Nimempoteza mke wangu kipenzi

Nimempoteza mke wangu kipenzi

Kifo ni ukumbusho mkubwa na wa kweli kwa kila Binadamu duniani kua maisha haya ya sasa ni mapito na kila nafsi itaonja umauti,
Kifo kinatukumbusha usawa wa binadamu,kifo hakibagui tajiri,masikini,mwenye cheo kikubwa wala asiye na madaraka,wote mwisho wao ni mmoja,
Kifo kinatukumbusha thamani ya wakati,kua muda wetu hapa duniani ni mchache sana,hivyo tunapaswa kuutumia kufanya mambo yenye maana na kuacha alama njema,

Pole sana mkuu,
That is Life.
 
Pole sana.

Kifo ni ratiba na mapenzi ya Mwenyezi Mungu, jitahidi kukubali matokeo.

Kila mja ana mwisho wake bila kujali umri, bali kwa kufuata kalenda ya Mungu.

Narudia tena kukupa pole, ninajua namna kifo cha mwandani kinavyouma.
Amefariki kwa sababu ya upasuaji (kupoteza damu nyingi wakati wa process, na unawezakuta mhusika hakuwa mzoefu) Mungu anahusikaje?
 
Siku isiyo sahaulika katika historia ya maisha yangu ni pamoja na hii tarehe 6/11/2026 saa 11 alfajiri nikiwa katika hospitali ya litembo, muda na saa ambayo mke wangu kipenzi alipoteza uhai baada ya kupata upasuaji kwaajili ya kuleta mtoto.

Ee Mungu nakusihi Ee Bwana wangu ikikupendeza wewe umfufue mke wangu kwaajili tu ya utukufu wako ili niwe naye tena, nashindwa kuhimili huu upweke
Pole Sana, Mimi pia najua uchungu wa kupoteza mke umpendae.
Kataa ndoa mna maoni gani sijui.
 
Maternal death bado ni shida kubwa kwenye nchi zetu hizi zinazoendelea. Anyway may GOD grant you quickly trauma recovery...
 
Msiba wa mtu umpendae unauma sana, Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi uweze kusonga mbele na maisha mengine yanendelee :ReeferSad:
 
Back
Top Bottom