Nimelikoroga

Nimelikoroga

heshima yenu wana MMU
hapa nilipo kichwa kimenivurugika naomba ushauri wenu na faraja pia.

ni hivi ninaishi nyumba moja na jamaa na mke wake (ni wakurya). ni mwaka na miezi kama kumi hivi mke hayupo yupo jijini Nairobi kimasomo. sasa tangu mke ameondoka jirani yangu kaleta msichana mwingine anaishi naye kama mke na mume. miezi sita iliyopita mke alinipigia simu na kuniuliza kama mumewe anaishi na mtu kwani amebadilika sana na mawasiliano yanasuasua, mimi nikamjibu kwamba mimi niko bize sana si rahisi kujua anavyoishi. wiki moja baadaye akanipigia tena kunisihi nimwambie ukweli kwani amepata taarifa kwamba mumewe anamsaliti. mimi nikamwambia niko safarini hivyo sijui kinachoendelea.
kwenye mwezi wa kumi hivi alinipigia tena simu kuniuliza hayohayo mi nikamwambia kama anahisi chochote aje mwenyewe ajiridhishe na nikakata simu. leo asubuhi kanipigia na kunisimulia namna anavyopata shida huko chuoni kwani mumewe amekuwa mgumu kutoa huduma, kiasi kwamba anashindwa hata kurudi likizo kwani hana hata nauli na taarifa alizonazo ni kwamba mumewe anaishi na mtu ila mtu aliyemwambia hamuamini sana kwani ni mwanaume ambaye huwa anamtaka. basi nikaingiwa huruma kubwa nikajikuta namwambia ukweli kwamba kuna mtu anaishi naye. ila nikamuonya asinitaje coz sitaki matatizo.
kumbe baada ya kuongea na mimi tu akampigia mumewe na kumwambia kwamba anavunja ndoa.

sasa huyu jirani anahisi mimi ndiye niyemwambia na amenipigia simu (akiwa anatetemeka kwa hasira) kuniuliza kama nimeongea na mke wake. mi nimeruka kimanga, amedai anakuja tuongee vizuri jioni.
mimi nimeamua sitaki kukaa hicho kikao. na nimepanga kuzua safari coz naogopa kupigwa panga.
wenzangu mnanishauri nini?
KUMBUKA: TUKIO LIMESHATENDEKA LAWAMA HAZITANISAIDIA KWA SASA.
cc Sista Kaizer Heaven on Earth mwekundu Munkari charminglady gfsonwin 'Valentina'
Mapi Mkoroshokigoli farkhina na wadau wengine

Sasa unaingia mkoa wa Mara
 
Last edited by a moderator:
Kaa nae chini uongee nae kila kitu,kumkimbia si suluhu.

Hakikisha mtakapo ongelea kuna watu maeneo hayo.
 
me kwakweli taarifa kama hii usinipe........yaani ukisema

usimwambie kama ni mimi ndio unakuwa ka wanisisitiza nikutaje kabisaaaa
Na huwaga wanachagua vya kusema hao... unadhani angekuwa anagegedwa na huyo mkurya wake angemwambia mkewe...???
 
Mie sijaelewa vizuri hiyo nyumba mnaishi wewe na huyo jamaa tu,?
na kwanini huyo dada aendelee kukuuliza wewe tu? au mnakauhusiano
furani?, hiyo siri unaiiua wewe na huyo mpangaji mwenzio?

hii nyumba tunaishi mimi na hawa wakurya. amenihisi mimi tu coz. majirani huko nje hatuna mazoea nao .
 
Ukisikia ufataani ndio huo.

Kiranga komo. Iwe fundisho kwako na kwa wengineo. Siku nyingine funga macho, mdomo na masikio kwa yasiyo kuhusu.

Umelikoroga sasa linywe.

Hii tabia ya kufumbia macho kila kitu ndio inatumaliza sio kwenye ndoa tu mpaka kwenye malezi ya watoto na taifa kwa ujumla..
Unaona mwenzio anahujumiwa unakaa kimya kisa hayakuhusu, unaona mtoto wa mwenzio anamegwa na kibabu kimya kisa mtoto wa mwenzio mkubwa mwenzio..huko kwenye maofisi unaona mwenzio anaua kampuni kimya kisa kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake.

Ukweli unamuweka mtu huru na kama kuna mtu anavunja ndoa hapo sio wewe bali ni huyo mume msaliti...
Mtu mpaka hamtumii matumizi mkewe hata ingekuwa mie roho ya huruma ingenipata ningesema tu tena mie ningemtumia nauli aje afumanie....

Kuna haja gani ya kumlinda mtu aliyekosa ustaarabu kiasi hicho si angefanyia umalaya wake huko nje.
 
umeongea kweli Nambe tabia ya kufumbia macho uovu ndio inayotucost waafrika.
 
Last edited by a moderator:
DEMBA ndg yng sinilikukataza lkn?

haaa haaaa SUZANE nimeshindwa kuendelea kulea uovu. ndio vizuri hata kufanya atafanya kistaarabu na sio kumdhalilisha mkewe kiasi hiki.
 
Last edited by a moderator:
haaaa haaaaa hakatwi mtu hapa.
Ukiwekewa panga utakatwa tu... Kwanza mwanzo tu ndo huwaga mgumu... hata anayebakwa naye anabisha mwanzoni tu huko kunakoendelea wanatoaga ushirikiano usipime
 
Ukiwekewa panga utakatwa tu... Kwanza mwanzo tu ndo huwaga mgumu... hata anayebakwa naye anabisha mwanzoni tu huko kunakoendelea wanatoaga ushirikiano usipime
haaa haaa wewe umejuaje? ulishawahi kubaka?????
maana waswahili walisema "aisifiye mvua imemnyea" ww utajuaje habari za mvua kama haijawahi kukunyeshea
 
nashangaa mwenzangu kuniletea hasira zake. tatizo huyu jamaa ameshindwa kula na kipofu. alipaswa kutoonyesha mabadiliko yoyote kwa mkewe.

Ohoo... kumbe tatizo ni kuonyesha mabadiliko kwa mkewe. Asingeonyesha poa tu, sio? Samahani nimevamia uzi wako bila kukaribishwa.

Wanaume wenzangu njooni mjisomee wenyewe wanachokitaka wanawake...
 
haaa haaa wewe umejuaje? ulishawahi kubaka?????
maana waswahili walisema "aisifiye mvua imemnyea" ww utajuaje habari za mvua kama haijawahi kukunyeshea
Si kila unachokijuwa kimekukuta wewe... Mbona huwa tunajuwa gari ikikugonga unaweza ukafa, je tuliwahi gongwa na magari na tukafa..???
 
Ohoo... kumbe tatizo ni kuonyesha mabadiliko kwa mkewe. Asingeonyesha poa tu, sio? Samahani nimevamia uzi wako bila kukaribishwa.

Wanaume wenzangu njooni mjisomee wenyewe wanachokitaka wanawake...

nahitaji maombi hali yangu si nzuri
 
Back
Top Bottom