Nakereka na watu hawa!!!!

ladyfurahia

JF-Expert Member
May 10, 2011
14,699
9,460
Habari mabestito

Nimeshindwa kuvumilia imenibidi niseme waziwazi hapa kwani wengine bila ya kuwasema hawatajirekebisha, nimekereka na vitabia vya marafiki wa siku hizi hapa mjengoni kiasi kwamba nimeshindwa kuwaacha tu waendelee na mambo yao ya kipuuzi.

Hivi wewe huwezi kuanzisha uzi wako, mpaka ufakamie uzi wa mwenzako na kumsema mwenzako eti yeye ndivyo alivyo unatafuta umaarufu kupitia mgongo wa mwenzio? hii imenikera sana kwani nimeona kule mmu mtu mzima na akili zake timamu anaanzisha uzi kwa kuchafua mtu kwa kuweka id ya mwenzake ili tu kumchafulia id yake kwanini lakini rafiki mnakuwa hivyo

Tabia hii wanayo hawa watu walioingia siku hizi hawafuati kanuni za hapa mjengoni wala hawajazisoma kwa umakini wao, wanafakamia utadhani wamelishwa shubiri ndani ya midomo yao,

Kwaniini unapenda kuweka kibanzi wakati boriti inakutazama wewe mwenyewe, Marafiki sijafurashwa na hii jambo ndo maana nimeona niwaambie ukweli kwani si busara akumuanika id mwenzako hapa wakati sisi sote ni marafiki na ni ndugu wa jf sio ustaarabu kwani hata katika vitabu vya MUNGU vinakataza kusengenya na kumsema mwenzio vibaya

hebu someni hapa:


siku ya hukumu kila mtu atatoa hesabu ndomaana Yesu akawaambia viache ngano na magugu vikue pamoja wakati wa mavuno mwenye shamba atachagua ngano na magugu kuyachoma motoni.

Hata ikiwa mtu anayo sifa ile lakini madamu unamsema nyuma yake na ni jambo ambalo mwenyewe asingelipenda kulisikia basi pia huingia katika hukumu hii ya ghiybah:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ : (( أَتَدْرُونَ مَا الْغِيبَةُ ؟ )) قَالُوا : اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ ، قَالَ
: ((ذِكْرُكَ أَخَاكَ بِمَا يَكْرَهُ )) ، قِيلَ : أَفَرَأَيْتَ إِنْ كَانَ فِي أَخِي مَا أَقُولُ ؟ قَالَ : (( إِنْ كَانَ فِيهِ مَا تَقُولُ فَقَدِ اغْتَبْتَهُ ، وَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِيهِ فَقَدْ بَهَتَّهُ))
[ أخرجه مسلم ]

Tuachane na tabia hizi kwani hazimpendezi Mungu marafiki, usimseme mwenzio vibaya, mmpende ndo maana tukaanzisha teamrafiki kwani ni team inayojali, inayopenda, na kusaidiana pia kwanini mchoreshe mwenzio kiasi hichi.

Wasalaam

Ladyf

cc: Mamndenyi, Mtambuzi, KakaKiiza, Mentor, Paloma, Jiwe Linaloishi, Nicas Mtei, charminglady, Passion Lady, @Vislay, mwallu, jouneGwalu, steven Robert Masaku, Erickb52, watu8, measkron, Kongosho, King'asti, Paw, Young Master, @C6, The secretary, mtoto Halali na pesa, Heaven on Earth, monaco, Asprin, na marafiki wengine karibuni tujadili hili namna gani tuwasaidie wale wanaowachafua watu mjengoni hapa.

 
Becoming a great thinker is not easy! Sometimes unaweza kuambulia matusi kwa kuwa tu mtu hajaipenda post yako au uko tofauti na kile anachokiamini
 
sasa ladyfurahia tufanyeje ili hao wanaoingia siku hizi wasifanye wanavofanya? tuwakataze kuja JamiiForums? sasa JamiiForums ni kwa ajili ya nani? tukiendelea kuwabeza hivo si wataona jukwaa limekuwa shubiri?

tuwaelilishe jamani sio wakongwe kuwabeza wageni kihivoo..

imagine jf ingekuwa ya wale waliojiunga 2006 tu,, tungeweza kupata elimu tunayopata hapa?

SERIOUSLY kuna viumbe vinakera lakini tujitahidi sana kujizuia kutoa hoja kwa kupitia mgongo wa HAWA WAGENI.. sio fresh..
 
Last edited by a moderator:
wako wanawake visebengo humu jf as mwenye uzi!!! Tatizo lenu mnajifanya ndio wenye jf kumbe ni suala fikra na mitazamo yenu ya kizamani mna hulka ya za kinazi, mna hofu gani kama watu wanatoa maoni yao!!! wako free kumuani mtu yeyote , nyie mmekuwa vigogo wa kutoa maoni kikandamiza wengine!!! ladyfurahia kajipange upya , badili mtazamo na fikra zako za kizamani huwezi fanya ujinga watu wakufumba macho!!! " watu huwasha taa nakuweka juu ya kinara si chini ya kitanda" ref injili ya luka. nasiwasilisha
 
Last edited by a moderator:
Wageni wana fujo....tumewaharibia jeiefu yao. Hujaelewa tu?

JF ni ya wote usipokubali mabadiliko hutagain chochote kila kitu kinabadilika iwe kwa uzuri au kwa ubaya JF is not excluded! Hata hao wakongwe umri wa mwaka jana si wa leo dunia ya mwaka uliopita si ya leo mabadiliko ni kila mahali na hayakwepeki taka usitake
 
wako wanawake visebengo humu jf as mwenye uzi!!! Tatizo lenu mnajifanya ndio wenye jf kumbe ni suala fikra na mitazamo yenu ya kizamani mna hulka ya za kinazi, mna hofu gani kama watu wanatoa maoni yao!!! wako free kumuani mtu yeyote , nyie mmekuwa vigogo wa kutoa maoni kikandamiza wengine!!! ladyfurahia kajipange upya , badili mtazamo na fikra zako za kizamani huwezi fanya ujinga watu wakufumba macho!!! " watu huwasha taa nakuweka juu ya kinara si chini ya kitanda" ref injili ya luka. nasiwasilisha

uko sawa kabisa mkuu
 
Last edited by a moderator:
Waache u.puuzi wao na fikra za "jf yetu zamani...." Hiyo zamani mlikuwa mnajadili nini ambacho ni tofauti na haya tunayojadili leo? Hii dhana huwa naipinga sana, kuna misemo kama " hivi vitoto vya facebook vinaharibu jukwaa",

most of the time nyie mnaojiita "vikongwe" ndio mnaharibu nyuzi kwa kuanzisha story zenu tofauti na mada.
 
mshana jr hayo maneno ya kwangu au ya mtoa mada?

Hapana Khantwe nimeongezea nyama kwenye post yako Kuna watu hawataki JF ikue ibadilike wao wanazeeka lakini hawataki kukubali mabadiliko
Mabadiliko yanaweza kuwa mazuri au mabaya lakini vyovyote viwavyo hatuwezi kuyakwepa
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom