Haki haipo CHADEMA wala CCM, jamii bado ipo gizani

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,863
HAKI HAIPO CHADEMA WALA CCM, JAMII IPO GIZANI.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Haki hutofautiana baina ya nchi na Nchi. Ingawaje zipo haki za ujumla za kila mwanadamu Kama vile Haki ya kuishi na kupata nyezo zinazomfanya mtu aishi.

Haki hutofautiana baina ya nchi na Nchi kutokana na utashi, utamaduni, elimu, mazingira, Aina ya jamii husika, miongoni mwa mambo mengine.

Pengine ili nieleweke zaidi, napaswa Kueleza Kwa kifupi maana ya HAKI;

Neno Haki kwa tafsiri ya kamusi ya Kiswahili sanifu lina maana ya ‘jambo ambalo mtu anastahiki au kitu anachostahili kuwa nacho.

Kwa tafsiri ya kamusi ya kisheria neno Haki lina maana ‘ kile mtu anachostahili kuwa nacho au kile anachoruhusiwa kufanya, au kile anachostahili kupokea kutoka kwa wengine kwa mujibu wa sheria’.

Kwa maana hizo zote mbili, tunaona kuwa Haki imejikita zaidi katika Utashi wa watu, mtazamo, elimu na utamaduni wa jamii.

Haki ya Zama hizi haiwezi kuwa Haki ya zama zijazo.

Hii ni kusema, haki huathiriwa na Wakati pia.

Haki huathiriwa na Wakati kutokana na sababu kuwa Mitazamo, utashi na utamaduni wa watu hubadilika kulingana na wakati.

Msingi wa haki kidunia umejikita zaidi katika Sheria za jamii husika, sheria za nchi. Hata hivyo sheria za nchi ni matokeo ya utashi na Mitazamo ya watu katika kipindi husika.

Katika Siasa za nchi yetu, haki hutafsiriwa kulingana na mtu yupo upande gani, utashi na mtazamo wake.

Mwana CCM anatafsiri yake ya HAKI, halikadhalika na mwana CHADEMA na watu wa vyama vingine, sio ajabu kila chama kinakatiba na sheria zake. Kumaanisha vile kinavyoona na kutafsiri haki.

CCM ambayo ilikuwa TANU baada ya TAA, ilipata ngekewa ya kuwa kiranja wa kupigana Uhuru wa nchi hii ikiwa Kama haki namba moja wanayoipigania. Sio kwamba hakukuwa na vyama vingine kama sivyo nisingalisema TANU ilikuwa kiranja.

Baada ya Uhuru, CCM ya zamani (TANU) iliunda katiba (pengine kufanya amendment Kwa baadhi ya vifungu kutoka katiba iliyorithiwa Kwa wakoloni) na kutengeneza katiba na sheria kadiri ya utashi wa viongozi wa wakati ule.

Haki ndio msingi wa sheria, lakini huongozwa na utashi ambapo kwenye utashi sharti ubinafsi(maslahi) yazingatiwe.

Kuondolewa Kwa vyama vingi miaka ya 1967 ni mwendelezo wa utashi wa viongozi wa wakati huo. Mpaka kufikia 1992 kulipofufuliwa tena vyama vingi ambapo kimsingi wafufuaji na waanzilishi wa vyama pinzani walitokea chama tawala Kwa sehemu kubwa.

CCM wengi huamini kuwa kuongoza nchi ni haki yao. Wakati vyama pinzani nao huona kuwa kuongoza nchi ni haki yao.

Kila mmoja anahaki kulingana na utashi, mtazamo na uelewa wake. Hata hivyo huwezi tenga mbali haki na maslahi.

CCM hawaioni kasoro ya Katiba mpya kwa sababu inalinda Haki(Maslahi) Yao. Pia Katiba hiyo waliiratibu vile ilivyo kulinda maslahi Yao ya kushika Dola na kuendelea kuwepo Dolani.

CHADEMA lazima wahitaji katiba mpya itakayolinda Haki zao(maslahi Yao), kwani maslahi ya chama cha Siasa ni yapo; Msingi WA uwepo wa chama cha Siasa ni Kushika Dola.

Ikiwa ni hivyo, lazima chama kiangalie njia zitakazo kisaidia Kushika Dola. Njia moja wapo ni uwepo wa Katiba na sheria nzuri zinazokiwezesha Kushika Dola Kama vile UWEPO WA TUME HURU YA UCHAGUZI.

CHADEMA Kama ilivyo CCM au vyama vingine inalinda maslahi ya chama na Wanachama kabla ya maslahi ya wananchi.

Ukiingalia jamii ya Watanzania walio wengi, Kwa kweli haina mpango wowote na wala haina mpango na masuala ya Siasa, jamii ya kitanzania wengi wao hata hawana mpango na Katiba mpya kwani hata yazamani hawalijui.

Katika uchunguzi huru nilioufanya Maeneo kadhaa ya nchi hii, nilibaini kuwa Watanzania waliowengi wapo gizani kabisa.

Watanzania wengi ni Bora liende, yote Sawa, ilimradi tunaishi na Kula ugali matembele.

Haki kuu ya Watanzania Kwa uchunguzi wangu, ni kuishi Kwa usalama bila kujali wanaishi maisha ya umasikini au Utajiri.

Pia nilibaini kuwa, Watanzania wengi hawapendi kujiingiza katika mkondo wa mambo ya Siasa, pia hawapendi marafiki wanaojihusisha na mambo ya Siasa.

Endapo utajiingiza kwenye Siasa, sio ajabu rafiki na watu wanaokuzunguka wakakuambia shauri yako, unakihere here, na mambo mengine Kama hayo.

Ikiwa Watanzania wengi hawataki kuisikia wala kujiingiza kwenye Siasa ni dhahiri hawana maslahi na Siasa,

Ni ngumu kuwaingiza Watanzania kwenye Katiba mpya ati waidai, wakati hawataki kujiingiza kwenye Siasa, na uhitaji wa Katiba ndio msingi Mkuu wa Siasa.

Haki za CHADEMA ni uwepo wa Katiba mpya itakayowapa fursa nao Kushika Dola.

Haki ya CCM ni kuendelea Kwa Katiba iliyopo itakayowafanya waendelee Kushika Dola.

Haki ya wananchi sio Katiba mpya wala Katiba iliyopo. Kwani wananchi hawana Uelewa na hawataki Uelewa wa mambo ya Katiba.

Wananchi wengi huwa na mtazamo kuwa iwe CCM iwe CHADEMA au ACT, itakayoshika Dola, hawatapata maslahi ya moja Kwa moja isipokuwa lazima waendelee kusota na kuhangaika na maisha Kama ilivyosiku zote.

CCM hawaioni haja ya Katiba mpya Kwa sababu wameshapima kina cha maji ya wananchi WA taifa hili kuwa wao hawapo upande wowote ule. Katiba sio kipaumbele cha wananchi. Hata hivyo hawajui hata hiyo Katiba ni nini.

Wananchi wa Tanzania wengi wao Wana mtazamo kuwa Maendeleo kuletwa ni hisani ya Viongozi, sio ajabu wakiwasujudia na kuwaogopa.

Katiba mpya itakuwa muhimu na yalazima pale jamii itakapobadili mtazamo, utashi, elimu, maarifa.

Ukosefu wa elimu miongoni mwa Watanzania imeathiri Kwa kiasi kikubwa utambuzi wa haki zenye manufaa kwa wananchi.

Wananchi wasio na elimu huona ni haki Yao kuishi vile waishivyo bila kujali wanaumia au law. Hii ni tofauti na Wale wenye elimu.

Katiba mpya itakuwa haki ya jamii siku jamii yenyewe ikipata Uelewa wa kile kinachohitajika ndani ya Katiba mpya na jinsi kitakavyoathiri maisha yao Kwa namna chanya.

Katiba mpya haitapatikana ikiwa sio hitaji la jamii, ikiwa itakuwa hitaji la chama Fulani hasa kisichokuwepo madarakani basi bado itakuwa ni ndoto kuipata.

Nafikiri,
Elimu ya maisha itolewe,
Jamii ielezwe Kwa nini wanamaisha mabovu,
Na Kwa nini wanapaswa wabadili maisha yao yawe Bora,
CHADEMA na vyama vingine havipaswi kutumia harakati Kali katika masuala haya.

Katika jamii ambayo elimu ya uraia bado ni changamoto,

Katika jamii ambayo ushabiki wa mambo ya udaku ni mkubwa mno,

Katika jamii ambayo huamini maisha ni bahati,

Katika jamii ambayo huona Siasa ni mchezo hatari,

Katika jamii ambayo uchawi na Ushirikina ni mkubwa,

Katika jamii ambayo ujenzi wa makanisa ya kuombea miujiza yanajengwa kila uchwao badala ya kujenga mashule na hospital.

Katika jamii ambayo ukiwapigania unaitwa kihere here,

Nafikiri namna Bora ya kuibadili jamii yoyote Ile sio kuwatetea Bali kuwapa Hali ngumu ya kiuchumi, kimaisha na kila Nyanja ya maisha.

Mabadiliko hutokea kwenye Hali ngumu.

Jamii ipo GIZANi,
Wenye Nuru hawataki Nuru iwafikie wanajamii.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
 
Kiukweli ni vigumu kwa mazingira ya sasa kuielimisha jamii hii ya Tanzania masuala yahusuyo haki za kijamii. CCM wamefanya makusudi kuhakikisha jamii haielimiki ili wao waendelee kunufaika na kutawala watakavyo.
 
Nimekusoma toka mwanzo nikawa sikuelewi ila nikawa nalazimisha kuendelea kukusoma hivyo hivyo, ila nilipofika pale unaposema Chadema lazima wahitaji Katiba Mpya ili iwape maslahi yao ndio nikaona napoteza muda kukusoma wewe "TAIKUN WA FASIHI"

Umenionesha mwenyewe huelewi maana ya Katiba Mpya, upo upo tu, ila unapenda sana kuizungumzia, nikwambie kitu, sio kila kitu lazima uwe unakianzishia mada, vingine wacha wengine waanzishe then ujifunze toka kwao, mambo ya biblia na mapenzi kidogo nimeona unajitahidi.

Nimalizie tu kwa kukwambia unaposema haki haipo Chadema ni kweli, lakini ukisema haki haipo CCM unakosea, kwasababu wao ndio wanufaika namba moja na maamuzi yote yanayosababishwa na uvunjwaji wa sheria za nchi.

Ndio maana tunataka Katiba Mpya irudishe mamlaka ya nchi kwa wananchi badala ya hayo mamlaka kubaki kwa watawala kama ilivyo sasa, na unaposema wananchi wengi hawana uelewa wa hayo mambo ni kweli lakini sio sifa kuendelea kuwaacha gizani.

Wacha Katiba Mpya ije kutoa miongozo ya namna keki ya taifa inavyotakiwa kufaidiwa na kila mwananchi, na kila kiongozi awe responsible kwa kila kosa atakalofanya badala ya kulindana kama ilivyo sasa.
 
Kiukweli ni vigumu kwa mazingira ya sasa kuielimisha jamii hii ya Tanzania masuala yahusuyo haki za kijamii. CCM wamefanya makusudi kuhakikisha jamii haielimiki ili wao waendelee kunufaika na kutawala watakavyo.

Ipo hivyo Mkuu
 
Nimekusoma toka mwanzo nikawa sikuelewi ila nikawa nalazimisha kuendelea kukusoma hivyo hivyo, ila nilipofika pale unaposema Chadema lazima wahitaji Katiba Mpya ili iwape maslahi yao ndio nikaona napoteza muda kukusoma wewe "TAIKUN WA FASIHI"

Umenionesha mwenyewe huelewi maana ya Katiba Mpya, upo upo tu, ila unapenda sana kuizungumzia, nikwambie kitu, sio kila kitu lazima uwe unakianzishia mada, vingine wacha wengine waanzishe then ujifunze toka kwao, mambo ya biblia na mapenzi kidogo nimeona unajitahidi.

Mkuu,

Suala la Katiba mpya jamii haina mpango nalo, labda unibishie tuu.

Mimi nipo kitaa, najichanganya na watu wa makundi yote ya kijamii.

Katiba mpya haina umuhimu Kwa jamii isiyohitaji.

CHADEMA wanaitaka Katiba mpya Kwa maslahi yao wakitumia mgongo wa wananchi. Hiyo IPO wazi kabisa.

Huwezi MPA au kumpigania mtu asiyehitaji kupiganiwa. Labda Kama Una maslahi na kitu unachotaka kumpa au unachompigania.
 
Unaposema Katiba Mpya wananchi hawana mpango nayo ni kwasababu ya ukosefu wa elimu, na Chadema kwasababu wako mbele kuihamasisha ili kuwaamsha hao wananchi unaodhani hawaitaki ni ili wananchi wajue haki zao, wala sio kwa maslahi ya Chadema, wacha upotoshaji.

Nikuulize, umeshawahi kubambikiwa kesi huko mtaani unapoishi? Unadhani ni raia wangapi sasa hivi wako jela kwa kesi za uongo? haki za vyombo vya habari, na makundi mengine yote, na hao wanaowaonea hao wananchi mwisho wa siku huwa wanachukuliwa hatua gani kama sio kulindana tu? Matendo ya Sabaya kwa raia wa nchi hii hayawezi kuwepo kama Katiba Mpya itakuwepo.

Ndio maana Katiba Mpya inapiganiwa ije kuweka standard kwa raia wote wa hii nchi, wananchi kutokuwa na mwamko ni kwasababu ya kukata tamaa na mfumo uliopo, lakini hilo haliwezi kuwa kigezo cha kuwaacha CCM na serikali yao waendelee kuumiza wananchi, Katiba Mpya lazima ije kuwaokoa wananchi toka kwa udhalimu wa CCM.
 
Unaposema Katiba Mpya wananchi hawana mpango nayo ni kwasababu ya ukosefu wa elimu, na Chadema kwasababu wako mbele kuihamasisha ili kuwaamsha hao wananchi unaodhani hawaitaki ni ili wananchi wajue haki zao, wala sio kwa maslahi ya Chadema, wacha upotoshaji.

Nikuulize, umeshawahi kubambikiwa kesi huko mtaani unapoishi? unadhani ni raia wangapi sasa hivi wako jela kwa kesi za uongo? haki za vyombo vya habari, na makundi mengine yote, na hao wanaowaonea hao wananchi mwisho wa siku huwa wanachukuliwa hatua gani kama sio kulindana tu? matendo ya Sabaya kwa raia wa nchi hii hayawezi kuwepo kama Katiba Mpya itakuwepo.

Ndio maana Katiba Mpya inapiganiwa ije kuweka standard kwa raia wote wa hii nchi, wananchi kutokuwa na mwamko ni kwasababu ya kukata tamaa na mfumo uliopo, lakini hilo haliwezi kuwa kigezo cha kuwaacha CCM na serikali yao waendelee kuumiza wananchi, Katiba Mpya lazima ije kuwaokoa wananchi toka kwa udhalimu wa CCM.

Sasa Mimi nasema kilichopo ndani ya jamii kuwa wananchi bado hawajielewi.

Mnachopaswa kufanya ni kuwaelimisha ili wajue umuhimu wa Katiba mpya, kisha wataidai hiyo Katiba mpya wenyewe ninyi mkiwasaidia.
 
Wananchi wataidai vipi hiyo Katiba Mpya wenyewe bila kuwa na viongozi? organisation yao itakuwaje? na sijui ni nani aliekwambia Katiba Mpya itakuwa mali ya Chadema, kwa haya mawazo yako hufai kuanzisha uzi kuhusu Katiba Mpya, huna uelewa wa kutosha.
 
Back
Top Bottom