Nimemshangaa General Mirisho Sarakikya

Nimemshangaa General Mirisho Sarakikya

mfano email ina despatch book?

Yeye kaonesha email Au kaonesha Barua aliyopeleka Bungeni Tena Barua hiyo anayosambaza mitandaoni haijasainiwa Pengine ame draft Siku hiyo hiyo!

Kama katuma email Pia aoneshe katuma Kwenye official email ya Mtu husika?
Mtendaji Mkuu wa Bunge Kwenye Masuala ya Utawala Ni Katibu sio Spika
 
email ni tofauti na barua?
 
email ni tofauti na barua?

Gari Na Meli havina tofauti Kwa Kuwa vyote ni Vyombo vya Usafiri

Gari Na Meli Vina tofauti kwa Kuwa kimoja ni Usafiri wa Baharini Na kingine ni Usafiri wa Nchi kavu

Sijajua unauliza hilo swali
Kwa muktadha upi?
 
Huenda mimi ndio sielewi, Nassari anatakiwa bungeni aonekane sura yake, au michango yake haionekani? Mfano profesa Muhonngo yuko bungeni? Umewahi kumuona akichangia? Huko bungeni nusu yao wapo kusaka sitting allowance tu ila hawana mchango wowote zaidi ya kujaza vyoo. Bunge lenyewe hilo dhaifu ndio la kwenda kuhudhuria muda wote? Kama una shughuli zako ni bora ufanye shughuli zako kuliko kwenda kupoteza muda kusikia bunge la kumsifia rais.
Professor Muhongo yuko bungeni kama kawaida halafu bungeni kuchangia siyo lazima uongee na kupiga kelele unaweza kutoa mchango wako kwa Maandishi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gen. Sarakikya njaa inamsumbua. Akipona njaa yake au kama njaa yake ikahama toka kichwani iliko kwa sasa ikarudi tumboni ataacha upuuzi alioamua kujihusisha nao.
Ujielewi kabisa.

Kumbuka ni nani halafu unasema ana njaa? Uyo anakula hadi anapoingia kaburini na anaijui nchi in and out kuliko wewe?

Uwe na heshima kwa watu wakubwa waliopambana hadi tunaona Tanzania ya sasa wamekusababisha uwe salama hadi leo umekaa kwenye keyboard unamtukana,serious?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Leo kulikuwa na kikao cha Wachili wa kabila la Wameru.Wachili ni viongozi wa kimila wa kabila la kimeru.Ni sawa na viongozi wa kabila la waMaasai Laigwanani.

Wachili leo wamekutana kwaajili ya kuunga mkono uamuzi wa Spika wa kumvua ubunge Mh Nassari kwa kosa la kutohudhuria vikao vitatu vya bunge kwa mujibu wa kanuni za Bunge adhabu yake ni kuvuliwa / kufukizwa bungeni.

Katika kikao hicho ambacho kiliitishwa haraka mara baada ya uamuzi wa Spika pia kilihudhuriwa na Mkuu wa JWTZ mstaafu General Mirisho ambaye pia alipongeza uamuzi huo wa Spika.

Kwa wadhifa wake nadhani hakutakiwa kujihushisha na siasa nyepesi nyepesi.

Najiuliza Nassari akienda Mahakamani na kuonekana alionewa General Mirisho atauweka wapi uso wake.CDF ni wadhifa mzito sana,sijawahi kuona au kusikia General Waitara au General Musuguri wakitajwa tajwa katika mambo ya ajabu ajabu.

Mbaya zaidi kikao chenyewe kilikuwa kimetamalakiwa na wanaCCM waliovalia kofia na fulana za Chama.

Pengine Mwl Nyerere alikuwa sahihi kumwondoa General Mirisho JWTZ na kumpeleka Nigeria kama Balozi.

Naomba kuwasilisha kwa unyenyekevu wa viwango vya kimataifa.

Ngongo mgombea ubunge mtarajiwa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya CUF ya Propesa Lipumba.
Kwani Sarakikya ni CDF?

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Hehehe ...sasa mbona Bananga anamfirigisa dogo janja?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu mada ni CDF mstaafu kushiriki vikao vya siasa.Unaweza kuongeza kiduchu je kikao kilikuwa kimeitishwa na Washili kweli au CCM iliwatumia washili kwaajili ya malengo ya kisiasa ?.

Suala la uhalali wa Nassari kukacha vikao vya Bunge hiyo ni mada nyingine pana kweli kweli tusichanganye mada.

Nje ya mada kiduchu.

Nassari anayajua mazingira ya siasa za awamu ya tano.Binafsi nadhani Nassari anatakiwa ajilaumu mwenyewe kwa kukifikisha chama chake katika wakati mgumu.

Utetezi wake unaweza kuwa katika sehemu mbili,Sheria ambayo nadhani ana nafasi kubwa ya kumshinda Spika iwapo atakimbilia mahakamani.

Pili ni utetezi wa kisiasa hapa hata Mimi napata kigugumizi kidogo.Itabidi afanye kazi kubwa sana kunishawishi na kuwashawishi wapiga kura wake kwamba hakuwemo katika lile kundi la kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa yule.

Zilikuwepo fununu kwa muda mrefu kwamba tayari alishanunuliwa lakini terms zilikuwa bado kuafikiwa na both parties.Hii biashara ya kuunga mkono juhudi kwa hakika itakuja kuwachanganya sana wanasiasa na wananchi siku za mbele.
 
Gen. Sarakikya njaa inamsumbua. Akipona njaa yake au kama njaa yake ikahama toka kichwani iliko kwa sasa ikarudi tumboni ataacha upuuzi alioamua kujihusisha nao.
Wewe jamaa zimo kweli kichwani au hii umetumia masaburi kuwaza.
CDF hata kama mstasfu ni mtu mkubwa sana katika nchi atalindwa, atavishwa, atalishwa na atazikwa na jeshi/serikali katika muda wote wa uhai na kifo.

Vitu vingine msivyojua ni bors kukaa kimya.

Upuuzi wake huyu mzee kwa cheo chake CDF mstaafu hakupaswa kufanya uungaji mkono wa mambo ya kisiasa kivile.
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Leo kulikuwa na kikao cha Wachili wa kabila la Wameru.Wachili ni viongozi wa kimila wa kabila la kimeru.Ni sawa na viongozi wa kabila la waMaasai Laigwanani.

Wachili leo wamekutana kwaajili ya kuunga mkono uamuzi wa Spika wa kumvua ubunge Mh Nassari kwa kosa la kutohudhuria vikao vitatu vya bunge kwa mujibu wa kanuni za Bunge adhabu yake ni kuvuliwa / kufukizwa bungeni.

Katika kikao hicho ambacho kiliitishwa haraka mara baada ya uamuzi wa Spika pia kilihudhuriwa na Mkuu wa JWTZ mstaafu General Mirisho ambaye pia alipongeza uamuzi huo wa Spika.

Kwa wadhifa wake nadhani hakutakiwa kujihushisha na siasa nyepesi nyepesi.

Najiuliza Nassari akienda Mahakamani na kuonekana alionewa General Mirisho atauweka wapi uso wake.CDF ni wadhifa mzito sana,sijawahi kuona au kusikia General Waitara au General Musuguri wakitajwa tajwa katika mambo ya ajabu ajabu.

Mbaya zaidi kikao chenyewe kilikuwa kimetamalakiwa na wanaCCM waliovalia kofia na fulana za Chama.

Pengine Mwl Nyerere alikuwa sahihi kumwondoa General Mirisho JWTZ na kumpeleka Nigeria kama Balozi.

Naomba kuwasilisha kwa unyenyekevu wa viwango vya kimataifa.

Ngongo mgombea ubunge mtarajiwa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya CUF ya Propesa Lipumba.
Upo sahihi General ni cheo kikubwa kujihushisha na upuuzi ule halafu wamekifanya kikao cha kikabila kuwa cha CCM wakati mbunge aliepigwa chini alikuwa kupitia CHADEMA hapo ndo ufala ulipo, lakini weka sawa hapo kipindi Musuguli alipokuwa mkuu wa majeshi(CDF) alikuwa Major General tu.
 
Mkuu nashukuru kwa kuona tatizo ambalo liliripotiwa na kituo chetu pendwa TBC katika taarifa habari saa 2 usiku.

Mkuu wakati General Mirisho akiwa CDF alikuwa na cheo cha Brigadier kabla hajapelekwa ubalozi wa Nigeria.Alikuja pandishwa cheo cha General na Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

General Musuguri alistaafu akiwa full General au ukipenda 4 star General.
 
Uenda ni njaa na mafaò hayatosherezi mahitaji yake

Au ndo mchawi anajidhihirisha kwa jamii

Mkuu wangu General Mirisho hana njaa hata kidogo kwa wadhifa wake jeshi litamtunza hadi mwisho wa maisha yake.CDF ni cheo kikubwa sana tena sana hana shida kumbuka pia Mirisho alishakuwa Balozi wetu Nigeria,Ethiopia kwa muda mrefu sana nadhani zaidi ya miaka 25 au 30 hivi huyu si mtu mwenye njaa hata kidogo.

Nafiki uswahiba wake na Mzee Baba labda ndio sababu lakini njaa hapana hana hizo shida hata kidogo.
 
Tambua kwamba njaa haina baunsa
 
Tambua kwamba njaa haina baunsa

Inategemea njaa ina tafsiri gani lakini kama ni njaa hizi tunazozijua General Mirisho hana kabisa tena kumhusisha na njaa ni kumvunjia heshima pasipo sababu za msingi.

Hoja mahususi si njaa,nadhani tumeelewana.
 
Hiyo email kakuoneSha?

1) Kaituma kwa nani Na lini?
2) ilikuwa ya Taarifa Au kuomba Ruhusa?

3) aliambatanisha Na uthibitisho ( attachment) ya huo udhuru?
4) alijibiwa?
5) Aliujulisha Uongozi wa Chama chake Bungeni kuhusu kutokuwepo kwake?

6) ilionesha huo udhuru Ni wa Muda gani?

Msilete Ujinga
Usiumie ndugu kwani watu wakizidisha mahaba hua wanajitoa ufaham

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom