Nimechoshwa na ubunifu wa fundi huyu..!

Nimechoshwa na ubunifu wa fundi huyu..!

Fundi Chitemo angekubali japo hata ushauri jamani pengine angefanya marekebisho kidogo na nguo ikakufaa.
Hii ingerudisha heshima yako mkuu....!
 
Fundi Chitemooo. Hata wewe uliyeandika pia ni fundi. Lakini kwa haraka naona kiza mbele ya Chitemo,labda kama hana ubunifu tena. Na kama hilo ni kweli asubiri kuona ushindani mkubwa kwa,mafundi wenzie.
Thubutuuuu! Chitemo ana mtia vifungo wake huko visiwani ana matata hadi kwa Sultani. Hukusikia jinsi alivyobadili kola ya kanzu ya mfalme wa visiwa kiasi ikasuswa mwishowe ikajavaliwa na asiyehusika?
 
Michael Christopher Chitemo. Jina tunaandika kwa kuanza la ukoo inakua Chitemo Christopher Michael.

Mkubwa kiumbo = Tz ni kubwa kwa nchi zote za A. Mashariki.

Mafundi wengine = Ushindani wa vyam... Fack sijui kwanini kila kitu nakihusisha na siasa?
 
Fundi Chitemooo. Hata wewe uliyeandika pia ni fundi. Lakini kwa haraka naona kiza mbele ya Chitemo,labda kama hana ubunifu tena. Na kama hilo ni kweli asubiri kuona ushindani mkubwa kwa,mafundi wenzie.
Hakika mkuu, mafundi wengine wanatamani Sana kunivisha pia..
 
Michael Christopher Chitemo. Jina tunaandika kwa kuanza la ukoo inakua Chitemo Christopher Michael.

Mkubwa kiumbo = Tz ni kubwa kwa nchi zote za A. Mashariki.

Mafundi wengine = Ushindani wa vyam... Fack sijui kwanini kila kitu nakihusisha na siasa?
Hahahaha..! nacheka mzee mimi
 
Mkuu kabon14,tatizo lipo kwenu wote wateja wa huyo fundi Chitemo,na pia hata kwa wale wasio wateja wake pia wanahusika kwa kiasi fulani. Miaka yote nyie wateja wa fundi Chitemo mmekuwa mkiambiwa ukweli na wale wateja wa mafundi wengine na wale wasio na mafundi kabisa ambao wao hununua nguo dukani siku ya sikukuu ikifika kwa kuangalia sifa ya nguo kwa kipindi hicho (fashion) na si kuangalia yeye mteja anataka nini (tailor made). Wakati wateja wa mafundi wengine wakiwaambia nyie wateja wa fundi Chitemo kuwa fundi wenu ameshindwa kuenenda na fasheni,au hana ubunifu mpya,mliwakaripia sana na kuwaita majina mbalimbali huku mkisema ni wivu tu ndio unawasumbua,lakini mlisahau kuwa anayekwambia ukweli ili ujirejebishe ni mtu anayekutakia mema.
Mwisho napenda kusema kuwa wateja wa fundi Chitemo hamkuwa mnamueleza ukweli fundi mkiogopa kuwa ama anaweza kuwaharibia nguo zenu na hivyo mkashindwa kupendeza katika jamii,au mliogopa kumwambia ni mitindo gani mlitokuwa mnaitaka ambayo ingewatosha vyema na kupendezesha maumbo yenu. Siku nyingine msifikiri kuwa tatizo ni aina ya kitambaa anachochagua fundi Chitemo,bali ukweli ni kwamba fundi Chitemo amekwisha choka,na hakuna mteja hata mmoja anayeweza kumbadilisha zaidi ya mafundi wenzake endapo watakuja na staili nzuri za kuwapa imani wateja kuwa watawapendezesha zaidi ya fundi Chitemo,jambo ambalo kwa sasa bado hao mafundi akina Charles,Christian,Adam na wengine bado hawajaonyesha kwa sasa. Chitemo kaishiwa pumzi. Mbadala hawana staili mpya ya kuwaaminisha wateja kuwa watapendeza.
 
Chitemo mbishi Sana, Na Ana mbinu za siri anazo tumia maana nnahis hata nyuzi anazotumia Ni tofauti kabisaa
Chitemo kabadilika sana,aliniambia kuwa hatoniangusha lakini kinachoendelea sasa hivi ni mateso bila chuki.
Au mimi ndio sikumsikia vizuri jamani?
Chitemoooooo,ni chakula gani upewe ambacho kitakufanya ukumbe ulivyoniahidi kisha utekeleze?
 
Mkuu kabon14,tatizo lipo kwenu wote wateja wa huyo fundi Chitemo,na pia hata kwa wale wasio wateja wake pia wanahusika kwa kiasi fulani. Miaka yote nyie wateja wa fundi Chitemo mmekuwa mkiambiwa ukweli na wale wateja wa mafundi wengine na wale wasio na mafundi kabisa ambao wao hununua nguo dukani siku ya sikukuu ikifika kwa kuangalia sifa ya nguo kwa kipindi hicho (fashion) na si kuangalia yeye mteja anataka nini (tailor made). Wakati wateja wa mafundi wengine wakiwaambia nyie wateja wa fundi Chitemo kuwa fundi wenu ameshindwa kuenenda na fasheni,au hana ubunifu mpya,mliwakaripia sana na kuwaita majina mbalimbali huku mkisema ni wivu tu ndio unawasumbua,lakini mlisahau kuwa anayekwambia ukweli ili ujirejebishe ni mtu anayekutakia mema.
Mwisho napenda kusema kuwa wateja wa fundi Chitemo hamkuwa mnamueleza ukweli fundi mkiogopa kuwa ama anaweza kuwaharibia nguo zenu na hivyo mkashindwa kupendeza katika jamii,au mliogopa kumwambia ni mitindo gani mlitokuwa mnaitaka ambayo ingewatosha vyema na kupendezesha maumbo yenu. Siku nyingine msifikiri kuwa tatizo ni aina ya kitambaa anachochagua fundi Chitemo,bali ukweli ni kwamba fundi Chitemo amekwisha choka,na hakuna mteja hata mmoja anayeweza kumbadilisha zaidi ya mafundi wenzake endapo watakuja na staili nzuri za kuwapa imani wateja kuwa watawapendezesha zaidi ya fundi Chitemo,jambo ambalo kwa sasa bado hao mafundi akina Charles,Christian,Adam na wengine bado hawajaonyesha kwa sasa. Chitemo kaishiwa pumzi. Mbadala hawana staili mpya ya kuwaaminisha wateja kuwa watapendeza.
Umenena mkuu
 
Mmmmm sasa kama ilo ni fumbo basi mm sijafumbua.. Sasa naamini mimi KILAZA
sasa elewa mkuu! nakusaidia japo nkidakwa ntakatwa maksi zangu! Acha km mbwai na iwe mbwai.

magu,ccm,vyama pinzani,katiba,vyombo vya usalama,wapiga kura,.....wengine wajazie!....weka majina/maneno hayo utaelewa mkuu.
 
Fundi chitemo alichokosea kwa sasa hashauriki anachofikiria yeye ni hichohicho anadhani ule mwili wako wa miaka ile na sasa ni huo huo haujaongezeka, nakushauri acha kuvaa hii nguo na uwaambie wengine wasiende kwake nadhani itasaidia na mafundi wengine kutokubweteka na kulewa kwa kuwa ni wakongwe, 2020 siyo mbali box la kura
 
Ila huwezi jua labda Chitemo ataanza kukuelewa.
Lakin mkuu ujue natamani nivae nguo za mafundi wengine ila tatizo Ni kwamba chitemo Anambinu nyingi Sana za kuwashinda mafundi wenzake, maana inasemekana anauwezo wa kushona nguo bila kuangalia
 
Fundi chitemo alichokosea kwa sasa hashauriki anachofikiria yeye ni hichohicho anadhani ule mwili wako wa miaka ile na sasa ni huo huo haujaongezeka, nakushauri acha kuvaa hii nguo na uwaambie wengine wasiende kwake nadhani itasaidia na mafundi wengine kutokubweteka na kulewa kwa kuwa ni wakongwe, 2020 siyo mbali box la kura
Nishazeeka sasa , natamani mawazo ya wanangu Na wajukuu zangu wote yabadilike Ili kwa pamoja tushauriane jinsi ya kufanya maana nguo hii nilonayo inanitia fedheha sasa
 
Back
Top Bottom