Nimemkosea sana mke wangu. Ushauri wenu tafadhali

Paploman

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
1,437
2,000
Kiufupi tu.

Ndugu zangu huwa mnafanyaje mnapojua kimada wa pembeni kapata mimba/kajifungua na mtoto ni wako? Sitaki kuona damu yangu hii inateseka wakati uwezo wa kuihudumia ninao, tatizo huwa mnafanyaje ili mke asijue na huku mtoto akipata matunzo yote ya baba?

Hapa najua nimemkosea sana mke wangu ni mrembo na ana kila kitu, lakini sihitaji mtu anilaumu kwa hilo, ni makosa yameshatokea. Wanaume nipeni mbinu ndugu zangu nini nifanye, mimi sihitaji kutelekeza damu yangu.

Binafsi nimenunua kiwanja nataka nimjengee huyu mtoto akaishi huko na mama yake, baadhi ya watu wamenishauri nisikurupuke kwa huo uamuzi, ushauri wenu wanaume wenzangu huwa mnafanyaje kwenye hali kama hii?
 
Pep

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
694
1,000
Nakosa cha kukushauri mkuu

Ila, one thing is certain, kwa ulichokifanya unetengeneza mazingira mazuri sana ya mke wako nae pia kutoka nje.

Yeye anaweza asipate mtoto huko nje, ila pia akipata hutafahamu na utamlea upende usipende.

All in all, you've made your bed...now lie in it

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mzee niko kikazi mbali na familia yangu, sikutegemea kupata mtoto nje ya ndoa lakini ndio hivo sasa nawezaje kuitelekeza hii damu yangu isiyo na hatia
 
Ligogoma

JF-Expert Member
Aug 27, 2010
3,039
2,000
Hakuna siri ya wawili jombaa, itamfikia tu mkeo kama si leo basi kesho! Kikubwa ni kujiandaa kukabiliana na chochote atachoamua mkeo ila tu usimnyanyase kwa kosa lako!

Back to the topic: Hapo sasa kama ulikuwa mapato yako unayaweka wazi kwa mkeo inabidi uanze kuficha ficha ili ulee mtoto wa pembeni.

Kama nguvu ya kumjengea ipo, mjengee na pia kama mama ana akili nzuri mfungulie biashara kwa mpango wa kupunguza usumbufu wa kutuma matunzo mara kwa mara, utashtukiwa mapema na mkeo.

Mpango wa kando unatakiwa baba uwe na majukumu makubwa na ya msingi tu kama ada (akianza shule) na/au ataumwa!
 
Paploman

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
1,437
2,000
Hakuna siri ya wawili jombaa, itamfikia tu mkeo kama si leo basi kesho! Kikubwa ni kujiandaa kukabiliana na chochote atachoamua mkeo ila tu usimnyanyase kwa kosa lako!

Back to the topic: Hapo sasa kama ulikuwa mapato yako unayaweka wazi kwa mkeo inabidi uanze kuficha ficha ili ulee mtoto wa pembeni.

Kama nguvu ya kumjengea ipo, mjengee na pia kama mama ana akili nzuri mfungulie biashara kwa mpango wa kupunguza usumbufu wa kutuma matunzo mara kwa mara, utashtukiwa mapema na mkeo.

Mpango wa kando unatakiwa baba uwe na mahitaji ya msingi tu kama ada (akianza shule) na/au ataumwa!
mkuu hayo sio tatizo kabisa, ninachohitaji ni familia yangu isijue haya, nifanyeje?
 
Pennstatepro

Senior Member
Nov 22, 2019
182
250
Jamaa wala usiwe na pressure, hyo ni kesi ndogo sana ushauri wangu kwako sasa;

Kwanza, waeleze wazazi wako ukweli maake ndo miungu yako ya hapa duniani.

Pili, Usimweleza mkeo chchte, nature itajibalance yenyewe tu siku za hapo usoni maake mwisho wa siku itajulikana tu.

Tatu, huyo mtoto wa nje anza kumuandalia mahali pake na vitu vyake, kama kujenga fanya hivo ila mamaake asijue chochote kuhusu hayo.

Nne, Wazo lako la kumjengea nyumba huyo mwanamke na mwanae wakaishi ninapnga vikali,atajihesabu yeye ni nyumba ndogo.

Tano, Usirudie tena hilo kosa na ukome kabsa michepuko......leo umeleta mtoto, kesho utaleta ukimwi na vurugu kubwa ndani ya ndoa.

Asante
 
Paploman

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
1,437
2,000
Jamaa wala usiwe na pressure, hyo ni kesi ndogo sana..............ushauri wangu kwako sasa;

Kwanza, waeleze wazazi wako ukweli maake ndo miungu yako ya hapa duniani.

Pili, Usimweleza mkeo chchte, nature itajibalance yenyewe tu siku za hapo usoni maake mwisho wa siku itajulikana tu.

Tatu, huyo mtoto wa nje anza kumuandalia mahali pake na vitu vyake, kama kujenga fanya hivo ila mamaake asijue chochote kuhusu hayo.

Nne, Wazo lako la kumjengea nyumba huyo mwanamke na mwanae wakaishi ninapnga vikali,atajihesabu yeye ni nyumba ndogo.

Tano, Usirudie tena hilo kosa na ukome kabsa michepuko......leo umeleta mtoto, kesho utaleta ukimwi na vurugu kubwa ndani ya ndoa.

Asante
mkuu hapo namba tatu umesema nimjengee huyo mtoto then mama yake asijue chochote, hii nyumba nitamkabidhi nani? nieleweshe hapa ndugu..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom