Nimechukia sana Simu za Samsung, bora TECNO tu

Nimechukia sana Simu za Samsung, bora TECNO tu

Mnaonunua simu kariakoo, makumbusho mnaambiwa mpya wengi mnapigwa.

Sio kwamba ni feki bali zinajulikana kama refurbs.

Yaani simu original zilizokua na matatizo mbalimbali zikatengenezwa kwa kubadilishwa parts zenye shida.

Refurbs hazina ubaya ila tatizo ni kwamba refurbs zote au asilimia 99 zinatoka china.

Mchina anakusanya simu zilizoharibika ana repair na parts za hovyo, kuanzia vioo, camera, battery, na component nyinginezo lengo ni kutumia gharama ndogo kadri awezavyo kisha zinakuwa packed kwenye mabox yake pamoja na chargers, earphone manual, full sealed ukiikuta kariakoo unaambiwa mpya.

Ukitaka samsung, mpya isiyo na longolongo nenda kwa samsung stores au authorised dealers wale wanazo brand new, ila tu bei zimesimamia ukucha inabidi uvumilie kwenye bei.

Chukua hii.
Mkuu inakuwaje matoleo ya A yana display mbaya sana kimuonekano? Mfano A11?
 
Hio ndio Samsung bana. Kuna rafiki yangu simu ilivunjikia Ulaya akaja itengenezea bongo. Maana kule cost ilikua zaidi ya 1M ya kibongo. Akaja weka kioo kwa laki 6 bongo.
Kioo tu laki sita. Kwani hiyo simu ina kitanda ndani? Mkome kutaka sifa eti anamiliki simu kali. Niko na infinix yangu hapa sina shida ikizingua kidogo nardi zangu dukani kuchukua mpya. Hata siwazi gharama.
 
Kioo tu laki sita. Kwani hiyo simu ina kitanda ndani? Mkome kutaka sifa eti anamiliki simu kali. Niko na infinix yangu hapa sina shida ikizingua kidogo nardi zangu dukani kuchukua mpya. Hata siwazi gharama.
Mkuu, hatuwezi kufanana. Kuna mtu akikuona na infinix anaona kama unachezea pesa kwakuwa gharama yake ni kubwa. Kadiri unavyokuwa na kipato ndivyo unajikuta gharama za maisha zinapanda. Ndio maana huwezi kumkuta Bakhresa anaenda karume kununua kiatu.
 
Mambo mengine ni ya kujitakia, mm natumia simu kubwa tu (ila sio brand ya Samsung) imepasuka kioo balaaaa! Michirizi kama mwanamke mnene aliyetoka kujifungua, lakini ngoma bado inadunda. Sometimes hadi naionea huruma infact angekuwa ni binadamu katika hali hii ningeshamzika
Nbrand gani mkuu
 
Aisee mbona ulinunua bei nzuri zana, mwaka jana mwezi 8, nafikir ndo A50 zilitoka ilikua 700K sikua na uwezo nikanunua A30 540k baba mpaka leo nadunda, simu imetulia mbaya, ila kioo kona cracks kibao sema haina tatizo lolote, sumsang series A pia ipo vizur
Nazikubali nyingi mkuu ila tatizo ni uchumi wangu tu hautoshi, saiv natumia A50 nlichukua kwa 600k coz hizo za milioni mbili simudu. Ila ukitaka simu angalau nzuri isiwe chini ya laki 5. Samsung za chini ya laki 4 zimevamiwa na mchina.
 
IMG_1788.jpg

Hv hzi samsung galax beam wap naweza pata..?
 
Samsung ni display, ikivunjika imekula kwako. Ila Samsung ndio my best phone ever, hasa note series.
Hizo note ndo best smartphone of the year fuatilia note 20 ultra linganisha na flagship zote hata new iPhone 12 pro max utaona bado note ni very premium.
 
...wabongo bana kwa kupenda status Kwenye vtu.

Sasa mtu yeye ni fb,inst na WhatsApp na jf afu anataka ajipinde anunue simu ya Bei...au aina fulani

Na wewe mama wa nyumbani kutwa unashinda jikoni au bustanini unataka ununue simu mayai....Bei hiyoooo

Wewe bodaboda kutwa wewe na pkpk unataka ununue simu mayai....Bei hvyoo

Yaani wengi tunanunua simu kwa kufuata mkumbo....ukweli hatujui kwanini tunanunua simu.
 
Yangu muda si mrefu itaniambia phone processor isn't responding yaan hapo automatically unakutana na pattern ya home screen.... In short ina vioja vjngj Mara YouTube is not responding WhatsApp ........
Yaani hata Mimi ndo hivohivo
 
Huo ni usenge sana.ndo ubaya wa Samsung
Tekno malewa yangu inantosha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom