Nimekwisha na UKIMWI

Nimekwisha na UKIMWI

Baba Mungu wetu akutangulie kwenye lolote ambalo mapenzi yake... Lakini zaidi akupe ustahimilivu na hekima ya kuenenda hilo

germve himself
 
mkuu usijifanye kama upo smart sana,haya yamenikuta ila na wewe siku yako inakuja hasa kama una aamini ukiwa kwenye ndoa ndio utakuwa salama,nimekiri makosa yangu,lkn pia kuishi nae miaka 3 nilimaanisha kuwa nae kwenye mahusiano,sikuwa sawa kipindi naandika,nilipanga kuanza kuishi nae baada ya ndoa,naomba usinihukumu hasa kama bado upo hai,lolote nawe laweza kukutokea,tena huwenda likawa baya zaidi ya hili la kwangu,kinachonipa moyo ni kwamba wiki tatu zimepita kuna mdogo wa rafiki yangu nilimtolea damu,na nahisi hadi wakaniruhusu nitoe inamaanisha ilikuwa salama,kesho ndio siku ambayo tajua mbivu na mbichi,nahisi kwa sasa nahitaji faraja zaidi na si kejeri,hii ishu haina mwenyewe,tuombe uzima kesho nitarejesha nitakachotoka nacho maabara...all in all nimefarijika sana kwa wana JF wengi kwa kuwa watu dynamic,mnajua jambo la utani na jambo ambalo ni serious,imenipa moyo sana na narudia kushukuru kwa wote mliooonyeshwa kuguswa na tatizo langu,ki`zaidi mlionifuata PM na kunipa msaada wa mawazo na kila kitu...
sikulaumuhata kidogo mkuu,dunia inaangamia kwa kukosa maadil,tukirudi kwa mungu haya yote hayatakuwepo,unaweza kuchangia damu tu lakini baadaye inatupwa maana unakuwa umeendaa kuchangia sio kupima afya!
 
Aise pole. Hiyo ni mojawapo ya machungu ya dunia hii. Bado una nafasi ya kuishi na kufanikiwa katika ndoto za maisha. Nenda kapime, pia kubali matokeo utakayo ambiwa. Sasa usisahau kutumia condom unapokutana na mkeo au mwanamke mwingine.kwa Ushauri zaid nitafute kwa 0752640448

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kinachonipa moyo ni kwamba wiki tatu zimepita kuna mdogo wa rafiki yangu nilimtolea damu,na nahisi hadi wakaniruhusu nitoe inamaanisha ilikuwa salama

Pole sana mkuu, ila kama mpenzio alizaliwa nao mpaka yeye anazaa bado yupo jua tu huo sio mwisho wa maisha.

Kuhusu kutoa damu kusikuaminishe kama damu inafaa au haifai, kwa sera ya utoaji damu ili kupunguza kunyoosheana vidole damu hutolewa kwa wote halafu baadae ndiyo vipimo vya magonjwa maambukizi ya damu hufanyika na ikikutwa ina maambukizi basi huharibu damu husika. Japo kwa kawaida wachangia damu hupaswa kurudi kuchukua majibu yao.

Muhimu ni kupima, nenda kapime
 
Kuna kitu hapa hakiko sawa. Kama kweli Huyo mkeo hakujua kama alizaliwa nao je kipindi anaanza clinic hakupima? Mana Mama anapoanza clinic lazima apime maambukizi Kama hayo
Kama alipima akajua ukweli 'na hakukwambia una uhakika gani alizaliwa nao? Kama kakuficha umekuja Kujua Leo huwez kusema alizaliwa nao Huyo alikuwa anajijua Zamani tu aliamua kukuficha Sema imefika muda meb hawez Tena kukuficha ndio kaona aseme alizaliwa nao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bro ukimwi ulikuwa miaka ya 80 sio siku hizi,,,kikubwa usipanic relax wala usimlaumu coz nae hakujua,,ukifuata masharti nakuhakikishia utazeeka salama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kwa roho mbaya ila kumuoa mtu aliyeficha siri kama hii duuh yataka moyo inaonekana unampenda sana maana mpaka uongo wake umeuamini kabixaa kwamba alizaliwa nao. Kwani ulimkuta bikira, mie hainiingii akilini kama alikuwa hajijui noway. Hebu fuatilia alipoanza clinic hakupima? Navyojua mimi kwa Sasa Hospital nyingi kama si zote ukianza clinic tu lazima upime VVU. Huyo namwita silent killer bhana sidhan kama anafaa Kuwa mke anaweza hata kukupa sumu ujifie kimya kimya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Mkeo" kakudanganya! Hajazaliwa nao, kaupata ukubwani, uliingia cha kike. Pole sana. Stori yako inafanana sana na ya ndugu yangu mmoja. Never ever pima kwa macho, never ever do this mistake ya kumuamini mtu kwa kumpima kwa macho!
 
Duuh! mkuu,huyo mpenzi wako sidhani kama alizaliwa nao halafu hakujua,mi nina uhakika kama kweli alizaliwa nao itakiaje afike umri wa kiutu uzima kabisa asiwe anatumia hata ARVs,huyo mtu ana kinga ya namna gani hadi asinyong'onyezwe..,na vilevile wakati anaenda kliniki inamaana hakuwahi kupima?

Aache ukatili ameshakuua tayari,na mbaya zaidi umenikumbusha kifo cha binamu yangu aliyekua kaathirika,amezikwa juzi tu,HIV is real.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wanaozaliwa nao ukimwi hua tofauti sana naongea hili kwa sababu nimelishuhudia

Weng hua unaasumbua utotoni bt kuna mda una stop unakua kama unajificha na anaendelea kuish maisha ya kawaida sana hata kiafya unaweza usimtambue

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aise pole. Hiyo ni mojawapo ya machungu ya dunia hii. Bado una nafasi ya kuishi na kufanikiwa katika ndoto za maisha. Nenda kapime, pia kubali matokeo utakayo ambiwa. Sasa usisahau kutumia condom unapokutana na mkeo au mwanamke mwingine.kwa Ushauri zaid nitafute kwa 0752640448

Sent using Jamii Forums mobile app
takutafuta kesho mkuu,nashukuru...kesho nikiamka nitaenda hospital kumcheki huyo mwanamke ameamkaje then nikitoka hapo naenda kupima,majibu nitakayoyapata nitayaweka hapa wakuu,nasisitiza tuwe makini,mjifunze kutokupitia niliyopitia mimi,hata kama bado sijajua majibu yatakavyokuwa hiyo kesho..
 
Back
Top Bottom