Nimejenga ujenzi rahisi kwa Milioni 7 tu

Nimejenga ujenzi rahisi kwa Milioni 7 tu

Wakuu, poleni na janga hili la corona. I hope mnachukua tahadhari zote ili kubaki salama. Basi leo nimeona vema nishee namna nilovokamilisha ujenzi wa kijibanda changu. Najua kuna mtu ntakua nmemsaidia na kumtia moyo kwamba kwa kidogo alichonacho, inawezekana kuepukana na adha za ma faza house.

Nyumba nimejenga ni ndogo ila inanitosha. Ni vyumba viwili vya kulala, sebule, choo na korido fulani ambapo ndo kuna jiko kupikia. Kiwanja nilinunua 25 kwa 25 nilinunua mwaka juzi 2018 kwa sh milion4.5 locationi ni madale mwisho. So nkaona kujenga nyumba kubwa itanichukua muda mrefu kulinganisha na kipato changu, so nkajenga nyumba hii ndogo pemben kabisa ya uwanza, na kuacha nafasi kubwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kubwa hapo baadae. Nyumba hii imeanza kuchimbwa msingi tar 22 feb 2020 na baada ya siku 29 me nkahamia.

Baada ya kuezeka milangoni na madirisha nmewekaMa drill. Na nyavu za kukinga mbu. Bado cjaweka plasta. Na chini ni rough floor. Sijaweka ceiling board , namaanisha dari. Hii nmeweka chooni tuu. Milango ya mbao ni miwili wa chooni na wa sebuleni. Umeme pia bado ila nmeshalipia nawasubiri jamaa wakuje kuwasha.

So nyumba hii cjacomplicate saana. Nmejenga simple tuu. Maana kuna bandiko niliona humu jf jamaa alisema ujenzi ni ww na maamuzi yako unatakaje. Unaweza jenga kwa m10 ramani ile ile ambayo mwingne kajenga kwa m20.

Gharama za ujenzi.
Vifaa vya ujenzi vyote vilinunuliwa siku moja. Tar 22 feb 2020. Lengo la kununua kwa siku moja ni kupunguza gharama za usafiri kununua kimoja kimoja. Nilinunua na nikaweka hapa kwa jirani yangu.

Vifaa vyote vilinunuliwa maduka ya madale mwisho. Actually kabla sijanunua nilienda maduka ya town tegeta kule, nkaulizia bei baada ya kupiga tathmin nkagundua cjakwepa kitu. Nei ni zile zile tuu. So nkaona bora ninunue madale ntasave kidogo kweenye usafiri. So gharama ni kama ifuatavyo.

Bati geji 32 @ 18,500 = 740,000
Cement 37 @13,500 = 499,500
Mbao papi 18 @ 10,000 = 180,000
Mbao kenchi 40 @ 5,800 = 232,000
Mbao zege 15 @ 7,500= 112,500
Misumari nchi 4 kg 10 @ 3,000 = 30,000
Misumari bati kg 9 @ 6,000 = 54,000
Misumari nchi 3 kg 2 @ 3,000 = 6,000
Koa 2 @ 3,500= 7,000
Nondo 10 @ 18,000 = 180,000
Sink la choo 1 @ 18,000
Bomba 2 nchi 4 @ 13,000 = 26,000
Bomba nusu nchi 1.5 @ 7,500 = 3,500
Pitrap 1 @ 2,500
Elbow 2 @ 3,500 = 7,000
Usafiri 40,000
Kuchimba shimo la choo 230,000
Mchanga tipa 4 @55,000 = 220,000
Kokoto tipa 1 @ 150,000
Tofali 1650 @ 1025 = 1,691,250
Grill madirisha 4 @ 150,000= 600,000
Grill mlango 1 @ 200,000
Grill dirisha choo 1 @ 30,000
Mlango wa sebule 150,000
Nyavu za mbu na zile zingne nilisahau kurekodi. Lets say 100,000

Fundi 1,300,000 ( alifanya kila kitu)
Saidia fundi 29 days @10,000 = 290,000
Chakula mchana 29 days @ 3,000= 87,000
Jumla niliyopata kwa gharama zote hizo juu ni
7,200,000

Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera sana mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiv mkuu gauge kubwa ndio bati zinapungua ubora au?mana kuna gauge 28 pia!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio, kwa mfano gauge 26 ni bora kuliko gauge 28. Hapo gauge 26 ni ngumu na imara sababu ina unene ( thickness) mkubwa.
Gauge 26 inauzwa bei kubwa kuliko ile ya 28.
Jinsi namba ya geji inavyokuwa kubwa ndiyo bati linakuwa jembamba sana na rahisi kulikunja, na hata kutoboa haliwi gumu.
Geji 32 hazidumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tupia picha we mzee.
Niliwahi kujenga mnara wa tenki za maji nikaweka chini stoo na choo na juu nikaweka chumba cha 3.5 by 3.5 na choo kidogo ndani kwa milioni 15 tu na juu nikaweka tenki la lia 10,000. Ukipaangalia utasema kighorofa cha nguvu. Kila kitu kinawezekana ndugu zangu tena uzuri wa ujenzi unanunua vitu kidogo kidogo sio sawa na gari mpk uwe na hela yote ndio unanunua
 
KIUFUPI HILI NI BANDA (samahani lakini ndo ukweli, umejenga banda la kulala)
Kwa Pesa hiyo ni sahihi kabisa ujenzi Wa banda kama hili;
Kwanza hata milioni 6 ingetosha!
we demu mkali hebu weka li mjengo lako hapa tulione?

"Not everything is for everybody"
 
Hongera
Wakuu, poleni na janga hili la corona. I hope mnachukua tahadhari zote ili kubaki salama. Basi leo nimeona vema nishee namna nilovokamilisha ujenzi wa kijibanda changu. Najua kuna mtu ntakua nmemsaidia na kumtia moyo kwamba kwa kidogo alichonacho, inawezekana kuepukana na adha za ma faza house.

Nyumba nimejenga ni ndogo ila inanitosha. Ni vyumba viwili vya kulala, sebule, choo na korido fulani ambapo ndo kuna jiko kupikia. Kiwanja nilinunua 25 kwa 25 nilinunua mwaka juzi 2018 kwa sh milion4.5 locationi ni madale mwisho. So nkaona kujenga nyumba kubwa itanichukua muda mrefu kulinganisha na kipato changu, so nkajenga nyumba hii ndogo pemben kabisa ya uwanza, na kuacha nafasi kubwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kubwa hapo baadae. Nyumba hii imeanza kuchimbwa msingi tar 22 feb 2020 na baada ya siku 29 me nkahamia.

Baada ya kuezeka milangoni na madirisha nmewekaMa drill. Na nyavu za kukinga mbu. Bado cjaweka plasta. Na chini ni rough floor. Sijaweka ceiling board , namaanisha dari. Hii nmeweka chooni tuu. Milango ya mbao ni miwili wa chooni na wa sebuleni. Umeme pia bado ila nmeshalipia nawasubiri jamaa wakuje kuwasha.

So nyumba hii cjacomplicate saana. Nmejenga simple tuu. Maana kuna bandiko niliona humu jf jamaa alisema ujenzi ni ww na maamuzi yako unatakaje. Unaweza jenga kwa m10 ramani ile ile ambayo mwingne kajenga kwa m20.

Gharama za ujenzi.
Vifaa vya ujenzi vyote vilinunuliwa siku moja. Tar 22 feb 2020. Lengo la kununua kwa siku moja ni kupunguza gharama za usafiri kununua kimoja kimoja. Nilinunua na nikaweka hapa kwa jirani yangu.

Vifaa vyote vilinunuliwa maduka ya madale mwisho. Actually kabla sijanunua nilienda maduka ya town tegeta kule, nkaulizia bei baada ya kupiga tathmin nkagundua cjakwepa kitu. Nei ni zile zile tuu. So nkaona bora ninunue madale ntasave kidogo kweenye usafiri. So gharama ni kama ifuatavyo.

Bati geji 32 @ 18,500 = 740,000
Cement 37 @13,500 = 499,500
Mbao papi 18 @ 10,000 = 180,000
Mbao kenchi 40 @ 5,800 = 232,000
Mbao zege 15 @ 7,500= 112,500
Misumari nchi 4 kg 10 @ 3,000 = 30,000
Misumari bati kg 9 @ 6,000 = 54,000
Misumari nchi 3 kg 2 @ 3,000 = 6,000
Koa 2 @ 3,500= 7,000
Nondo 10 @ 18,000 = 180,000
Sink la choo 1 @ 18,000
Bomba 2 nchi 4 @ 13,000 = 26,000
Bomba nusu nchi 1.5 @ 7,500 = 3,500
Pitrap 1 @ 2,500
Elbow 2 @ 3,500 = 7,000
Usafiri 40,000
Kuchimba shimo la choo 230,000
Mchanga tipa 4 @55,000 = 220,000
Kokoto tipa 1 @ 150,000
Tofali 1650 @ 1025 = 1,691,250
Grill madirisha 4 @ 150,000= 600,000
Grill mlango 1 @ 200,000
Grill dirisha choo 1 @ 30,000
Mlango wa sebule 150,000
Nyavu za mbu na zile zingne nilisahau kurekodi. Lets say 100,000

Fundi 1,300,000 ( alifanya kila kitu)
Saidia fundi 29 days @10,000 = 290,000
Chakula mchana 29 days @ 3,000= 87,000
Jumla niliyopata kwa gharama zote hizo juu ni
7,200,000

Sent using Jamii Forums mobile app
o
 
Kumbe pale kwenye plot yangu ya 50 kwa 30 tashusha mjengo mkubwa sana.!
Eti bosi ulitumia tofali ngapi kwenye msingi+boma(pagale).

5/5
 
Pole sana Mkuu. Allah hajakukatia tamaa, shukuru kwa jinsi ulivyojiuguza,anza ukurasa mpya ukimtumaini Allah kwake hakuna linaloshindika,Inshaallah atakufanyia wepesi.

Sent using Jamii Forums mobile app
asante sana kwa kunitia moyo, kitanzi kingine nilipoanza kuzitafuta ni CORONA, NIMEISHIWA POZI KWAKWELI
 
Back
Top Bottom