Nimelikoroga

Nimelikoroga

Si kila unachokijuwa kimekukuta wewe... Mbona huwa tunajuwa gari ikikugonga unaweza ukafa, je tuliwahi gongwa na magari na tukafa..???

si kwa sababu huwa tunaona watu wanakufa? sasa wewe huo ushirikiano wanaoutoa wanaobakwa uliuona wapi?
 
Ohoo... kumbe tatizo ni kuonyesha mabadiliko kwa mkewe. Asingeonyesha poa tu, sio? Samahani nimevamia uzi wako bila kukaribishwa.

Wanaume wenzangu njooni mjisomee wenyewe wanachokitaka wanawake...
sio poa hata kidogo. maana yangu ni kwamba asingeonyesha mabadiliko mimi asingejisumbua kutafuta ukweli na pengine mimi nisingeingia katika mgogoro huu.
 
Kaa nae chini uongee nae kila kitu,kumkimbia si suluhu.

Hakikisha mtakapo ongelea kuna watu maeneo hayo.

nilikuwa nataka kumkwepa kwa muda si unajua hawa watu akiwa hasira aweza sababisha maafa bure.
 
Fursa nzuri hizi shem! Hata kaka yangu atafurahi akijua nimekusaidia...

Na weweeeeee...ntakuita kikao jioni ujue!!!!:frusty:

hahaha sa si ka usuluhishu ulikuwa wafanyikia sebuleni hao tutahamia chumbani ili tusuluhishe vizuri
 
Pole sana,,,, jioni ndo hiyo imefika sipati picha ulivyonywea.. Hahahahahaha!!!!!!!"!!!
Huna haja ya kuzua safari we kwenye kikao uwepo kama una mume awepo or mpenzi wako ili kuepusha huyo jamaa asikuonee kivile.
 
Usingemwambia tu. Hapo hapakufai tena. Kama umepanga nipange kuondoka. Na kama jamaa yuko jf je?
 
Pole mdada, omba tu huyu asiwe ni member humu maana mhh! Kama walivyo shauri wengine usionane nae ukiwa mwenyewe, mi nahisi anataka kukutumia umtetee kuwa yanayosemwa ni uongo kwani wewe ndo jirani!
 
Kwanza chagua cenue

Pili usimwe mwenyewe

Tatu kataa kata kata tena mpige biti mwambie mambo ya nyumba na ndoa yake hayakuhusu na akome kukuhusisha
 
Pole sana,,,, jioni ndo hiyo imefika sipati picha ulivyonywea.. Hahahahahaha!!!!!!!"!!!
Huna haja ya kuzua safari we kwenye kikao uwepo kama una mume awepo or mpenzi wako ili kuepusha huyo jamaa asikuonee kivile.
ndio hivyo ma dia namsubiri arudi ili nijue mbivu na mbichi ila ki ukweli ninaogopa, isingekuwa jf sijui ningefanyaje.
 
Kwanza chagua cenue

Pili usimwe mwenyewe

Tatu kataa kata kata tena mpige biti mwambie mambo ya nyumba na ndoa yake hayakuhusu na akome kukuhusisha

ahsante mpenz siwez toka nje na hapa kwangu akija ntamwambia maongezi ni hapahapa nyumbani
 
Pole mdada, omba tu huyu asiwe ni member humu maana mhh! Kama walivyo shauri wengine usionane nae ukiwa mwenyewe, mi nahisi anataka kukutumia umtetee kuwa yanayosemwa ni uongo kwani wewe ndo jirani!

mwenzangu, kweli umenena ukute naogopa bure tu.
 
Pole DEMBA,kwanza nikupe hongera kwa kumwambia huyo mwanamke ukweli maana siku zote hizo ulikuwa unashiriki na huyo mwanaume kwenye dhambi!Ukweli ni mchungu,lakini wakati mwingine tunatakiwa kupindisha ukweli!Msubiri huyo jamaa then simamia msimamo wako wa awali kuwa hujamwambia mkewe,tena mwambie akome mambo yake ya ndoa kuyaleta kwako!Kama unaogopa kuongea naye muombe Kaizer aje kwako, atakuwa barazani anakunywa zake soda wakati nyie mnaongea sebuleni!Ukikwepa kuongea naye atajua hisia zake ni za kweli na ataanzisha uhasama!
 
Last edited by a moderator:

Kaizer umesikia?? njoo unilinde bana in case of anything
 
Last edited by a moderator:
heshima yenu wana MMU
hapa nilipo kichwa kimenivurugika naomba ushauri wenu na faraja pia.

ni hivi ninaishi nyumba moja na jamaa na mke wake (ni wakurya). ni mwaka na miezi kama kumi hivi mke hayupo yupo jijini Nairobi kimasomo. sasa tangu mke ameondoka jirani yangu kaleta msichana mwingine anaishi naye kama mke na mume. miezi sita iliyopita mke alinipigia simu na kuniuliza kama mumewe anaishi na mtu kwani amebadilika sana na mawasiliano yanasuasua, mimi nikamjibu kwamba mimi niko bize sana si rahisi kujua anavyoishi. wiki moja baadaye akanipigia tena kunisihi nimwambie ukweli kwani amepata taarifa kwamba mumewe anamsaliti. mimi nikamwambia niko safarini hivyo sijui kinachoendelea.
kwenye mwezi wa kumi hivi alinipigia tena simu kuniuliza hayohayo mi nikamwambia kama anahisi chochote aje mwenyewe ajiridhishe na nikakata simu. leo asubuhi kanipigia na kunisimulia namna anavyopata shida huko chuoni kwani mumewe amekuwa mgumu kutoa huduma, kiasi kwamba anashindwa hata kurudi likizo kwani hana hata nauli na taarifa alizonazo ni kwamba mumewe anaishi na mtu ila mtu aliyemwambia hamuamini sana kwani ni mwanaume ambaye huwa anamtaka. basi nikaingiwa huruma kubwa nikajikuta namwambia ukweli kwamba kuna mtu anaishi naye. ila nikamuonya asinitaje coz sitaki matatizo.
kumbe baada ya kuongea na mimi tu akampigia mumewe na kumwambia kwamba anavunja ndoa.

sasa huyu jirani anahisi mimi ndiye niyemwambia na amenipigia simu (akiwa anatetemeka kwa hasira) kuniuliza kama nimeongea na mke wake. mi nimeruka kimanga, amedai anakuja tuongee vizuri jioni.
mimi nimeamua sitaki kukaa hicho kikao. na nimepanga kuzua safari coz naogopa kupigwa panga.
wenzangu mnanishauri nini?
KUMBUKA: TUKIO LIMESHATENDEKA LAWAMA HAZITANISAIDIA KWA SASA.
cc Sista Kaizer Heaven on Earth mwekundu Munkari charminglady gfsonwin 'Valentina' Mapi Mkoroshokigoli farkhina na wadau wengine

Wewe mwambie mie nimemwambia huwa namwona dada fulani anaingia na kutoka, na huenda ni housegirl.
 
Back
Top Bottom