Nimefiwa na BABA Yangu Mzazi

Inna Lillah wa inna lilaah lajuun! X-P Mungu awe nawe na familia yako kwa ujumla hasa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kumpoteza mpendwa wetu! na Mungu akawatie nguvu na uvumilivu! Amen
 
X paster, poleni sana wewe na familia yako, mungu awajaze kheri ya kukabiliana na msiba mkubwa uliowafika, ni vigumu kukabaliana na hali hii lakini kwa rehema za mwenyezi mungu tunaamini mtaweza.

Apumzike kwa amani. Amina
 
Pole sana mkuu dunia hii ni mapito na kila nafsi lazima itaonja mauti binadamu ni mavumbi na mavumbini tutarudi mungu ailaze roho ya marehemu baba yetu mahala pema peponi. Amen
 
"Hakika kila nafsi itaonza mauti",pole sana ndugu mwenyezi MUNGU akupe faraja na roho ya kustaimili katika kipindi hiki kigumu wako
 
Pole ndugu,wote ndio tuendako tu njiani,Mungu ampe Pumziko la Milele Amen
 
Pole sana Mpwa, Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe milele na milele. Amen
 
X-PASTER,
pole sana mkuu Mwenyezi Mungu aiweke roho yake Peponi,
tuombe kheri sisi tuliobaki maana sote tu watu wa njia moja,
Yeye Muumba huamua atakalo, nasi yabidi kumshukuru
ingawa ni ngumu kwa jinsia ya mioyo yetu ya kibinadamu
R.I.P MZEE WETU
 
Pole mwana jamii kwa msiba wa mzee wetu.. Hakika yeye ametangulia cc tunafuata
Rabbi amuweke katika fungu la waja wema na amsamehe na adhabu
Ameen
 
Bwana alitoa, naye ametwaa, jina lake libarikiwe. Pole sana mkuu
 
Mkuu X-PASTER,

Pole sana kwa msiba huo mzito sana maishani mwako. Mwenyezi Mungu awapeni nguvu na hekima nyingi katika kipindi hiki kigumu sana. Nipo pamoja nawe katika msiba huu kwa maombi na sala.

Kwa Mungu kila goti litapigwa na kila nafsi itauonja umauti.......! Mwenyezi Mungu ailazi roho ya mzee wetu mahali pema peponi ...Amen!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom