Nimechoshwa na ubunifu wa fundi huyu..!

Nimechoshwa na ubunifu wa fundi huyu..!

Wakuu habar..!

Kwa umri wangu ninastahili kuitwa mzee, maana Nina zaidi ya miongo mitano tangu kuzaliwa kwangu,
Kila ninapokaa huwa nnaikumbuka sana nguo yangu niliyowah kuivaa miongo kadhaa iliyopita (enzi za ujana) ile ilikuwa ni nguo ya kwanza kuimiliki kwa muda mrefu sana nikiwa baba wa watoto kadhaa..

Mpaka sasa nna takribani nguo kadhaa ambazo nimezvaa kwa muda mrefu japo nimewahi kupima na kutamani kuvaa nguo nyingi Sana,

Nguo yangu ya kwanza ilinipendeza sana na kunipa mwonekano wenye mvuto kwa kila aliyeniona, ndani na nje ya familia yangu, ilinipa busara na heshima kubwa sana. Niliipenda sana Kwan kabla ya kuchakaa na kuchanika kwake muda mwingine niliiva hata baada ya kupata nguo ya pili na ya tatu..

Sikuwa na jins Kwani muda ulifika nguo yangu pendwa sikuweza kuivaa tena maana ilichakaa na kuchanika kabisa..

Niliamua kumfuata Fundi wangu Mahili aliyenishonea nguo ile( miongo kadhaa iliyopita) nikampa tenda ya kunibunia nguo ya pili yenye mwonekano mpya na mvuto zaidi..
Alinibunia nguo ya pili, tatu hadi hii nilonayo sasa, ambapo nguo zote alizowahi kunishonea zilikuwa tofauti lakin zilikuwa na alama flaniflani za utambulisho ambazo kamwe hakuwahi kuacha kuziweka katika kila nguo, hii ni kwaajili ya kuitambulisha kazi ya mikono yake..

Fundi wangu anafahamika kwa jina la Michael Christopher Chitemo ni Fundi mahili Sana, mwenye uzoefu, asiyetaka kupitwa kiushindani kwa njia yoyote japo mafundi wengine Kama Charles, Adam, Christian na wengine wengi wamekuwa wakitamani walau siku moja wanishonee vazi la kunifaa na kuvutia pia.

Sasa wakuu kilicho niletakwenu ni kuwaeleza kuhusu maajabu ya nguo hii ya mwisho niliyonayo kutoka kwa Fundi chitemo..

Kiukwel mm ni mkubwa Sana kiumbo, kiasi kwamba wale mafundi wengine wamekuwa wakiumiza vichwa jins gani wanaweza kupata mtindo wa nguo itakayo nivutia ili nimuhame huyu Fundi chitemo..lakin shida ni kwamba huyu Fundi Ana vipimo vya siri ambavyo humsaidia kubuni nguo yoyote pind nnapo hitaji.

Sasa wakati nilipo mpa tenda ya kunishonea nguo hii niliyonayo, alipata changamoto kubwa kutoka kwa Fundi Charles Kwani, Charles alifanikiwa kumuibia baadhi ya materials aliyo tumia kubuni nguo hii, sasa nguo ya Charles ilionekana ni nzuri na yakuvutia sana Kwan nakumbuka niliwahi kujipima nguo ile nikasifiwa Sana kwa mwonekano niliokuwa nao,niliambiwa ilinipendeza Sana na kunifaa.

Baada ya muda Fundi chitemo aliona jinsi soko lake linavyoelekea kuporwa na Fundi Charles, alilazimika kutumia mbinu zake za siri katika kubuni hii nguo ambayo ilinivutia zaid na nikajikuta naachana na ile ya Fundi Charles.

Ni mwezi mmoja sasa umepita tangu nianze rasmi kuvaa nguo hii,ni nguo ambayo ilinivutia Sana na nilisifiwa na wanangu, wajukuu na hata vitukuu kwa mwonekano makin niliokuwa nao..

"Kwanini nguo hii?" Hili swali nimekuwa nikijiuliza Sana, sijui ni kwasabab Fundi chitemo ni mzee sasa, kias kwamba hawez kushona nguo itakayonifaa kwa muda mrefu zaidi Kama awali, maana sijamaliza hata mwaka lakin Tayari nishaanza kunyooshewa vidole na baadhi ya watoto na wajukuu wangu wakidai nguo hii inanipa mwonekano wa ajabu ambao unanipa sifa mbaya Sana ndani na nje ya nyumba yangu.

Nashindwa kuelewa ni vipimo gani alitumia Fundi chitemo katika kubuni nguo hii maana imekuwa ikibadilika kimaajabu,.nikila nikashiba nguo hii hubana Sana kias kwamba nashindwa hata kupumua vizuri,nikiwa na njaa nguo hii hupwaya kias kwamba nakosa mvuto kwa watu wanaonitazama.

Niko njia panda sijui niibadili au niifanyie marekebisho , cha ajabu n kwamba hata nikisema niifanyie marekebisho nahis bado kutakuwa na matatizo bado,maana Fundi chitemo ni mbish na hatokuwa tayar kupokea msaada wa mawazo kutoka kwa watu na mafundi wenzake..

Nashindwa kuelewa mwonekano huu wa sasa unajadiliwa kwa sababu Fundi chitemo hakuwa makini wakati wa kubuni mtindo wa nguo hii au ni tatizo la materials ya hii nguo.!
Ni mapema lakin nimechoshwa na maneno ya watu wanao nizunguka na sielewi nifanye nini maana kila mtu anasema lake kuhusu Mimi..!!

Nimekaa nazitazama picha za nguo yangu ya kwanza natamani Jana ingekuwa Leo..!

Don't you have more serious issues to engage your grey matter? Get a life man!!
 
Jf bhana raha sana.
Uhuru wa mwandishi lazima upatikane tu
Huyo fundi MCC simpendi kama nini
 
Chetemo sasa tabaan yu njiani kurejea nyumbani baada ya kushshwa na Treen
 
Fundi Michael Christopher Chitemo siyo fundi sio lolote yule ni tapeli na mwizi sana haswa wa vitambaa vya wateja,

Mara zote ukidai kitambaa kilichobaki au maelezo ya ukweli wa rangi ya kitambaa ulichompatia anakuwekea kinyongo sana.

Hata me alinishonea miongo miwili ila huu wa tatu nilikataa kupeleka nguo kwake. Ameshanitoka kama mabaki ya sanda [emoji1492][emoji1492][emoji1492][emoji1492][emoji1492]
 
Fundi Michael Christopher Chitemo siyo fundi sio lolote yule ni tapeli na mwizi sana haswa wa vitambaa vya wateja,

Mara zote ukidai kitambaa kilichobaki au maelezo ya ukweli wa rangi ya kitambaa ulichompatia anakuwekea kinyongo sana.

Hata me alinishonea miongo miwili ila huu wa tatu nilikataa kupeleka nguo kwake. Ameshanitoka kama mabaki ya sanda [emoji1492][emoji1492][emoji1492][emoji1492][emoji1492]
Kweli mkuu
 
Tatizo lipo kwako wee Mzee, uliamini Jina kutokana na mazoea. Wakati unampa kazi huyo Mzee mwenzio Chitemo akina fundi Chale waliomba japo uwajaribishe kwa nguo hiyo tu.

Lakini kwa nyodo zako ukadai eti huwezi jaribisha fundi, Chitemo umemzoea haya kiko wapi sasa unachekwa hata na watoto.

Ila Mzee wangu acha niseme ukweli mwanzoni wakati umeivaa hiyo nguo zile siku za kwanza kwanza ulipendeza mpaka nikakuonea donge kwa nn sikukuunga mkono wakati ulipomteua Chitemo kuwa fundi wako. Mpaka nikaahidi na mimi safari ijayo nampelekea Mzee Chitemo anishonee.

Ila ulipofua tu hilo koti duu!! baada ya miezi michache, ndo nimeona nilikuwa sahihi kutokukuunga mkono, mi nadhani kutokana na umri wa Mzee mwenzio Chitemo alibambikiwa kitambaa, ametumia kitambaa kingine ambacho hajakikusudia. Kitambaa hakikubali pasi, hakinyosheki, ila hamna jinsi nguo zako za zamani huwezi kuzitumia tena vaa hivyo hivyo usogeze siku.

Anyway Mzee usikate tamaa tuombe uzima kukosea njia ndo kujua njia. Ukipata pesa zako za kiinua mgongo usikurupuke tena tafuta fundi mzuri ikiwezekana na kitambaa ununue mwenyewe.
 
Kubadilisha fundi kazi sana maana amekuwa akikushonea miaka yote kwa hiyo mwili wako vipimo vyako amevizoea. Unaweza kuacha fundi wa zamani ukasema niende kwa fundi mwingine akatoa kituko usiweze hata kuvaa... I feel you mzee tatizo ni uoga unaogopa kuthubutu, unajiuliza vipi huyu Charles kama ataharibu kabisa kuliko huyo Chitemo. Ila usiogope kwani Charles akikuharibia ukaamua kurudi kwa Chitemo atakukataa? Jilipue tu[emoji23]
 
Hahaha mimi sitaongelea kuhusu fundi Chitemo.

Ila nimependa ubunifu wako...big up mkuu!
 
Back
Top Bottom