Nimekamata Ujumbe Katika Simu ya Mke Wangu Akimtumia Mama Yake Majina ya Wanawake Anaohisi Kuwa ni Michepuko Yangu, Nimeshangaa na Kufadhaika.

WhoWeBe

JF-Expert Member
Dec 18, 2022
2,301
4,243
Msaada wenu tafadhali.

Amechambua jumbe zangu katika simu yangu, kila jumbe ya kike iliyokuwa tata kidogo kwake amelitafuta jina la namba hiyo na sasa amemtumia mama yake majina yote. Hili nimeligundua leo baada ya kuinasa katika siku yake.....bila shaka alijisahau kuifuta.

Majina haya wanataka wakayafanyie nini?!!! Ni wachawi hawa?!!!!!!! Mpaka sasa nimekausha tu kimya nasubiri kwanza nipate hili na lile katika ushauri.

Kwa kawaida huwa sifuti meseji kila wakati na nina marafiki wengi tu wa kike ambao tunaongea ya maana, tunaongea yasiyo na maana, tunataniana n.k katika kupitisha siku. Hili nimewahi kumuelekeza na simu yangu ni yake tu.

Nimefadhaika na kushangaa sana!!
 
Alafu wakiitwa wanaume na wewe utatoka? Mwanamke anashikaje simu yako?
Nnachojua Mwanaume kushika simu ya Mke ndio umama ila Mke kushika simu yangu iyo kawaida na atakayokutana nayo humo ndio atajua mwenyewe ameze dawa gani, simu yangu hata mwanangu wa miaka mitano anajua password na Mama yao pia ila akishoboka kuchunguza yasiomhusu atajua mwenyewe ila mimi simu yake sijawahi kuigusa hata akiacha wapi sina huo muda mimi natimiza majukumu yangu tu
 
Msaada wenu tafadhali.

Amechambua jumbe zangu katika simu yangu, kila jumbe ya kike iliyokuwa tata kidogo kwake amelitafuta jina la namba hiyo na sasa amemtumia mama yake majina yote. Hili nimeligundua leo baada ya kuinasa katika siku yake.....bila shaka alijisahau kuifuta.

Majina haya wanataka wakayafanyie nini?!!! Ni wachawi hawa?!!!!!!! Mpaka sasa nimekausha tu kimya nasubiri kwanza nipate hili na lile katika ushauri.

Kwa kawaida huwa sifuti meseji kila wakati na nina marafiki wengi tu wa kike ambao tunaongea ya maana, tunaongea yasiyo na maana, tunataniana n.k katika kupitisha siku. Hili nimewahi kumuelekeza na simu yangu ni yake tu.

Nimefadhaika na kushangaa sana!!
Kwanza tuambie .

Unachepuka au huchepuki??
 
kama mkeo ni mtu wa mikoa ya pwani kuanzia tanga shuka hadi mtwara bas kua na wasiwasi ANATAKA KUWALOGA hao wanawake otherwise endelea kupiga bia tuu hamna kitu, ila narudia kama mkeo ni mtu wa pwani mkuu stay at ease
 
Nnachojua Mwanaume kushika simu ya Mke ndio umama ila Mke kushika simu yangu iyo kawaida na atakayokutana nayo humo ndio atajua mwenyewe ameze dawa gani, simu yangu hata mwanangu wa miaka mitano anajua password na Mama yao pia ila akishoboka kuchunguza yasiomhusu atajua mwenyewe ila mimi simu yake sijawahi kuigusa hata akiacha wapi sina huo muda mimi natimiza majukumu yangu tu
Sanamu lako lijengwe round about ipii??

Wewee ndo MWANAUME.
 
Back
Top Bottom