Nimechoshwa na ubunifu wa fundi huyu..!

kabon14

JF-Expert Member
Jun 14, 2016
1,233
867
Wakuu habar..!

Kwa umri wangu ninastahili kuitwa mzee, maana Nina zaidi ya miongo mitano tangu kuzaliwa kwangu,
Kila ninapokaa huwa nnaikumbuka sana nguo yangu niliyowah kuivaa miongo kadhaa iliyopita (enzi za ujana) ile ilikuwa ni nguo ya kwanza kuimiliki kwa muda mrefu sana nikiwa baba wa watoto kadhaa..

Mpaka sasa nna takribani nguo kadhaa ambazo nimezvaa kwa muda mrefu japo nimewahi kupima na kutamani kuvaa nguo nyingi Sana,

Nguo yangu ya kwanza ilinipendeza sana na kunipa mwonekano wenye mvuto kwa kila aliyeniona, ndani na nje ya familia yangu, ilinipa busara na heshima kubwa sana. Niliipenda sana Kwan kabla ya kuchakaa na kuchanika kwake muda mwingine niliiva hata baada ya kupata nguo ya pili na ya tatu..

Sikuwa na jins Kwani muda ulifika nguo yangu pendwa sikuweza kuivaa tena maana ilichakaa na kuchanika kabisa..

Niliamua kumfuata Fundi wangu Mahili aliyenishonea nguo ile( miongo kadhaa iliyopita) nikampa tenda ya kunibunia nguo ya pili yenye mwonekano mpya na mvuto zaidi..
Alinibunia nguo ya pili, tatu hadi hii nilonayo sasa, ambapo nguo zote alizowahi kunishonea zilikuwa tofauti lakin zilikuwa na alama flaniflani za utambulisho ambazo kamwe hakuwahi kuacha kuziweka katika kila nguo, hii ni kwaajili ya kuitambulisha kazi ya mikono yake..

Fundi wangu anafahamika kwa jina la Michael Christopher Chitemo ni Fundi mahili Sana, mwenye uzoefu, asiyetaka kupitwa kiushindani kwa njia yoyote japo mafundi wengine Kama Charles, Adam, Christian na wengine wengi wamekuwa wakitamani walau siku moja wanishonee vazi la kunifaa na kuvutia pia.

Sasa wakuu kilicho niletakwenu ni kuwaeleza kuhusu maajabu ya nguo hii ya mwisho niliyonayo kutoka kwa Fundi chitemo..

Kiukwel mm ni mkubwa Sana kiumbo, kiasi kwamba wale mafundi wengine wamekuwa wakiumiza vichwa jins gani wanaweza kupata mtindo wa nguo itakayo nivutia ili nimuhame huyu Fundi chitemo..lakin shida ni kwamba huyu Fundi Ana vipimo vya siri ambavyo humsaidia kubuni nguo yoyote pind nnapo hitaji.

Sasa wakati nilipo mpa tenda ya kunishonea nguo hii niliyonayo, alipata changamoto kubwa kutoka kwa Fundi Charles Kwani, Charles alifanikiwa kumuibia baadhi ya materials aliyo tumia kubuni nguo hii, sasa nguo ya Charles ilionekana ni nzuri na yakuvutia sana Kwan nakumbuka niliwahi kujipima nguo ile nikasifiwa Sana kwa mwonekano niliokuwa nao,niliambiwa ilinipendeza Sana na kunifaa.

Baada ya muda Fundi chitemo aliona jinsi soko lake linavyoelekea kuporwa na Fundi Charles, alilazimika kutumia mbinu zake za siri katika kubuni hii nguo ambayo ilinivutia zaid na nikajikuta naachana na ile ya Fundi Charles.

Ni mwezi mmoja sasa umepita tangu nianze rasmi kuvaa nguo hii,ni nguo ambayo ilinivutia Sana na nilisifiwa na wanangu, wajukuu na hata vitukuu kwa mwonekano makin niliokuwa nao..

"Kwanini nguo hii?" Hili swali nimekuwa nikijiuliza Sana, sijui ni kwasabab Fundi chitemo ni mzee sasa, kias kwamba hawez kushona nguo itakayonifaa kwa muda mrefu zaidi Kama awali, maana sijamaliza hata mwaka lakin Tayari nishaanza kunyooshewa vidole na baadhi ya watoto na wajukuu wangu wakidai nguo hii inanipa mwonekano wa ajabu ambao unanipa sifa mbaya Sana ndani na nje ya nyumba yangu.

Nashindwa kuelewa ni vipimo gani alitumia Fundi chitemo katika kubuni nguo hii maana imekuwa ikibadilika kimaajabu,.nikila nikashiba nguo hii hubana Sana kias kwamba nashindwa hata kupumua vizuri,nikiwa na njaa nguo hii hupwaya kias kwamba nakosa mvuto kwa watu wanaonitazama.

Niko njia panda sijui niibadili au niifanyie marekebisho , cha ajabu n kwamba hata nikisema niifanyie marekebisho nahis bado kutakuwa na matatizo bado,maana Fundi chitemo ni mbish na hatokuwa tayar kupokea msaada wa mawazo kutoka kwa watu na mafundi wenzake..

Nashindwa kuelewa mwonekano huu wa sasa unajadiliwa kwa sababu Fundi chitemo hakuwa makini wakati wa kubuni mtindo wa nguo hii au ni tatizo la materials ya hii nguo.!
Ni mapema lakin nimechoshwa na maneno ya watu wanao nizunguka na sielewi nifanye nini maana kila mtu anasema lake kuhusu Mimi..!!

Nimekaa nazitazama picha za nguo yangu ya kwanza natamani Jana ingekuwa Leo..!
 
Kila nikirudia kurudia kuitazama filamu ya Minions ndivyo ninavyopotea, nimeshindwa kufahamu maudhui ya filamu hii kama ambavyo thread hii ilivyonishinda.
images.jpg
 
hlf Fundi chitemo mwenyewe mashati anayojishonea ni over size,Fundi Charles yeye alijitahidi kujipima vzr akavaa size yake,sasa swali je?km yeye tu anashindwa kujipima vzr ataweza kukushonea size unayotaka wewe Mzee wangu??
 
Pole sana maana unatakiwa kuivaa nguo yako kwa miaka 5 na ukirudia makosa ya kurudi kwa fundi Chitemo itafanyiwa marekebisho kidogo na utaivaa kwa miaka 10 nakushauri usirudie makosa vinginevyo utanyooshewa vidole mwisho wake wajukuu watakupiga hadi makofi.
 
Fundi Chitemooo. Hata wewe uliyeandika pia ni fundi. Lakini kwa haraka naona kiza mbele ya Chitemo,labda kama hana ubunifu tena. Na kama hilo ni kweli asubiri kuona ushindani mkubwa kwa,mafundi wenzie.
 
Back
Top Bottom