Hongera kwa mawazo mbadala...ila kuhusu kuiangalia hiyo movie kwa upande wangu sijui.
Kila ninapotaka kuangalia movie za kibongo hua naishia mwanzoni.
Kuna vitu kama vile sound track,mwanga,sauti zisizopangiliwa, watu wasiobeba na kuwakilisha uhalisia (mtu akiigiza umasikini, anakuwa na sura ya kutia huruma, nani kasema masikini hana furaha?) na wengi wao wanaigiza kuwa wanaigiza vitu hivi huniboa mapema, ni movie chache sana naweza kuziangala moja ni kama hiyo ya Irene Sanga.
Pia watunzi wengi hawawapendi wahusika wao wote kwa usawa kulingana na nafasi zao. Utaona kabisa nyota wa filamu husika ameandaliwa mazingira yote ya kupendwa na audience, wakati washiriki wengine wanapotezewa hata maana ya uwepo wao kati filam husika.