Nimekamatika!!!

Nimekamatika!!!

Kuna waliofunga ndoa bomani kwakuwa dini tofauti. Baba wa mke akasema mwanae haweziw kuzini lazima waozwe kwa ubani. Sheikh aliitwa jamaa akabadili dini wakati ana.
Mama wa mume alivyosikia aliwaita akaweka mkwara lazima ndoa ya kanisani. Walibatizwa na kuozwa kanisani.
Ahahaaaaaaa.....sasa kimsingi wamefunga ndoa hao au wamefungishwa ndoa na wazazi wao...anyway heri mie dini tofauti na hakuna ndoa ya serikali wala dini na maisha yanasonga mbele na watoto wanabatizwa wakikuwa ruksa kusilimu au hata kuwa walokole...dini zilikuja hiI usishangae zikaja zingine na watu wakaenda kuzifuata.
 
Nakumbuka dada yangu alichumbiwa na jamaa mwaka 96 pia jamaa alikuwa muislam, kilichotokea jamaa alikubali kufunga ndoa ya kikristo lakin baada ya mda matokeo yake dada yangu ndo kabadili dini na kuwa muislam na maisha yakasonga wana watoto ambao wote wamefata dini ya kiislam lakin mmoja kaamua kuwa mkristo na bado maisha yanaendelea vizuri hakuna ubaguz wala nini
 
Dini ni swala mhimu sana, hakuna urafiki kati ya nuru name giza, kaskazini haiwezi kushikamana na kusini kamwe, mwombe Mungu atakupa wa type yako!
 
Habari za jpili wakuu?

Kuna binti nimempata nina kama miezi mi3 niko naye kwenye mahusiano, alishawahi kuolewa ila mumewe alifariki, kiukweli binti ni mzuri wa sura na tabia pia na kiukweli nampenda kupita kiasi.

Tatizo linakuja kwamba yeye ni muislamu nami ni mkristo, nimejitahidi kumshawishi atoke huko ila amegoma maana mzee wake ni Sheikh, mm nahitaji kumuoa huyu binti, sasa nimefikiria kubadili dini kwa sekunde kadhaa ili nimweke tu ndani japo sina dhamira ya dhati kuwepo huko.

Naombeni ushauri kwa wenye uzoefu na ndoa za namna hii.
Pole na wewe unalo jaribu kumpa muda akigoma achana naye tu km hataki badilisha dini kwa hiari yake.
 
Habari za jpili wakuu?

Kuna binti nimempata nina kama miezi mi3 niko naye kwenye mahusiano, alishawahi kuolewa ila mumewe alifariki, kiukweli binti ni mzuri wa sura na tabia pia na kiukweli nampenda kupita kiasi.

Tatizo linakuja kwamba yeye ni muislamu nami ni mkristo, nimejitahidi kumshawishi atoke huko ila amegoma maana mzee wake ni Sheikh, mm nahitaji kumuoa huyu binti, sasa nimefikiria kubadili dini kwa sekunde kadhaa ili nimweke tu ndani japo sina dhamira ya dhati kuwepo huko.

Naombeni ushauri kwa wenye uzoefu na ndoa za namna hii.
Pendaneni tu ila ishu za kubadili dini ndio itakuwa fimbo ya kuwatenganisha.... Na hata mmoja akibadili dini na mkaoana always kuna mikanganyiko itawatokea... Sishauri yoyote kati yenu abadili dini.. Na kama mna masikio basi sikieni
 
Hi mkuu

Kwa mtazamo wangu nakupa hinti mbili

Ya kwanza.
Muislam kubadili dini ni ngumu aidha ukibadili wewe kurudi ukristo ni ngumu sana, ukibadili wewe ukubali kuwa mwanamke na yeye awe mwanaume kwa nn. Iko hivi mwanaume ukishindwa kumconvinsi mwanamke mkiwa wachumba jua mkiwa mke na mume huwezi pia kumkomvinsi hivyo akiweka msimamo lzm uufyate tu na ukigoma hakuna ndoa doa linaingia

Pili
Mtoto wa kike akiwa na msimamo wa wazazi unatakiwa kumwelewesha haswa kuwa yeye anapaswa aamue hatma yake sasa na sio kuamuliwa , umwambie hataishi na wazazi wake milele , mzazi wake akiamua yeye ndo maisha waliyonayo kwa sasa . yeye anapaswa aamue yeye maana akiolewa pia hatakuwa na mamlaka ya kufuata wazazi wanasemaje Bali mustakabali wa familia yao umo mikononi mwao yaani yeye na mumewe. Ukiwa mwanaume nyimbo zote hizo asielewe piga chini maana utajuta

Hamjaanza kupitia karaha za kuwa wawili mtakapoanza hiii
 
Pendaneni tu ila ishu za kubadili dini ndio itakuwa fimbo ya kuwatenganisha.... Na hata mmoja akibadili dini na mkaoana always kuna mikanganyiko itawatokea... Sishauri yoyote kati yenu abadili dini.. Na kama mna masikio basi sikieni
Yes kaka
Watu wanashindwaje kupendana kwa kuwa wanasali.kwenye majengo tofauti!!
 
Achana NAE huyo.....
Hao kwao wewe mwanaume unapo badili dini kwao ni SHEREHE KUU.

Na ukija kutoka wakati umesha muabisha binti, ujue MAJINI, VIPANDE, NAPEPO N.K
na mikosi ya kila aina itakuandamaaa kaka,,,,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom