Nimefikia maamuzi, najitoa rasmi CCM

Nimefikia maamuzi, najitoa rasmi CCM

Bora kuchelewa lakini ufike, hongera kwa maamuzi hayo na Mungu amekusamehe dhambi zako za kuwaleta hayo yote yaliyokukimbiza huko ccm, umefanya maisha ya wananchi kuwa magumu sana, dhambi zako zimeonolewa kwa kuijua kweli na kuikiri nawe umekuwa kiumbe kipya. Free max.
 
Chadema wao wanashangilia tu.

Maana ndio kazi inayowapeleka huko ulaya kuichafua nchi kwa gharama yoyote.
Sijui kuichafua nchi ni lazima uende ulaya?! Je anaetumbua watu kwa kusema ukweli kwa kupitia taaluma zao ili kuwakomboa watanzania yeye haichfui nchi?! Uchafu haupandi ndege ila unaonekana bila hata darubini.
 
Ni ccm anaye jitambua sio zuzu kama ww.
hakuna uzuzu unaozidi wakwenu wa kumkumbatia fisadi.
2946ec747c4b616a8be60f0da9e3de16.jpg
 
I am sorry, siwezi kuendelea kuwa sehemu ya tabaka kandamizi! si katika mafunzo ya dini yangu


Biblia
Mithali 31

Tazama unavyokandamizwa na hiyo "dini" yako bila kujijuwa:

4 Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?

5 Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.

6 Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
 
Watu wengi sana wamejitambua sana kupitia JF. Huyu jama Maxence anaweza kuja kuwa shujaa wa kitaifa
 

Nmekumbuka mnamo mwezi wa sita mwaka huu niliumwa malaria kali sana, siku nikaamka nkasema jamani nmehamia C.cm dah ikabidi daktari aitwe haraka sana kuja kabla hata ajafanya uchunguzi akauliza mgonjwa kasemaje? Wakajibu anataka kuhamia C.cm! Dktari
afu huyu mgonjwa itakuwa malaria imepanda kichwani. Kweli kupimwa ikabainika ni kweli. Sasa sijui daktari alijuaje mpaka leo najiuliza bila jibu
 
Natumai mpaka shujaa [HASHTAG]#Melo[/HASHTAG] akitoka atakuwa amefanya mabadiliko makubwa sana kwenye fikra za watu bila ya yeye mwenyewe kujua amebadilisha watu fikra na nyoyo zao kwa kiasi gani.

Dhahabu inapoingizwa kwenye moto na kugongwa gongwa ndio huongezwa uthamani wake, hata uipake vipi maavi hautaweza kuishusha uthamani wake.

Viva JF. Viva Maxence.
 
hii inafanana na kauli hii"if u dont like to be behind my troops,u are welcome infront of.."..
 
Nina sababu kadhaa kwanini naamua kujitoa CCM na kutoendelea kuisapoti serikali yake hii ya awamu ya tano.Nina sababu kadhaa;

i. Ubabe na vitisho vya viongozi kuanzia ofisi kuu hadi watendaji wa chini, wote wamekuwa wababe na wanataka waabudiwe na kudujudiwa

ii. Ukandamizaji wa demokrasia na uhuru wa kutoa maono ( ref kesi ya Melo, Lema na Ben saanane).

iii. Kuvurugwa kwa elimu kunakoendelea mf. kuwanyima mikopo ya elimu ya juu watoto wa kimaskini

iv. Kusitisha ajira kwa maelfu ya vijana wa kimaskini tofauti na kipindi cha JK! na

v. Elements za udini na ukanda-ukabila Sitaki kuisikia tena CCM, nilikuwa mpiganaji mkubwa. wa ccm! ila yanayoendelea kwa sasa sina hamu tena.

Mkuu, wakiyatatua mambo uliyoorodhesha hapo, utarudi??
 
Back
Top Bottom