kuinua viwango vya huduma ili tuuze huduma duniani.
Chini ya mpango huu tumefanikiwa kuzalisha makocha wengi marefaree wachezaji na watendaji wengine wenye ubora unaokidhi viwango vya kimataifa".
Ni Kwa muktadha huu sio ajabu Tanzania tumejaza makocha warundi wachezaji warundi yaani ni aibu tupu. Hata hivyo nieleweke vizuri sina tatizo na warundi kuja kufanya kazi as long as wana sifa na vigezo.
Hoja yangu ni kwamba tumewawezeshaje watu wetu kuteka masoko ya ajira zinazohusu vipaji vyao Kwa mataifa ya nje?.