Nimefiwa na mama yangu mzazi

Mchaka Mchaka

JF-Expert Member
Jul 20, 2010
4,516
1,404
ndugu zangu jumapili iliyopita tarehe 15.5.2011 ilikuwa siku mbaya kwangu kuliko zote. Mama yangu kipenzi alitangulia mbele ya haki. Tulimzika juzi jumanne. Ila kila nikijaribu kufanya chochote nashindwa nishaurini wenzangu. Nahisi nitamfuata huko.
 
pumzika kwa amani mamake mchaka mchaka na bwana akuangazie mwanaga wa milele.....
 
pole sana kwa msiba uliokupata. Jipe moyo, ongeza sala na ni muda wa kuwa karibu na familia. Ukisikitika kupita kiasi utakufuru
 
Pole sana, tunajua upo katika wakati mgumu sana wa janga la mawazo. Usijali hayo ndo maisha jipe moyo, na usipende kukaa peke yako, kazi ya Mola haina makosa, alimleta sasa amemchukua, sote tutaenda huko.
 
ndugu zangu jumapili iliyopita tarehe 15.5.2011 ilikuwa siku mbaya kwangu kuliko zote. Mama yangu kipenzi alitangulia mbele ya haki. Tulimzika juzi jumanne. Ila kila nikijaribu kufanya chochote nashindwa nishaurini wenzangu. Nahisi nitamfuata huko.

Pole sana Mchaka Mchaka. ni hali ngumu uliyonayo lakini muombe sana Mungu na jitahidi kusoma mandiko yatakupa faraja
 
Pole sana ndugu yetu, na Muumba ampokee katika ufalme wake. Kumbuka kuwa sote tumo kwenye foleni - kwa hiyo hali halisi ni kukabalofu.
 
pole sana kaka. ni njia ya kila mtu ukisema unataka kumfuata unamkosea Mungu ambae ndie mpangaji.cha kujiuliza ni kuwa je utaishi miaka alioshi yeye? iga mazuri yake na nasaha zake alizokuachia na malezi aliokupa nawe uyatumie kuwalelea wanao utakaojaliwa au uliojaliwa.Tunaambiwa mbinguni kuna raha hakuna tabu wala mateso,ishi kadiri ya mafundisho ya dini yako na imani kwa Mungu wako ili baadae uje kurithi uzima wa milele.
 
Asante.
 
Pole sana kwa kufiwa na Mama, usiwaze sana ukampa shetani nafasi ya kukutumikisha. unatakiwa ujue unapaswa sasa kuendelea na shughuli zingine.
 
Pole sana mkuu..Pole sana.

Kumbuka wewe sio wa kwanza kukumbwa na kisa hiki.. Wapo waliopata machungu hata zaidi yako. Jipe moyo kwamba, unahitaji kufarijika kwa sasa na kufikiria mbele..

Kipindi hiki usipende kukaa peke yako..tafuta watu ukae nao, na mpige stori..Jishughulishe kiasi, ili akili ianze kuzoea.
 
Pole Mchaka mchaka, lfe must continue, Jifunge sawasawa na usonge mbele.
 
pole sana kwa kufiwa ndugu yetu.
ni wajibu wetu kufa. Wakati unaendelea kuomboleza, pia kumbuka maisha ya mama, mshukuru mungu kwa kukutanisha nae. MAma ni kiumbe wa mbungu kwanza, na wewe sasa ukawe mzazi mzuri
 
usihuzunike sana najua angekuwepo angetaka we uwe na furaha. mkumbuke kwa mema yake.POLE SANA.
 
Back
Top Bottom