Hataki niishi naye kwanza mpaka nijitambulishe kwao

SuperHb

JF-Expert Member
Mar 21, 2016
897
697
Habari zenu wanajf..kuna mambo yananitatiza kidogo.

Kuna Binti niko nae kwenye Mahusiano takribani mwezi mmoja na nusu hivi..kiukweli nampenda sana,,,sina hata mpango wa kumsaliti. Huyu binti anaishi mbali kidogo na wazazi wake ana group la Mabinti wengine anaoishi nao....wanapanga kwa kushare chumba,

MWAZO WA SINTOFAHAMU:
katikati ya Mahusiano yetu,binti alisimamishwa kazi mpaka muda huu ninaoongea, anadai mimi ndo chanzo maana kuna muda alikuwa anatumia Simu ya Boss wake kuchati namimi, kwahiyo anadai Boss aliona Chatting zetu akaamua kumfukuza kisa ni kwamba,eti ameendekeza mapenzi kuliko kazi.

Mimi baada ya kuona hali hiyo nikaamua kumwambia kwamba niko tiyari nimuoe kwa maana ya kuishi nae kama mke, afu baada ya Siku kadhaa niende kwao kwa Wazazi wake nitoe taarifa ya kwamba binti nataka nimtolee mahali ya kumuoa.

Binti ninapomwambia anasema hawezi kuishi na mimi mpaka niende kwa Wazazi kwanza

WASIWASI WANGU
(Hofu yangu, kwa sasa binti hana kazi yoyote, anapoishi kodi, maji, umeme, chakula anahitajika alipie, pia Wanaishi Group la Mabinti watatu wenzio wana kazi zao. Je, wataweza kumtunza mpaka lini? Si itafika hatua watamchoka?)

Kwa upande wangu sina uwezo wa kumlipia akiwa anaishi peke yake huko mimi nilitaka Aje aishi na mimi mahitaji yote atayapata akiwa kwangu kama mke, afu baadae mimi niende kujitambulisha kwao ila yeye Binti hataki hilo wazo langu anataka tuendelee kuwa kama wapenzi, ila swala kuishi namimi hataki mpaka nijitambulishe kwao.

Sasa ndugu zangu kweli mnaona kuna dalili nzuri za mahusiano yetu?

NB: Binti alishawahi nidokeza kwamba Wenzio anaoishi nao wanaenda makrabu usiku yeye wanamuacha ndani, na anasema yeye wala hajihusishi nao japo wanaishi wote.

Nisamehe kwa mpangilio mbaya wa ujumbe ASANTENI
 
Habari zenu wanajf..kuna mambo yananitatiza kidogo...

Kuna Binti niko nae kwenye Mahusiano takribani mwezi mmoja na nusu hivi..kiukweli nampenda sana,,,sina hata mpango wa kumsaliti. Huyu binti anaishi mbali kidogo na wazazi wake...Ana group la Mabinti wengine anaoishi nao....wanapanga kwa kushare chumba,

MWAZO WA SINTOFAHAMU:
katikati ya Mahusiano yetu,binti alisimamishwa kazi mpaka muda huu ninaoongea,,,anadai mimi ndo chanzo,,,maana kuna muda alikuwa anatumia Simu ya Boss wake kuchati namimi...kwahiyo anadai Boss aliona Chatting zetu akaamua kumfukuza kisa ni kwamba,eti ameendekeza mapenzi kuliko kazi...

Mimi baada ya kuona hali hiyo nikaamua kumwambia kwamba niko tiyari nimuoe...kwa maana ya kuishi nae kama mke...afu baada ya Siku kadhaa niende kwao kwa Wazazi wake nitoe taarifa ya kwamba binti nataka nimtolee mahali ya kumuoa,,,

Binti ninapomwambia anasema hawezi kuishi na mimi mpaka niende kwa Wazazi kwanza,,,

WASIWASI WANGU
((Hofu yangu,Kwasasa binti hana kazi yoyote,Anapoishi Kodi,Maji,Umeme,Chakula anahitajika alipie,,,pia Wanaishi Group la Mabinti watatu,,wenzio wana kazi zao...je wataweza kumtunza mpaka lini? Si itafika hatua watamchoka?))

Kwa upande wangu sina uwezo wa kumlipia akiwa anaishi peke yake huko....mimi nilitaka Aje aishi na mimi mahitaji yote atayapata akiwa kwangu kama mke...afu baadae mimi niende kujitambulisha kwao....Ila yeye Binti hataki hilo wazo langu anataka tuendelee kuwa kama wapenzi,,,ila swala kuishi namimi hataki mpaka nijitambulishe kwao...

Sasa ndugu zangu kweli mnaona kuna dalili nzuri za mahusiano yetu??

NB:Binti alishawahi nidokeza kwamba Wenzio anaoishi nao wanaenda makrabu usiku yeye wanamuacha ndani....na anasema yeye wala hajihusishi nao japo wanaishi wote.

Nisamehe kwa mpangilio mbaya wa ujumbe ASANTENI
Ana akili sana. Kama kweli kajitambulishe naunga mkono hoja
 
Ana akili sana. Kama kweli kajitambulishe naunga mkono hoja
Sikatai..wasiwasi wangu anaoishi nao...wanatabia mbovu za kulala nje kwenye ma nightcrub,,wanywaji wa pombe...wanaweza muambukiza tabia mbovu...ndo maana nataka niishie nae kwanza
 
Inawezekana wewe ni dizaini ya wale masela mnaovaa jeanz za kuchanika chanika magotini, vipensi vya kubana au unanyoa upara pembeni halafu juu unaacha tunywele twingi twingi halafu unatunyongolota rasta na umeachia uchebe wa kutosha kama Rick Ross

In short huyo binti ana akili na ameshtuka unataka ukae nae kigeto geto baadae ukimchoka upite hivi, mwisho aishie kupata majuto na usingo maza juu..

Kama una nia ya kweli nenda kajitambulishe ndio uishi nae. No short cut. Man up bro!!!
 
Sasa hapo tatizo nn? Si muende kwao ukajitambulishe, au unataka muishi tyuu kivileee, afu baadae umteme?

Na ninachoona anakupa majaribu na anakupima je kweli unampenda wee.

Akili kichwan kwako.
 
Sikatai..wasiwasi wangu anaoishi nao...wanatabia mbovu za kulala nje kwenye ma nightcrub,,wanywaji wa pombe...wanaweza muambukiza tabia mbovu...ndo maana nataka niishie nae kwanza
Wahi ukajitambulishe
 
Acha kuishi na mtoto wa mtu kiholela co nzuri kabsa hii bas tu ndo ivo tunapendaga shortcut
 
Habari zenu wanajf..kuna mambo yananitatiza kidogo...

Kuna Binti niko nae kwenye Mahusiano takribani mwezi mmoja na nusu hivi..kiukweli nampenda sana,,,sina hata mpango wa kumsaliti. Huyu binti anaishi mbali kidogo na wazazi wake...Ana group la Mabinti wengine anaoishi nao....wanapanga kwa kushare chumba,

MWAZO WA SINTOFAHAMU:
katikati ya Mahusiano yetu,binti alisimamishwa kazi mpaka muda huu ninaoongea,,,anadai mimi ndo chanzo,,,maana kuna muda alikuwa anatumia Simu ya Boss wake kuchati namimi...kwahiyo anadai Boss aliona Chatting zetu akaamua kumfukuza kisa ni kwamba,eti ameendekeza mapenzi kuliko kazi...

Mimi baada ya kuona hali hiyo nikaamua kumwambia kwamba niko tiyari nimuoe...kwa maana ya kuishi nae kama mke...afu baada ya Siku kadhaa niende kwao kwa Wazazi wake nitoe taarifa ya kwamba binti nataka nimtolee mahali ya kumuoa,,,

Binti ninapomwambia anasema hawezi kuishi na mimi mpaka niende kwa Wazazi kwanza,,,

WASIWASI WANGU
((Hofu yangu,Kwasasa binti hana kazi yoyote,Anapoishi Kodi,Maji,Umeme,Chakula anahitajika alipie,,,pia Wanaishi Group la Mabinti watatu,,wenzio wana kazi zao...je wataweza kumtunza mpaka lini? Si itafika hatua watamchoka?))

Kwa upande wangu sina uwezo wa kumlipia akiwa anaishi peke yake huko....mimi nilitaka Aje aishi na mimi mahitaji yote atayapata akiwa kwangu kama mke...afu baadae mimi niende kujitambulisha kwao....Ila yeye Binti hataki hilo wazo langu anataka tuendelee kuwa kama wapenzi,,,ila swala kuishi namimi hataki mpaka nijitambulishe kwao...

Sasa ndugu zangu kweli mnaona kuna dalili nzuri za mahusiano yetu??

NB:Binti alishawahi nidokeza kwamba Wenzio anaoishi nao wanaenda makrabu usiku yeye wanamuacha ndani....na anasema yeye wala hajihusishi nao japo wanaishi wote.

Nisamehe kwa mpangilio mbaya wa ujumbe ASANTENI
Kwanini vijana wenzangu mnakuwa vipofu, mnakuwa viziwi mnakuwa kama mazombie, mnakuwaje? Kila muda unavyoenda ndio kasi ya wanaume mazezeta ndio inaongezeka.

Kwanini utumie nguvu kubwa kulazimisha kuishi na kahaba, huyo kazoea kudanga akiwa na marafiki zake hapo huna demu bali una kahaba.
Kuwa mwanaume acha upumbavu.
 
Huezi funika konyagi na mfuniko wa Jack Daniel af ukasema hiyo ni pombe ya bei ghali.
Wote wawili ni hopeless. Kuna red flags mob, simu ya bosi kuchat na wewe, kukaa na viruka njia, kukataa kukaa na wewe but at the same time umgharamie e.t.c. wat i know lazma akwepe kukaa na wewe because akifanya hivo utajua kabisa yeye ni mtu wa aina gani na uhuru utapungua, lakini ukienda kwao ukamuoa tayari umefungwa pingu mbaya.
KwAko pia unakosa msimamo, kama unataka kumuoa nenda kwao umuoe fullstop af upambane na hali yako. Ukiishi na mwanamke kama una roho ndogo huoi
 
Kwani binti kwao ni Kyiv kiasi uogope kwenda kujitambulisha?

Ikitokea binti akakufia huku unaishi naye bila kumtolea mahari huwa ni patashika kama ni mkurya.

Wanakutoza mahari na faini msibani ndiyo wanazika.
 
Mwezi mmoja na nusu kwenye mahusiano ni muda mfupi sana, huyo Binti yuko sahihi kabisa kama kweli una mpenda na una malengo naye nenda kwa wazazi wake ukajitambulishe, kila lakheri kwenu.
 
Back
Top Bottom