Heshima kwenu wanajamvi,
Leo kulikuwa na kikao cha Wachili wa kabila la Wameru.Wachili ni viongozi wa kimila wa kabila la kimeru.Ni sawa na viongozi wa kabila la waMaasai Laigwanani.
Wachili leo wamekutana kwaajili ya kuunga mkono uamuzi wa Spika wa kumvua ubunge Mh Nassari kwa kosa la kutohudhuria vikao vitatu vya bunge kwa mujibu wa kanuni za Bunge adhabu yake ni kuvuliwa / kufukizwa bungeni.
Katika kikao hicho ambacho kiliitishwa haraka mara baada ya uamuzi wa Spika pia kilihudhuriwa na Mkuu wa JWTZ mstaafu General Mirisho ambaye pia alipongeza uamuzi huo wa Spika.
Kwa wadhifa wake nadhani hakutakiwa kujihushisha na siasa nyepesi nyepesi.
Najiuliza Nassari akienda Mahakamani na kuonekana alionewa General Mirisho atauweka wapi uso wake.CDF ni wadhifa mzito sana,sijawahi kuona au kusikia General Waitara au General Musuguri wakitajwa tajwa katika mambo ya ajabu ajabu.
Mbaya zaidi kikao chenyewe kilikuwa kimetamalakiwa na wanaCCM waliovalia kofia na fulana za Chama.
Pengine Mwl Nyerere alikuwa sahihi kumwondoa General Mirisho JWTZ na kumpeleka Nigeria kama Balozi.
Naomba kuwasilisha kwa unyenyekevu wa viwango vya kimataifa.
Ngongo mgombea ubunge mtarajiwa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya CUF ya Propesa Lipumba.