Kiufupi tu.
Ndugu zangu huwa mnafanyaje mnapojua kimada wa pembeni kapata mimba/kajifungua na mtoto ni wako? Sitaki kuona damu yangu hii inateseka wakati uwezo wa kuihudumia ninao, tatizo huwa mnafanyaje ili mke asijue na huku mtoto akipata matunzo yote ya baba?
Hapa najua nimemkosea sana mke wangu ni mrembo na ana kila kitu, lakini sihitaji mtu anilaumu kwa hilo, ni makosa yameshatokea. Wanaume nipeni mbinu ndugu zangu nini nifanye, mimi sihitaji kutelekeza damu yangu.
Binafsi nimenunua kiwanja nataka nimjengee huyu mtoto akaishi huko na mama yake, baadhi ya watu wamenishauri nisikurupuke kwa huo uamuzi, ushauri wenu wanaume wenzangu huwa mnafanyaje kwenye hali kama hii?