Nimekwisha na UKIMWI

Nimekwisha na UKIMWI

Naandika huku hali yangu ya akili ikiwa mbaya sana, mchumba wangu niliyeishi nae kwa miaka mi 3 amejifungua jana kwa upasuaji, na mwezi November mwaka huu ilikuwa tufunge ndoa.

Ndugu jamaa na marafiki wote tushawatangazia na vikao viwili vya ndugu kujiweka sawa vishafanyika, nimeenda leo asubuhi nimekutana na habari tofauti kuwa mke wangu ni MUATHIRIKA na kibaya ni kwamba alizaliwa nao.

Nimemuuliza kwanini hakuwahi kuniambia tangu mwanzoni, anasema na yeye alikuwa hajui, kesho na mimi nataka nikapime kama hospital 5 hivi ili nijue hali yangu, mwenye lolote la busara naomba anishauri na kunipa moyo, hivi inawezekana majibu ya kesho yakaniacha salama kweli?

Kubwa nawakumbusha wote kamwe usirudie kosa nililofanya mimi la kumwamini huyu mwanamke, tayari nimeshafanya kosa naomba nisilaumiwe.

Nishaurini vizuri nifanyaje kwa sasa, bado sijamwambia ndugu wala rafiki yeyote juu ya hili, nasubiri nipime kwanza ili nijue hatima yangu, nikipima nitareta mrejesho kwa litakalokuwa nimelipata huko.

Ahsanteni
Mkuu hayo ni mapito utatoka salama kwa kua hukujua hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
To live is to suffer,to survive is to find some meaning in the suffering!
 
Tulia kwanza mkuuu endelea na mambo yako jiaminishe Ni kitu Cha kawaida tuu kupima utapima tuu siku za usoni jazba na wasiwasi utakapokua umepungua ila Ni njema pia kujua afya yako mapema.
Wasiwasi hauwezi pungua mpaka atakapopima....
 
Mkuu kwa nini unasema una ukimwi? Je vipimo fake hospitali ndo vinakufanya useme una ukimwi?
Je umedhoofu?
Ngoja nikuambie ndugu, Ukimwi upo na unasababishwa na lishe duni tu pamoja na matumizi mabaya ya mwili kama Pombe, ngono nyingi, na baadhi ya dawa za hospitali ukizitumia unapata Ukimwi.
lakini ukimwi hausababishi na kirusi cha HIV kama tulivyoamanishwa. Huyo mkeo hana anaweza kuwa na Ukimwi lakini asiwe na HIV.
Tena nakuonya usijaribu kuanza kutumia ARV ndo utaanza kuugua kweli ukimwi, anza lishe bora na ufuate kanuni za afya ili uepuke mtego wa ARV.
Hizo dawa ni mtego wa kibiashara ya madawa ya Viwanda vya madawa. Chunga sana na ujifunze zaidi kuhusu hiyo kitu.
Jaribu ku google na ujifunze zaidi kuhusu "Aids is a hoax".

 
Usipime mkuu kwa sasa,sababu ikiwa umeathirika kwel unaweza kuchukua maamuz magumu hata ya kujiondoa uhai,au hata kuathirika kias kikubwa kisaikolojia kias cha kushusha kinga yako ya mwil kwa kias kikubwa,maana hata msongo wa mawazo hushusha kinga ya mwili(stress),muhim ni kutuliza Kwanza akil na kufanya inshu zako kama kawaida,na kingine Ukimwi siyo ugonjwa wa hatar kama wengi wanavyouchukulia ukizingatia kuna dawa za kuongeza umri wa kuishi,kuna wangapi? wamekufa vifo tofauti na Ukimwi ilhali walikuwa na Ukimwi,eg ajali,pia ni wangapi? hawana Ukimwi lakin wamefariki wakawacha walio na Ukimwi,ukizingatia kwa sasa kuna tetesi ya kuvumbuliwa kwa Dawa ya Ukimwi inayotibu na kukinga kwa asilimia 98,ila haijaanza kusambazwa rasmi,mpaka mwaka mmoja upite,kwa sasa inaendelea kufanyiwa taathimin kabla ya kuruhusiwa kusambazwa,hivyo mkuu usiwe mwepes kukata tamaa,jipe moyo,hakuna atakaeshi milele hapa dunian,sote tu wapita njia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasiwasi hauwezi pungua mpaka atakapopima....
Sawa ila angalau Hali ya kupaniki itapungua akipima kwa Sasa akapata majibu asiyoyataka anaweza akafanya maamuzi ya ajabu zaidi Ni Bora atulie Kama hivi humu atapata faraja pia akishirikisha ndugu na jamaa zake anaowaamini zaidi itamsaidia.
 
UKIMWI SIO KIFO nenda kapime kama itagundulika una maambukizi basi zingatia ushauri wa daktari kwa kufuata masharti utaishi maisha marefu na yenye furaha. Wangapi wanatangulia mbele ya haki (Wanakufa) bila kuumwa UKIMWI? Unaweza ukaumwa na ukaishi miaka mingi pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kawaida tu hiyo mkuu usijali sikuhizi ni ugonjwa wa kawaida tu maana dawa wanameza Mara mbili kwa mwaka na nimepata habar kuna dawa za Mara moja kwa mwaka by 2020 kutakuwa na dawa safi kabisa na ukimwi utakuwa SI kitu.

ukimwi sio mwisho wa maisha
 
Sawa ila angalau Hali ya kupaniki itapungua akipima kwa Sasa akapata majibu asiyoyataka anaweza akafanya maamuzi ya ajabu zaidi Ni Bora atulie Kama hivi humu atapata faraja pia akishirikisha ndugu na jamaa zake anaowaamini zaidi itamsaidia.
Akikutana na wataalam watajua jinsi ya kumhandle na huenda akawa hana maambukizi tofauti na anavyo jihukumu. Ni kwenda tu kwa wataalam...the earlier the better.
 
Kama ni miaka3 nakuhakikishia una 100% hauna huo ugonjwa! Sababu ntakuambia baada ya kupima..
 
Pole braza,hili ni zito siwezi kutoa kauli yoyote zaidi nitakaa hapa kupata idea kutoka kwa wale watakaokuja ili siku nikikutana na situation kama hii nijue jinsi ya kui-handle.Mungu awe nawe ktk kipindi hiki kigumu.

sent from Kibiti with Nokia3310 using Jf app
 
Duuh! mkuu,huyo mpenzi wako sidhani kama alizaliwa nao halafu hakujua,mi nina uhakika kama kweli alizaliwa nao itakiaje afike umri wa kiutu uzima kabisa asiwe anatumia hata ARVs,huyo mtu ana kinga ya namna gani hadi asinyong'onyezwe..,na vilevile wakati anaenda kliniki inamaana hakuwahi kupima?

Aache ukatili ameshakuua tayari,na mbaya zaidi umenikumbusha kifo cha binamu yangu aliyekua kaathirika,amezikwa juzi tu,HIV is real.

Sent using Jamii Forums mobile app
"Aache ukatil ameshakuua",hii kauli siyo sahihi kabisa kwa Mtu mwenye wakati mgum anayehitaj kufarijiwa,tambua kama umepima na hauna siyo mwisho wa kupata Ukimwi,na unaweza ukamdharau mgonjwa w Ukimwi na kumdhihaki,we ukatangulia kufa yeye akabaki,suala la kufa ni mipango ya Mungu,na siku zote tambua hakuna aliye salama katika ulimwengu huu,kufa kupo pale pale,uwe na Ukimwi usiwe na Ukimwi lazima utaondoka tu.
Siku hizi huu ugonjwa siusikiagi tena, sijui ushainekana wa kawaida?

Sent From Ikulu-Magogoni street


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom