Nimekutana na mtu mwenye miguu ya kwato za ng'ombe kama hii

Kirikou Wa Kwanza

JF-Expert Member
May 24, 2013
3,564
1,991
Jamaa katoka klabu usiku njiani kakutana na mwanamke mrembo.

Jamaa: Mambo mrembo? Mrembo: Poa. Jamaa: Unaelekea wapi? Mrembo: Naelekea nyumbani. Jamaa: Ingia ndani ya gari nikusogeze kidogo.

Mrembo akaingia ndani ya gari wakaanza safari. Wakati safari ikiendelea yule mwanamke mrembo akacheka sana, Jamaa akauliza, "Unacheka nini?" Yule mwanamke mrembo akamjibu, "Angalia miguu yangu." Jamaa kuangalia miguu akaona ni miguu ya kwato za ng'ombe, Jamaa akasimamisha gari akaanza kukimbia, akakimbia sana akafika mahali akasimama huku akihema kwa nguvu. Kwa mbali akaona mwanamke mmoja anakuja mahali alipo yeye akamwita, "Dada samahani naomba msaada wako, nimekutana na mtu mwenye miguu ya kwato za ng'ombe." Yule mwanamke akamjibu huku akimuonesha, "Kama hii."

Tehe tehe tehe kilichoendelea nasikia Jamaa hakugeuka nyuma alikimbia kutoka Makumbusho mpaka Bagamoyo kwa miguu!
 
Lakini hizi ni story za pwani tena miaka ile ya 70
 
Back
Top Bottom