Nimekamatika!!!

Nimekamatika!!!

Kuna waliofunga ndoa bomani kwakuwa dini tofauti. Baba wa mke akasema mwanae haweziw kuzini lazima waozwe kwa ubani. Sheikh aliitwa jamaa akabadili dini wakati ana.
Mama wa mume alivyosikia aliwaita akaweka mkwara lazima ndoa ya kanisani. Walibatizwa na kuozwa kanisani.
Hekaya za Abunuasi hizi.
 
Tia mimba uone kama huyo babake sheikh ajakufata na kukuuliza "sasa kijana tunafanyaje kuhusu hili"!!
 
Mdogo wangu najua kwa sisi vijana tunaotafuta binti wa kuoa huwa inakuwa ngumu kumpata kwa sababu tu unania ya dhati ya kuwa na familia na hautaki kumchezea.
Ninachokushauri maswala ya imani ya kidini nimagumu sana ingawa kila kitu kinaweza badirika saa yoyote. Neno ninalokupa ni kwamba chagua moja 1. Muoane kwa makubariano kila mmoja aabu dini lake.
2. Jaribu kumuomba mungu akupe wa dini lako
 
Huko kwenye dini yako wanawake wamekwisha?! Baniani mbaya kiatu chake kizuri!! teh! teh!
 
Pole sana! Kuna wengine hapa wanakushauri uachane nae yani kirahisi rahisi tu, lakini hawajui mapenzi yako na huyo mrembo yalianzia wapi. Lakini sasa kama shida ni yeye hataki kubadili dini. Je, wewe unashindwa nini kuibadili ya kwako ukamfuata kwenye imani yake kama kweli unampenda? Usilazimishe ushindi usioweza kuupata au kutamani mafanikio ambayo huwezi hata kuyafikia. Dini kwenye mahusiano ni kitu kikubwa siyo kitu cha mzaha mzaha wakati mwingine mtu unaweza kufanya nae kila kitu, lakini imani zenu zikawatenganisha. Siyo jambo la rahisi kumtoa mtu kwenye imani yake ambayo amekuwa nayo akiiamini tangu utotoni. Mtoto wa watu ameshasema hawezi kubadili dini, basi wewe huna budi kumfuata kama huwezi bora muachane kuliko kuendelea kuitenda dhambi ya zinaa.
 
Halafu wewe umeshakuwa mtu mzima, eti unataka kubadili kwa sekunde...kubadili dini kwa sekunde ndio nini? Kitu unachotaka kukifanya mzee utakuja kujuta maisha yako yote!
 
Habari za jpili wakuu?

Kuna binti nimempata nina kama miezi mi3 niko naye kwenye mahusiano, alishawahi kuolewa ila mumewe alifariki, kiukweli binti ni mzuri wa sura na tabia pia na kiukweli nampenda kupita kiasi.

Tatizo linakuja kwamba yeye ni muislamu nami ni mkristo, nimejitahidi kumshawishi atoke huko ila amegoma maana mzee wake ni Sheikh, mm nahitaji kumuoa huyu binti, sasa nimefikiria kubadili dini kwa sekunde kadhaa ili nimweke tu ndani japo sina dhamira ya dhati kuwepo huko.

Naombeni ushauri kwa wenye uzoefu na ndoa za namna hii.
naomba namba zake. usimpotee muda bure.
 
Dini ni swala mhimu sana, hakuna urafiki kati ya nuru name giza, kaskazini haiwezi kushikamana na kusini kamwe, mwombe Mungu atakupa wa type yako!
Hamna kitu kama hicho, sisi wote tumeumbwa na Mungu mmoja, hayo ya kaskazini na kusini kufungamana Mimi huwa naona ni utashi tu wa wanaadam, vinginevyo kila dini ingeishi eneo lake, lakini tunachangamana kwa sababu ya Baba mmoja,

Wakati mwingine tunafanya vitu kinafiki, mfano hawa wawili tayari wameshafanya mapenzi, hilo halionekani kama ni tatizo, ila ndoa ndo tatizo.

Hili ni tatizo
 
Habari za jpili wakuu?

Kuna binti nimempata nina kama miezi mi3 niko naye kwenye mahusiano, alishawahi kuolewa ila mumewe alifariki, kiukweli binti ni mzuri wa sura na tabia pia na kiukweli nampenda kupita kiasi.

Tatizo linakuja kwamba yeye ni muislamu nami ni mkristo, nimejitahidi kumshawishi atoke huko ila amegoma maana mzee wake ni Sheikh, mm nahitaji kumuoa huyu binti, sasa nimefikiria kubadili dini kwa sekunde kadhaa ili nimweke tu ndani japo sina dhamira ya dhati kuwepo huko.

Naombeni ushauri kwa wenye uzoefu na ndoa za namna hii.
Kama hataki kubadili dini achana naye wanawake ni wengi mkuu.
 
hua sielewi wanaume mnaosema mtie mimba huyo... maana papuchi ni ya mwanamke, mimba itaingia pale tu atapokua tayari...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom