Nimechoshwa na ubunifu wa fundi huyu..!

Nimechoshwa na ubunifu wa fundi huyu..!

Lakin mkuu ujue natamani nivae nguo za mafundi wengine ila tatizo Ni kwamba chitemo Anambinu nyingi Sana za kuwashinda mafundi wenzake, maana inasemekana anauwezo wa kushona nguo bila kuangalia
Charles, Adam, Christian na wengine wanaona mbinu za Chitemo ni chafu hawaziwezi. Halafu mafundi wa maeneo mengine wana tabia za kung'ang'ania wateja kwahiyo hata hao wa huko wanaona sawa tu.
Hawaelewi hadi akaripiwe na mteja ndiyo humuachia, kuna Kamari Madafu na mwingine kaanza juzi anaitwa Yala Jamani.
 
Nishazeeka sasa , natamani mawazo ya wanangu Na wajukuu zangu wote yabadilike Ili kwa pamoja tushauriane jinsi ya kufanya maana nguo hii nilonayo inanitia fedheha sasa
Waelekeze na liwe kama somo la kila wiki wataelewa tu, hali hii akiendelea nayo hautashona tena nguo anaboronga zaidi
 
ukiona watu wanaongea kimafumbo i bet 1000$ wanamsema faru joni.
 
Sasa kama fundi Chitemo anaonekana ameishiwa ilikuaje fundi Charles kwenda kuiba materials kwa fundi huyo huyo Chitemo aliyeishiwa? Hii inaonesha hawa mafundi wengine hawana ubunifu au vp?
 
Sasa kama fundi Chitemo anaonekana ameishiwa ilikuaje fundi Charles kwenda kuiba materials kwa fundi huyo huyo Chitemo aliyeishiwa? Hii inaonesha hawa mafundi wengine hawana ubunifu au vp?
Yawezekana ilikuwa Ni mbinu ya kiushindani tu
 
Muda mwingine unaweza kuomba fundi Chitemo atangulie mbele ya haki tu.

Mungu nisamehe kwa hili.

Wakuu habar..!

Kwa umri wangu ninastahili kuitwa mzee, maana Nina zaidi ya miongo mitano tangu kuzaliwa kwangu,
Kila ninapokaa huwa nnaikumbuka sana nguo yangu niliyowah kuivaa miongo kadhaa iliyopita (enzi za ujana) ile ilikuwa ni nguo ya kwanza kuimiliki kwa muda mrefu sana nikiwa baba wa watoto kadhaa..

Mpaka sasa nna takribani nguo kadhaa ambazo nimezvaa kwa muda mrefu japo nimewahi kupima na kutamani kuvaa nguo nyingi Sana,

Nguo yangu ya kwanza ilinipendeza sana na kunipa mwonekano wenye mvuto kwa kila aliyeniona, ndani na nje ya familia yangu, ilinipa busara na heshima kubwa sana. Niliipenda sana Kwan kabla ya kuchakaa na kuchanika kwake muda mwingine niliiva hata baada ya kupata nguo ya pili na ya tatu..

Sikuwa na jins Kwani muda ulifika nguo yangu pendwa sikuweza kuivaa tena maana ilichakaa na kuchanika kabisa..

Niliamua kumfuata Fundi wangu Mahili aliyenishonea nguo ile( miongo kadhaa iliyopita) nikampa tenda ya kunibunia nguo ya pili yenye mwonekano mpya na mvuto zaidi..
Alinibunia nguo ya pili, tatu hadi hii nilonayo sasa, ambapo nguo zote alizowahi kunishonea zilikuwa tofauti lakin zilikuwa na alama flaniflani za utambulisho ambazo kamwe hakuwahi kuacha kuziweka katika kila nguo, hii ni kwaajili ya kuitambulisha kazi ya mikono yake..

Fundi wangu anafahamika kwa jina la Michael Christopher Chitemo ni Fundi mahili Sana, mwenye uzoefu, asiyetaka kupitwa kiushindani kwa njia yoyote japo mafundi wengine Kama Charles, Adam, Christian na wengine wengi wamekuwa wakitamani walau siku moja wanishonee vazi la kunifaa na kuvutia pia.

Sasa wakuu kilicho niletakwenu ni kuwaeleza kuhusu maajabu ya nguo hii ya mwisho niliyonayo kutoka kwa Fundi chitemo..

Kiukwel mm ni mkubwa Sana kiumbo, kiasi kwamba wale mafundi wengine wamekuwa wakiumiza vichwa jins gani wanaweza kupata mtindo wa nguo itakayo nivutia ili nimuhame huyu Fundi chitemo..lakin shida ni kwamba huyu Fundi Ana vipimo vya siri ambavyo humsaidia kubuni nguo yoyote pind nnapo hitaji.

Sasa wakati nilipo mpa tenda ya kunishonea nguo hii niliyonayo, alipata changamoto kubwa kutoka kwa Fundi Charles Kwani, Charles alifanikiwa kumuibia baadhi ya materials aliyo tumia kubuni nguo hii, sasa nguo ya Charles ilionekana ni nzuri na yakuvutia sana Kwan nakumbuka niliwahi kujipima nguo ile nikasifiwa Sana kwa mwonekano niliokuwa nao,niliambiwa ilinipendeza Sana na kunifaa.

Baada ya muda Fundi chitemo aliona jinsi soko lake linavyoelekea kuporwa na Fundi Charles, alilazimika kutumia mbinu zake za siri katika kubuni hii nguo ambayo ilinivutia zaid na nikajikuta naachana na ile ya Fundi Charles.

Ni mwezi mmoja sasa umepita tangu nianze rasmi kuvaa nguo hii,ni nguo ambayo ilinivutia Sana na nilisifiwa na wanangu, wajukuu na hata vitukuu kwa mwonekano makin niliokuwa nao..

"Kwanini nguo hii?" Hili swali nimekuwa nikijiuliza Sana, sijui ni kwasabab Fundi chitemo ni mzee sasa, kias kwamba hawez kushona nguo itakayonifaa kwa muda mrefu zaidi Kama awali, maana sijamaliza hata mwaka lakin Tayari nishaanza kunyooshewa vidole na baadhi ya watoto na wajukuu wangu wakidai nguo hii inanipa mwonekano wa ajabu ambao unanipa sifa mbaya Sana ndani na nje ya nyumba yangu.

Nashindwa kuelewa ni vipimo gani alitumia Fundi chitemo katika kubuni nguo hii maana imekuwa ikibadilika kimaajabu,.nikila nikashiba nguo hii hubana Sana kias kwamba nashindwa hata kupumua vizuri,nikiwa na njaa nguo hii hupwaya kias kwamba nakosa mvuto kwa watu wanaonitazama.

Niko njia panda sijui niibadili au niifanyie marekebisho , cha ajabu n kwamba hata nikisema niifanyie marekebisho nahis bado kutakuwa na matatizo bado,maana Fundi chitemo ni mbish na hatokuwa tayar kupokea msaada wa mawazo kutoka kwa watu na mafundi wenzake..

Nashindwa kuelewa mwonekano huu wa sasa unajadiliwa kwa sababu Fundi chitemo hakuwa makini wakati wa kubuni mtindo wa nguo hii au ni tatizo la materials ya hii nguo.!
Ni mapema lakin nimechoshwa na maneno ya watu wanao nizunguka na sielewi nifanye nini maana kila mtu anasema lake kuhusu Mimi..!!

Nimekaa nazitazama picha za nguo yangu ya kwanza natamani Jana ingekuwa Leo..!
 
Ukiona huelewi fumbo jepesi hivi ujue madesa yalikuharibu. Cha msingi tangulia tu kaburini siku ya kufa ikukute huko
kwanza unajiita motoka pambaya, maana yake hukuzaliwa sehemu sahihi ya kiungo lengwa, badala yake umetokea kile kiungo pendwa na akina sir Eltoni John na wenzie akina George Michael (0713)
 
[emoji276] [emoji276] [emoji276] [emoji276] [emoji276] [emoji119] [emoji119] [emoji119] [emoji4] pale unapoelewa baada ya kurudia mara ya 9
 
Back
Top Bottom