Nahisi Nimetupiwa kombola la kichawi usiku wa kuamkia leo, nahisi ganzi kwenye nyao za miguu, viganja vya mikono na mdomoni

Mohamedex121

JF-Expert Member
Jan 27, 2022
1,688
3,142
Wakuu salam zenu, nimepatwa na tatizo aisee nashindwa kuelewa je ni uchawi au maradhi ya kawaida.....

Kuna siku nilileta uzi humu jukwaani suala la kuota ndoto ya ajabu kuomuona mtu mweusi na anamacho mekundu ndotoni aise hili jambo lilinitisha sana nikaongeza ibada kwenye maombi ile hali haikunitokea tena....

Sasa jana usiku wakati nimelala nikaota kuna mtu ( kimuonekano ni mmama mnene kiasi ila kavalia vazi jeusi kama kanikin kanisimamia mbele ya kitanda changu upande nilipolala ni kama tunaangalia uso kwa uso mimi nikiwa kitandani nimeegemea mto wakati huyu mtu akiwa kanisimamia mbele yangu.

Wakati naendelea kushanga shanga gafla nikamuona anaanza kurudi nyuma huku akipiga hatua kidogo kidogo yaani kama mtu anavyonyata huku alielekea kwenye kona moja ya ukuta wa chumba...

Alivyofika kwenye ile kona akainama chini then akapotea gafla nikaanza kuhisi mwili mzima unaganzi, kuinuka kitandani nashindwa, kuongea sauti aitoki, nikijaribu kujigeuza napo nashindwa...

Nikabaki kujisemea kimoyoni moyoni " AUDHU'BILLAH. Gafla nikaanza kusikia sauti ya miyonzi masikioni, kadri sauti inavyopungua na ndivyo ile ganzi mwili inapotea. Ufahamu ukarudi huku macho yakiwa yapo wazi ( I means tukio nzima wakati linatokea macho yalikuwa wazi ) sasa sijui ndio ndoto au mauza uza?

Niliogopa sana nikaamua kuwasha taa mpaka kuna kucha taa ya chumbani kwangu ilikuwa inawaka. Nikachukua simu nikaanza kugoogle maana ya tafsiri mbalimbali za ndoto ya namna hii..sikutaka kulala kabisa kwa hofu niliyokuwa nayo. Ilivyofika saa 11 alfajiri nikalala nakuja kuamka saa 5 nahisi baadhi ya viungo vya mwili wangu nahisi ganzi.

Kuanzia kwenye nyayo za miguu. Nikitembea sisikii chochote yaani hakuna hisia zozote zile natembea kama sitembei hii hata nikivaa malapa au viatu nahisi kama sijavaa chochote. Pia kwenye viganja nako pia nahisi ganzi sametimes kushika kikombe cha chai nashindwa kabisa kwa hofu ya kumwaga chai yaani nahisi kama sijashika chochote kitu.

Pia mdomoni napo pia nahisi ganzi kuanzia kwenye ulimi na meno yote yanaganzi....

Je, kwa hali hii wapi naweza kupata msaada wa kitabibu kabla hali haijawa mbaya zaidi.

NATANGULIZA SHUKURANI.
 
Je tiba za kisuni kwenye maduka ya karibu na msikiti mtoro zinaweza kusaidia??
Wakuu!
 
Upo kwenye hatua kufanikiwa ndio maana wanakushambulia
Kurogwa kwangu kunauhusiana vipi na mafanikio yangu mkuu??? Maana kama kusoma nimesoma japo sina ajira rasmi zaidi ya umachinga, nimeshapoteza biashara yangu ya studio naishi kusogeza siku...
 
omba duq ya kupinga kukataa na kufuta hilo tukio. Ila ili ufanikiwe uombe kwa Jina la Yesu na kutambia mamlaka zake.

Njia nyingine nje ya hapo utakuwa unahairisha tatizo ila hulitatui.

Ni hilo tu
Mi ni muislamu bado sijawa na imani na mambo ya kikristo. Ila shukurani nitalifanyia kazi kwa kuhudhuria makanisani maana kwenye matatizo kama haya nisiweke udini
 
Mkuu nunua mafuta ya zaitun Chua maeneo hayo ya ganzi fanya hivyo kama itaendelea usisite kunambia
Shukrani sana mkuu. Mafuta ya mzaituni nilikuwa nishayaweka kwenye list kwenda kuyanunua apo kesho.
Mengine ni mafuta ya abatsoda, pia nataka nimtafute shekhe aje anipe kisomo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom