Prove me wrong Hakuna fundi tajiri.

Prove me wrong Hakuna fundi tajiri.

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
2,226
Reaction score
7,500
Graduate mlioenda VETA mnaendeleaje?
Tarehe 7 Agosti 2025, Waziri Mkuu wa wakati huo, Kassim Majaliwa, aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha vijana wanapelekwa kwenye mafunzo ya ufundi stadi yanayoratibiwa na VETA na Ofisi ya Waziri Mkuu. Alisisitiza kuwa lengo ni kuwapa vijana ujuzi wa kuajiriwa au kujiajiri.
Mimi tokea makuzi yangu yoote sijawahi kuona fundi mwenye financial freedom, sjjawahi kuona nilipokuwa mdogo kuna jamaa alikuwa ni fundi wa gari la pale home imepita miaka 20 sasa hakuna chochote anachokimiliki naona maisha yake ni magumu tu.

The same na mjomba wangu alikua fundi mechanics mzuri miaka mingi iliyopita kamaliza ujana wake wote sasaivi yupo na 63 na hakuna chochote anachokimiliki,

Mimi sijawai kuona fundi aliefanikiwa ni wachache sana ambao waliingia kwenye mfumo wa kubadilisha ufundi kuwa biashara nb wachache sana, shida ya hapa Tanzania kwa kijana ambae anachipukia kwenye ufundi ni mjuano (nepotism) mimi nikiwa na kazi nitamtafuta mtu ninayemfahamu anifanyie kazi , unajifunza labda umeme wa magari au mechanics au umeme wa majumbani, nani atakayekupa kazi? Je uwezo wa kufungua workshop yako unao?

Mkombozi kwa vijana ni kuwekeza upande sahii, kuwaelekeza upande sahii ambao ni productive nimeona kwenye biashara watu wengi wakianzia chini kabisa, mpaka kufikia kiwango kikubwa mno, nimeona watu wakilima mpaka kumiliki tractor zao binafsi. Lakini sijaona fundi pikipiki, bajaj, tiles, mechanics, n.k akifanikiwa.
 
Kipimo chako Cha utajiri Ni Nini?

Ili nijue kwamba huyu mwambegesye pamoja kuwa na gari mashamba na frame zake kumbe bado masikini kwakua anaamkia garage kufungua gearbox
Mkuu nakuelewa sana, lakini mimi sio mchawi ila huyo jamaa anamiliki gereji yake mwenyewe na anao vijana wa kuwatumikisha kwa ujira mdogo, kazi ya million 2 anawapa 20,000/=
 
Hahaha sasa kaka, hao unaowasemea wana channels kali sana yani mpaka upate tenda ya kufanya kazi mgodini sio uwezo tu, uwezo plus network sasa mimi ninaoongelea ni hawa vijana ambao wanaenda kusoma mechanics, then hao mafundi wanofanya automation viwandani kwa viwanda vipi? After installation kuna kipi cha ziada? Viwanda ni vingapi?
 
Kuna ukweli katika hili kuwa asilimia kubwa ya mafundi huishia kuwa choka mbaya

Na hili sio kwasababu hawapati hela ila ni matumizi mabaya ya hela wanayoipata

Fundi anaweza kupiga hela safi sana ila yote anamalizia kwenye starehe akiamini kuwa uhakika wa kupata tena upo na pia kazi yake hakuna kustaafu
 
Mkuu nakuelewa sana, lakini mimi sio mchawi ila huyo jamaa anamiliki gereji yake mwenyewe na anao vijana wa kuwatumikisha kwa ujira mdogo, kazi ya million 2 anawapa 20,000/=
Sure nigga anamasela 6 wazee wakulowa oil yeye Ni niletee hiyo box 26 kanichukulie maji dukani....
MAWEED nyonga bangi tukaangalie game sokoine hapo kamaliza
 
 
Kuna ukweli katika hili kuwa asilimia kubwa ya mafundi huishia kuwa choka mbaya

Na hili sio kwasababu hawapati hela ila ni matumizi mabaya ya hela wanayoipata

Fundi anaweza kupiga hela safi sana ila yote anamalizia kwenye starehe akiamini kuwa uhakika wa kupata tena upo na pia kazi yake hakuna kustaafu
Fundi gereji miaka 60 hafanyi kazi tena au unamanisha mafundi wa nini? Ujenzi?
 
RUGE MUTAHABA (R.I.P) alisema kwamba;
"Tafuta nafasi, ukiipata onyesha uwezo wako, talanta yako, bidii yako. Utajiri na mafanikio yatakuja baada ya hapo".

Sijajua wewe upo mkoa gani, lakini hapa mjini Daslam, kuna watu walianza na gereji za spana mkononi, sasa hivi wana "brand" zao za gereji. Kunq ankoli mmoja wa Mwinyi, alitoka Polisi Ufundi Kurasini, akaanzisha gereji yake hapa mjini, ukiongelea mafundi wazuri wa Land Rover discovery kuanzia matoleo ya chini yale, mpaka hizi mpya. Watakwambia nenda gereji kwa Mwinyi.

Kuhusu utajiri: Kwa macho yangu naona anao. Importers na users wengi wa magari hayo wanamjua huyo bwana. Anashughulika na gari hizo tuu, amejibrand hivyo, kuanzia discovery matoleo yote, Range Rover matoleo yote, zipo chungu nzima gereji kwake.
 
Back
Top Bottom