Rais Jakaya Kikwete ameamua kwenda Mikumi National Park kwa mapumziko. Naambiwa na wahusika kuwa Rais amekuwa ndani ya mbuga hiyo kwa siku kadhaa sasa. Jana mchana nikiwa ndani ya mbuga hiyo nilikutana na msafara wake ( Pichani). Naam. Mh. Rais ameamua kujichanganya na watalii wengine akiwa kwenye gari la wazi la kitalii na nyuma landrover ya FFU. Huko mbugani, kama watalii wengine, naye amehangaika kutafuta simba walipo ndani ya mbuga hiyo. Na juma lijalo atakuwa kule Butiama, huko anatarajiwa kuunguruma na kutoa maamuzi ya kutikisa nchi. Labda Mheshimiwa Rais anahitaji kuutafuta ujasiri wa simba na tembo wa Mikumi katika kuunguruma na kutikisa ardhi! Angalia picha zaidi na soma maoni: http://mjengwa.blogspot.com