Kabla ya kuingia kwenye Mahusiano tufanye uchaguzi wa Kina

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Naomba tujengane kwenye masuala ya mahusiano. Majuzi nilicheki uzi ambao watu wanasema kataa ndoa, wengine wanalaumu, wengine wanaponda ndoa na wengine wanazisifu, mimi binafsi nilijenga hoja zangu na watu wakadai nimewabomoa! Yaah! Sometimes inabidi tubomoe ili tujenge kitu imara zaidi.

Fanya maamuzi yako ya hovyo katika maisha yako lakini maamuzi ambayo utatakiwa kutulia zaidi ni kutafuta mwenza wa maisha yako. Wengine hatujaoa kwa sababu hatujatulia, si kutokutulia kwa kuwa na wanawake, hapana, kutokutulia na kuanza kumtafuta mwenza wa dhati.

Kwenye mahusiano, kitu cha kwanza epuka sana kuingia kwenye ndoa na mtu ambaye hujafahamiana naye vizuri. Ni lazima umjue mtu unayetaka kumuoa, yupo vipi, ni lazima ujue hata life style ambayo yupo nayo mtaani kwao.

Tatizo letu huwa ni moja tu, utamsikia kijana: “Yaani mimi Rutashobya na wewe Kokubanza tunaanzia hapa, yaliyopita yamepita, tugange yajayo. Hata kama umetembea na wanaume 50, mimi sijali.”

Bro! Kuna watu waliosema hivyo ambao sasa hivi wanalia na wengine kujimaliza. Unatakiwa kumfahamu kiundani mtu ambaye unataka kuingia naye kwenye ndoa, utamfahamu vipi? Cha kwanza jenga urafiki naye.

Jiruhusu kuwa karibu naye, uwe rafiki yake, kwenye urafiki huo ataanza kukushirikisha mambo yake mengi, utamfahamu kwa undani na hata utakapotaka kumuoa, utajua ni nani unakwenda kumuoa.

Hatuoi marafiki! Tunakutana na mwanamke, ndani ya mwaka tu, umemvarisha pete, mara umemuoa, mwisho wa siku unakuja kugundua umefanya kosa kubwa sana.

Asili ya binadamu ni unafiki, ukiwa naye atakuficha mengi tu, ila hawezi kukificha kama utaanza kuwa na urafiki naye.

Tembeeni mitaa ya wanawake wenu kwanza msikie stori zao. Kuna mwanamke unaweza kuoa, wazazi wake wakaona kama wametua gunia la misumali. Usijifanye shababi eti naflashi yote yaliyopita, bro! Mengine hayaflashiki kwa sababu yatakuja kukuumiza huko mbele, utake usitake.

Binadamu hawezi kuacha asili yake, ukioa ama kuolewa na malaya usijidanganye eti kuna siku atabadilika. Hakuna mtu anayebadilika wakati damu bado inachemka. Mwanamke akiwa malaya, umri wa kubadilika na kutulia ni miaka 35. Wa kwako amefika miaka hiyo?

Kwa mwanaume akiwa malaya siku ya kubadilika ni ile tunapokwenda kumpeleka makaburini kumzika. Kuna tabia mtu hawezi kubadilika hata iweje, mwanamke anabadilika kwa kuwa umri umechoka, amekwisha, anaona bora atulie, ila kwa mwanaume hilo jambo sahau.

Ndoa nyingi za siku hizi zinasumbua kwa sababu watu hawakuwahi kuwa marafiki. Ukiuliza, utasikia yule nilikutana naye, tukawa wapenzi na tukaoana, hii ni mbaya sana.

Wanawake sina cha kuwaambia kwa sababu nyie huwa mnaolewa bila hata maamuzi yenu. Yaani rafiki zako tu wanaweza kukuuliza mbona huolewi? Akija mhuni yeyote mbele yako, unaona bora tu uolewe ili usiulizwe tena.

Wengi hawajaolewa kwa maamuzi yao, waliendeshwa na presha za nyumbani, mtaani, walizungumziwa vibaya, hivyo wakaolewa na watu wasiowahitaji kwa sababu tu ya presha zilizowaendesha.

Pamoja na hayo yote, ndugu yangu kumbuka jambo moja. UZINZI NA ULAWITI NI DHAMBI YENYE KISASI.

Hapa namaanisha nini! Kama wewe uliwahi kulala na mke wa mtu kwa namna yoyote ile, kuna siku isiyo na jina jamaa fulani atakuja kulala na mke wako, tena Mungu alivyo fundi, utakuja kulijua hilo na hutakuwa na nguvu ya kumuacha. Itakutafuna mpaka kifo chako.

Kama uliwahi kutembea na mume wa mtu, siku ukiolewa, kuna mwanamke atakuja kutembea na mume wako, na utajua kabisa kwamba mumeo anatembea na mwanamke mwingine.

Kama wewe ni mfiraji, kazi kufira watoto wa kiume wa wenzako, nikwambie tu bro mtoto wako atakuja kufirwa, yaani utake usitake. Nenda kaulize stori za wazazi wa mashoga, wana mengi ya kukwambia.

Yaani kila kitu kiovu utakachokifanya, kina malipo yake hapahapa. Kama uliwahi kuua, damu itakulilia tu, kuna siku utakuja kuuliwa, yaani upanga kwa upanga. Kama ulimtesa mtoto wa watu aliyekuja kuishi kwenu, jua kabisa watoto wako watakwenda kuteswa huko mbeleni.

Mungu ameipa karma hii dunia kwa kumaanisha kwamba kila ukifanyacho kitazunguka humuhumu ndani, hakitotoka. Lolote utakalolifanya, litakurudia wewe ama uzao wako.

Unasikia tu baba alikuwa malaya kweli, na mtoto naye karithi kawa malaya. Unasikia mzee yule alikuwa mwizi sana, halafu na mtoto wake naye kawa mwizi. Kila kitu kiovu ukifanyacho, kitakuja kukurudia kwa staili hiyohiyo.

Ni vizuri kujua historia ya familia ya mtu unayetaka kuolewa naye ama kumuoa. Kuna familia zingine zimerithi mizimu, kuna familia nyingine zina magonjwa ya kurithi, kuna familia zingine mtu akifikisha miaka 50 tu lazima awe kipofu. Unatakiwa kuchunguza hayo yote, sio unajiolea tu halafu baadaye unasababisha matatizo makubwa zaidi.

Kaa na mtu, kuwa rafiki yake, mchunguze, tafuta hata stori za mtaani kwao hasa kwa bodaboda, ujue kabisa sio kujiolea tu.

Hii inanikumbusha mwaka 2019 jamaa alinifuata na kuniuliza kuhusu msichana fulani wa mtaani kwetu. Alijifanya wakala wa vitabu ila alitaka kumjua zaidi huyo msichana kupitia mimi. Na mimi sina ajizi, nikamsifia sana, tena sana tu na leo yumo ndani ya ndoa.

Bro! Usiendeshwe na presha ya kuoa, kabla ya kufanya maamuzi, chukua huo ushauri wangu. Kuna mtu leo mwezi mzima hana raha na ndoa yake. Watu wengi waliooa, ukiwaambia wakushauri, swali pekee watakalokuuliza: “UTAWEZAAAA?”

Humo ndani ni pagumu. Ukikosea kuoa ni sawa na kununua kifo chako, kuukaribisha umasikini kwenye maisha yako, kuzima ndoto zako, kuingiza huzuni na majonzi maishani mwako, kukutenganisha na Mungu wako ama kuleta furaha na utajiri maisha yako yote.

KUWA MAKINI KWENYE UCHAGUZI.

#kakaameongea
 
JamiiForums-553690719.jpg
 
Kwa kweli shida kubwa kwenye ndoa huanzia kwenye kuchagua

Wengi tunafanya wrong selection kisha baada ya kupata maumivu ndio tunakuja kugeneralize kuwa ndoa ni utapeli,nk

Kumbe sisi wenyewe tumechagua matapeli
 
Lakin mkuu mm nina hoja,unasema dhambi ya uzinzi na ina tabia ya kurithi?je huoni haya tunayoyafanya Sisi ni sehemu ya karma kwamba hatuwezi kuepuka?
 
Ujinga ni pale mshazini mpaka kupata mtoto halafu mnaenda kuhalalisha uzinifu eti kubariki ,mnaona aibu kwa vile mshazaa.
20231222_192158.jpg
 
Mkuu ahsante kwa kutuelimisha,somo zuri sana,lakini kuna hoja nataka tuwekane sawa.1 Swala la mtu kubadilika,nina uhakika asilimia mia,mtu huwa anabadilika ila kosa wanalofanya watu ni kumkuta mtu anatabia flani isiyoridhisha halafu anasema ntambadilisha,Hilo ndio tatizo lilipo,kila kitu kina hatua,kwaiyo ni vyema umjue mtu vzuri kama ulivyosema ndio umchumbie kwa kuridhika na jinsi alivyo na sio kutegemea utambadilisha,yani kama umekuta ni mlevi weka kichwani yeye ni mlevi,lakini pia mtu anaweza kubadilika kutoka kuwa mzuri kitabia mpaka kuwa mbaya.2 Swala la karma,hili swala wengi mnaliongea sana lakini halina ukweli,Mungu sio wa visasi,bro Mungu akikusamehe anafuta mpaka kumbukumbu kuwa uliwai kumfanyia kosa tofauti na wanadamu wanaosamehe lakini Bado wanakinyongo moyoni,unafahamu mtume Paulo kabla ya kuwa mkristo alifanya maasi kiasi gani? Unawezathibitisha kama karma ilimpata?, Kila mtu anabeba msalaba wake,kosa ulilofanya wewe,mwanao hawezi kuhukumiwa nalo,mifano uliyotoa ya mzazi muhuni na mtoto kuwa muhuni ni Kutokana na mazingira ya kumlea mtoto,ukizingatia ni kwamba watoto wanawaiga zaidi wazazi kulingana na matendo yao na siyo maneno,,ila hayo mengine uliyoyasema nakubaliana na wewe
 
Kwa kuongezea ni kwamba kosa ambalo wengi wanalifanya ni kutongoza kwanza halafu ndio wanaanza kuchunguzana,hahahah hapo huwezi kumjua mtu maana atakuwa anaigiza si anajua anafwatiliwa! So anza kuwa rafiki wa kawaida ili awe huru kwako,then ukijiridhisha baada ya muda ndio uombe urafiki wa kimapenzi,one love members.
 
Back
Top Bottom