Nimefurahi kukutana na Gentamycine

Mtumaini Mungu

JF-Expert Member
Aug 3, 2021
879
1,061
Tumshukuru Mungu kwa pumzi hii na riziki anazotupatia.

Mnamo tarehe 28 September niliweka Uzi hapa JF nikimuulizia na kumtafuta mwanachama maarufu Bw. GENTAMYCINE ambaye happy awali sikuwahi kumfahamu kwa lolote lakini namna alivyoongelewa na wanajukwaa ikanibidi nitie muhuri katika ulimwengu wa roho na kuanza Kumtafuta, Namshukuru Sana Mungu kwani ni Mwema kila wakati Amenijibu na hatimaye jana nimeona comment ya huyu ndugu popoma.

Kaka popoma nimefurahishwa Sana na ujio wako wa mara ya pili hapa jukwaani, ni imani yangu utakuwa mstari wa mbele kutema madini "Heavy" ili "kuwafunda" vijana, Mimi pia niko mstari wa mbele kujifunza toka kwako.

Ubarikiwe sana ndugu yetu popoma, Nakukubali.

 
Ni Matumaini yangu makubwa kuwa umeshajiandaa Kisaikolojia kuambiwa kuwa hii ID yako ni Mimi Mwenyewe na hapa nimejianzishia Uzi kwa kutaka Sifa na 'Fame' zaidi JamiiForums.

Ukitaka Uzi wako Uchangiwe kwa Kasi na haraka Siku nyingine anzisha Uzi wa Kunisema na Kunichafua ila kwa huu wa Kunipongeza nakuhakikishia kuwa utaenda Kudoda ( Kukudodea ) tu.

Asante kwa Kuiona Tunu yangu Mkuu. Na huwezi Kubarikiwa na Mwenyezi Mungu kuwa 'Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer' kama GENTAMYCINE halafu usichukiwe na usiwe Midomoni mwa Watu.

Shukran Mungu kwa Kuniumba tu hivi.
 
Ni Matumaini yangu makubwa kuwa umeshajiandaa Kisaikolojia kuambiwa kuwa hii ID yako ni Mimi Mwenyewe na hapa nimejianzishia Uzi kwa kutaka Sifa na 'Fame' zaidi JamiiForums....
' Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer '
 
Inaonekana huyu kijana hana shughuli ya kufanya..... yupo mjini kwa shemu.
Hujakosea sina Kazi ya Kufanya kwani hata hili Bando la kuwa hapa JamiiForums huwa unaniwekea Wewe.

Ni kweli Sina Kazi ya Kufanya kwani hata Kula yangu ya Kutwa nzima Wewe ndiyo huwa unanipa Pesa ya Kula.

Ni kweli kabisa sina Kazi ya Kufanya ndiyo maana Watu wote wenye Kazi zenu ( Wewe ukiwemo ) Kutwa hamuachi Kufungua Threads zangu na Kupoteza muda wenu Kuzisoma na hadi kupata muda wa Kunijibu wakati mnatakiwa kuwa busy na Kazi.

Na wala si tu kwamba sina Kazi nakuongezea lingine kuwa GENTAMYCINE ndiyo JF Member Masikini wa Kipato na ana Maisha Magumu kuliko nyote mliopo hapa.

Ni kweli kuwa sina Kazi kwani huyo huyo Mwenyezi Mungu aliyekupa Wewe hiyo Kazi ndiyo ameninyima ila amenibariki na Akili nyingi ambazo pamoja na kukupa Wewe Kazi hiyo ila aliuacha Upumbavu mkubwa ulionao ili uzidi Kujidhihirisha Kwetu hivi.

Ukifungua Kampuni yako naomba Ajira.
 
Back
Top Bottom