Nimemkuta Mheshimiwa Rais Mikumi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimemkuta Mheshimiwa Rais Mikumi!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, Mar 21, 2008.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Mar 21, 2008
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Rais Jakaya Kikwete ameamua kwenda Mikumi National Park kwa mapumziko. Naambiwa na wahusika kuwa Rais amekuwa ndani ya mbuga hiyo kwa siku kadhaa sasa. Jana mchana nikiwa ndani ya mbuga hiyo nilikutana na msafara wake ( Pichani). Naam. Mh. Rais ameamua kujichanganya na watalii wengine akiwa kwenye gari la wazi la kitalii na nyuma landrover ya FFU. Huko mbugani, kama watalii wengine, naye amehangaika kutafuta simba walipo ndani ya mbuga hiyo. Na juma lijalo atakuwa kule Butiama, huko anatarajiwa kuunguruma na kutoa maamuzi ya kutikisa nchi. Labda Mheshimiwa Rais anahitaji kuutafuta ujasiri wa simba na tembo wa Mikumi katika kuunguruma na kutikisa ardhi! Angalia picha zaidi na soma maoni: http://mjengwa.blogspot.com
   
 2. a.9784

  a.9784 Senior Member

  #2
  Mar 21, 2008
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo tunafanyaje kama JK yuko mikumi.
   
 3. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Anataka ujue kama Rais yupo Mikumi akitalii!Rais kuwepo mikumi akitalii ni habari!labda angeandika amemuona MBowe ungeuliza hayo!
   
 4. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  This is not a politics bwana
  Hapa ni siasa na mambo yanayohusiana na siasa, sasa kwani Raisi kwenda Mikumi kuna tatizo na ni ajabu jamani??
  Tatizo watu wanapenda sana copy and paste, sasa kila wanachokiona wanataka kucopy tu na kupaste

  Ebu jifunze kuleta habari zenye mantiki na za kulisaidia taifa, hapa JF tunachambua habari za kulisaidia Taifa na si vinginevyo

  Acha copy and Paste please
   
 5. RR

  RR JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2008
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Sio mbaya kuwepo hapa wa thread hii.
  Kunawezekana kukawa na mitizamo miwili tofauti hapa:
  1. Akitembelea mbuga yaweza kuwa hamasa kwa watz, ila pia anahitaji kupumzika (si watu wanamwita Vasco Da Gama akienda nje?)
  2. Kwamba anaacha kushughulikia matatizo ya msingi ndani ya nchi yake na kwenda 'kutanua' mbugani. Yapo mengi yanayohitaji utashi na maamuzi yake.
  All in all, JK is normal human being, anahitaji mapumziko.
   
 6. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #6
  Mar 21, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,427
  Trophy Points: 280
  ....ni habari hii pia..ni rais wetu...but all in all rais wetu amezidi kupenda mapumziko ..nafikiri kila mwezi anajipa ka off...inabidi kaka pinda afanye kazi sana kama msimamizi wa serikali..maana rais wetu hata kabla tulijua anapenda raha zake[mtoa hoja hajatuambia kama amemuona ameambatana na mama au kama kawaida akiwa off yupo single and available...maana mama juzi alikuwa lindi......

  mwaka huu pekee ameshapuymzika mwanza,serengeti,arusha..na bado mapumziko ya easther inaonekana ameyaanza mapema sana......

  lakini pia its a good gesture kukuza utalii wa ndani!!
   
 7. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Asante Maggid kwa hii story,

  Unajua juzi wakati Tanesco inatangaza kuwa bei ya umeme itapanda kwa asilimia mia mbili nilijiuliza hili swali kuwa hivi Kikwete yupo wapi? Nyakati kama hizi ndipo maraisi wa nchi huja kutoa matamko na kuwatuliza wananchi kuwa mambo yatakuwa ok.

  Nimesubiri kwa siku kadhaa na kuona kimya.. kumbe Mkwere yuko Mikumi anaenjoy maisha kama hana akili? Huyu Kikwete jamani hata roho huna? Watanzania wanaumia kwa bei za umeme wewe uko Mikumi unakula vekesheni zako kama kawa!?!?!??!?

  Shame on you Kikwete! muogope MUNGU maana unakoipeleka hii nchi ni kubaya kuliko hata kuzimu kwenyewe. Shame on you!
   
 8. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Rais Akitoka Mikumi aende Bilicanas akajurishee!!!!
   
 9. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 135
  Jamani Raisi ni binadamu kama sisi tu na habari kama hii ina umuhimu wake,its always good to know Rais alipo na kile anachokifanya, asante Maggid kwa kutujulisha. Mbona wenzetu mlioko bongo mnakula shushu from friday to monday na hamuoni kuwa hili ni tatizo? Hata hivyo naamini Raisi yupo kazini wakati wowote, hata kama ni personal holiday, his job is all about giving instructions and decision making and we all know how that can be done haswa ukizingatia jinsi technology ilivyokua kwa sasa.
   
 10. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  kujilusha Bilicanas?! hatakuwa ameanza leo. Uliza upewe nyeti za Kikwete kila mara akija marekani ndio utagundua kuwa kwenda Bilicanas ni cha mtoto!
   
 11. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mambo mengine's all about Positive Mental attitude. Si (Watanzania) tunataka kukuza Utalii?

  ...hii nayo imetulia, it's all about PROMOTION kwa vitendo!

  Big Up Mr Prez!...
   
 12. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  PM,

  Kikwete ameamua kutumia solution ya Kichaka... kukiwa na tatizo nchini, kaa kimya usiliongelee ukitegemea kuwa litakwisha lenyewe. Tatizo la umeme ni kubwa sana na watu wanaumia ila JK ndio hivyo yeye anakula vekesheni na kukaa kimya tu.

  Unajua Kichaka hapa marekani ndio amechukua vekesheni kuliko raisi yoyote wa marekani (according to the news). Inaonekana JK anafanya kila kitu anachofanya Kichaka na wanaoumia ni wale wanaotumia zaidi ya nusu ya mapato yao kulipia umeme na usafiri.

  shame on you JK! unawezaje kulala wakati wananchi wako wanaumia?
   
 13. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  akiwa mikumi then??????ulitaka je kupungua hewa iringa,,
  na kama ina umuhimu mbona kwenye blog yako umeshindwa
  kuiweka au huku kuna vilaza wengi wa kushabikia
  unyoronyoro kijana koma tena usirudie mwache ajipumzzishe tena
  yuko na mwenzake mwingine nani sijui labda anaweza kuwa dada yako uliza hapo vizuri,,,,,,,,,,,,
  pasaka njema
   
 14. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ...Samahani, lakini mbona sioni kosa la ndugu Mjengwa kuweka habari yake hapa? Naomba kuuliza, je, unaugonvi binafsi na bwana Mjengwa?!
   
 15. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  lugha chafu ya nini tena...... ?
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,490
  Likes Received: 81,808
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi bei yetu ya umeme katika Afrika ya mashariki na kati kama sikosei ndiyo ya juu kuliko nchi nyingine yeyote. Wakiongeza hiyo asilimia mia mbili ndio utakuwa haushikiki kabisa na labda umeme wetu ndio utakuwa wa bei kubwa duniani kuliko nchi nyingine yeyote. Athari yake itakuwa viwanda vingi vitafunga virago kwenda 'kuwekeza' kwenye nchi ambazo umeme ni bei poa ukilinganisha na wa Tanzania.

  Miti ndiyo itazidi kukatwa ili kutengenezea mkaa na kuifanya Tanzania iongeze speed kubwa sana kuelekea kuwa jangwa. Watanzania wengi kutokana na mishahara duni umeme hawataweza kuumudu basi watarudi katika maisha ya mwaka 47 ya kutumia mishumaa, vibatari au chemli. Sijui maisha bora aliyoyaahidi Muungwana yako wapi, labda alitaka kusema maisha magumu kwa kila Mtanzania.

  Halafu bado wakisafiri nchi za nje wanawaambia Watanzania walio nje warudi nyumbani maana sirikali inaboresha hali ya maisha ili warudi na pia 'wawekeze' Tanzania. Nani anataka kurudi kuja kuishi maisha ya mwaka 47! Kama kuna Watanzania waliokuwa wanafikiria kufungasha na kurudi Tanzania, basi asilimia kubwa watakuwa wamebadilisha mawazo yao
   
 17. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hivi Rais wa nchi kwenda kujirusha kaa bwana mdogo wa miaka 25 ni jambo la kujivunia?

  Tulicheza naye disco MH huyu pale Tazara, watoto wadogo walipolivamia wengine tulijihuzuru, mwenzetu Kikwete ambaye kwa umri ni braza etu bado anajirusha?
   
 18. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kuendelea kukaa kimya kwa rais kuhusu suala la umeme ni dalili moja kubwa kwamba kazi tuliyo mpa ya kuongoza nchi imegeuka kuwa zigo zito la kumlemea.

  Tumejikaanga kwa mafuta yetu wenyewe.
   
 19. K

  Konzogwe JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 441
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  THANK U MAGGID,KUTUJULISHA,SI VIBAYA SISI KUJUA MR PRESIDENT ALIKO AFTER ALL HE IS MORTAL CREATURE AS U N' ME HAKUNA NOMA ON THAT.NINALOMWOMBA MR PRESIDENT NI HILI:-Kuna tatizo sugu la maji pale mikumi ambalo lilimshinda Lowassa,Makamba, Karembo na wengine. Kuna 200million toka WORLD BANK huenda zimeliwa.Then aulize kuna somebody ZUNDA is very stubborn na huyu ndo hao waheshimiwa wamemshindwa. Naamini mzee kwa kuwa yupo pale akikohoa hakuna litakaloshindikana.
   
 20. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Rais akiwa kimya tunasema serikali ina usiri mkubwa tukijulishwa tunasema haina umuhimu na mustakabali wa taifa letu, inabidi akapumzishe kichwa baada ya kupeleka vijana wetu kwenye operation ya kumtoa Bacar madarakani, unafikiria ni decision ndogo hiyo?
   
Loading...