Nimechanganyikwa jamani msaada!

You know mpaka mtu ana fight kukutoa Africa ng'ambo ujue pana kipengele hapo, ukizingatia nchi hizo zinavyobana kuachia njia kwa urahisi kwa mweusi kupita. Sasa ninarudi kwenye hoja kwamba, huyo jamaa anampenda mke wake ndo maana alidiriki kumchukua mpaka kiwanja badala ya kuwaachia wavimba macho na wakaanga sumu mkewe. Hata hivyo weka wazi pande zote mbili za shilingi kuujua undani naona kama kuna jambo jingine limejificha hapa kwani sababu ya lugha si ya kumfanya mume aseme maneno haya kwa mke, kwani hata kimada (concubine) huwezi mwambia maneno machafu na ya kejeli kiasi hicho, ...kinorway ndo nini? Hajui kama kuna Air-Craft Engineers wa Kirusi, Professors wa Kichina na hata Marais wasiojua Lugha nyingine zaidi ya lugha zao? Kama ameshindwa kumlisha mke na kumlazimisha kutafuta vibarua ambavyo mpaka asome kwanza, ni vyema aseme kwamba 'JAMANI SHAMBA LIMENISHINDA, ILI WATU WA KULIMA WAJE, MAANA WAPO. GARI LIKIKUSHINDA , SISI WAPIGA MISELE TUPO......Hebu tupatie mawasiliano ili tumshauri vilivyo tafadhali maana mambo mazuri hayapo huko tu
 
Title: Nimechanganykwa jamani msaada............. Is it about yourself?

Kama ni wewe mwenyewe pole sana dada yangu kaza moyo chunguza kama huyo mume anakupenda kiukwelii au la (kwangu mtu akupendaye akikukashifu kwa ajili ya kitu kidogo kama hiki cha wewe kumweleza udhaifu wako) hainiingii akilini.

Mwambie jinsi jibu lake lilivyokuathiri maana umesema hadi tendo la ndoa linakuwa gumu kwako. Ni heri akajua damage aliyoisababisha kwa majibu yake yasokuwa na utu. Kujifunza kitu kunategemea interest ya mtu na uwezo wake wa kuelewa sasa kama inakuwa ngumu kwa wewe kuelewa ni vema akalielewa hilo na kutafuta njia ya kukusaidia (ikiwa ni pamoja na kukufundisha yeye kwa upendo kwa sababu inaelekea yeye tayari ameshamaster lugha hiyo).

Sometime MJ1 unakuwaga kama shushushu,,,, anatuzuga ni mdada mmoja kumbe bwana ni yeye!lol alijuaje hata tendo la ndoa shida. Sema mume wangu kaniita norway natakiwa nijifunze kilugha cha huko na mimi ni mzito kwenye lugha tutakuelewa. Kona nyiingi! Kaza buti bibie jifunze lugha ufanye kazi. Jamaa anajutia faranga zake za ticket alizokutumia mkasaidiane kusaka maisha. Si bora kama angejua kilugha hakipandi angekutumia kamtaji ka mama ntilie uendelee kuka kibarazani!
 
Jamani asanteni sana kwa mawazo murua, kwa kweli dada ni mtu wa uganda kaolewa na mganda mwenzie. Ameshakaa huku mwaka na mwezi sasa. Ni kweli huyo bwana anaijua lugha vilivyo ila hapendi hata kuongea naye wakiwa pamoja maana yuko busy (for nothing)na misele yake...mmewe ni rafiki mkubwa wa mume wangu, so tuko karibu sana na huyo dada, naweza kusema mimi ndie niliyemfanya awe hapa mpaka leo, maana mwaka jana alitaka kurudi kwao...ukizingatia kinachomuuma zaidi ticket yenyewe alijilipia mwenyewe mpaka huku, maana alimwambia mmewe aende kumchukua akaanza kulalamika ni wastage ya pesa basi bibie akaamua kuchukua pesa zake za akiba akaja huku. Kinachomuuma zaidi ni kwamba aliacha kazi yake ya maana na worldbank.
 
Moods mmeniudhi sana...nilipoweka hii article kule mambo ya wakubwa nilikuwa namaana yangu. Maana mzee naye ni mpenzi mzuri huku ndani. ID yake naijua hajaomba kuingia kwenye chumba cha ma love maana ni mpenda siasa zaidi. So if possible can you muvuzisha this to mambo ya kikubwa please. Au nainze kucharanga ni norwigian!lol
 
Pole sana dada, mwambi shostito wako aende akajichanganye na weupe kwa sana atajua tuu.
 
Moods mmeniudhi sana...nilipoweka hii article kule mambo ya wakubwa nilikuwa namaana yangu. Maana mzee naye ni mpenzi mzuri huku ndani. ID yake naijua hajaomba kuingia kwenye chumba cha ma love maana ni mpenda siasa zaidi. So if possible can you muvuzisha this to mambo ya kikubwa please. Au nainze kucharanga ni norwigian!lol

Kwani mzee akiiona kuna tatizo? Nadhani atakupa credit kwa kuwa active member wa JF.
 
Binafsi kulazimishana kujifunza lugha za kikoloni ni zaidi ya utumwa.
Asanteni kwa michango yenu nilimpa dada ushauri mizuri mlionipa...ila katika mazungumzo alianza kuhisiwa eti anatembea na mwanafunzi mwenzake kisa tuu kamtambulisha kwa mr. wakiwa kwenye party alafu huyo dada akaondoka zake kurudi nyumbani na kumuacha mr. huko maana alishindwa kuvumili uchungu aliokuwa nao...mzee alimbadilikia nakuwa mkali kweli.
 
Huyo mume naye mshamba tu atamwambiaje laaziz wake maneno ya kashfa badala ya kumuinkareji!! Wanaume wengine bwana.........

Mama hiyo iwe changamoto ajifunze kwa bidii na amweleweshe huyo mume maana ya mke ni nini!! Kumleta ulaya isiwe chanzo cha kumnyanyasa ama!!

usiseme hivyo. Inafika pwent mtu unaboreka. Huyo mwanamke ni gunia la misumari. Hata ww mwanaume wako angekuboa
 
mnh makubwa,pale life linapoweka strain kny relationship...mnh pananogaje?:hatari:
 
Za leo wandugu wapendwa,

Napenda kuuliza swali tafadhali, hivi mwanamme anaishi Norway,ameamua kuoa mwanamke toka mfano kwetu Tanzania na kumpeleka huko wakaanze maisha pamoja. Then huyo bibie akaanza kusoma hiyo lugha ili aweze kupata kazi...lugha imegoma akamueleza mumewe hali halisi ili kama nikutafuta kazi nchi nyingine iwe hivyo. Huyo baba baada ya kuelezewa hayo akawa mkali nakutoa maneno ya kejeli kwa huyo mwanamke eti kama haiwezi lugha kaenda huko Norway kufanya nini! Kwa kweli huyo dada roho ilimuuma karibia ajinyonge. Je tunaweza kumsaadia vipi huyu bibie katika swala hili maana yaelekea mume ameshamuona mzigo sasa, ambayo imempelekea hata tendo la ndoa kuwa gumu kwake. Asanteni.

Mwambie huyo dada maisha sio lazima kwa huyo.mwanamme njaa!
Huyo jamaa amemgeuza mkewe kuwa kitega uchumi!?
Haya maanamme mengine bora hata yangezaliwa bata au kuku yangekuwa na faida kidogo!
Mwambie huyo aunty kama ana sheria ya huko (permanently status ktk passport yake) ahame aende England au France maisha safi tu!
Na kama uk unafanya kazi hata kama lugha yako sio nzuri sana!
Na hata hapo sweden akiwafuata wale wanaosaidia kina mama serikalini atapewa msaada! Mwambie akaseme kila kitu! Asifiche hata neno moja!
 
Hizi threads nyingine noma sana, hii ya miaka minne na ushee iliyopita!!!
 
yaani bado mnamshauri,pengine mwenzenu alishasahau kama alikuwa haijui lugha.
 
Hizi threads nyingine noma sana, hii ya miaka minne na ushee iliyopita!!!

Threads kama hizi zinatakiwa kufutwa tu!
Sisi wengine tunatumia jf on the move!
Hatuoni ni ya mwaka gani! Na hii app yao bado dhaifu mno!

Lkn tunakwenda kibongobongo tu!

What more could we do!!?
 
Za leo wandugu wapendwa,

Napenda kuuliza swali tafadhali, hivi mwanamme anaishi Norway,ameamua kuoa mwanamke toka mfano kwetu Tanzania na kumpeleka huko wakaanze maisha pamoja. Then huyo bibie akaanza kusoma hiyo lugha ili aweze kupata kazi...lugha imegoma akamueleza mumewe hali halisi ili kama nikutafuta kazi nchi nyingine iwe hivyo. Huyo baba baada ya kuelezewa hayo akawa mkali nakutoa maneno ya kejeli kwa huyo mwanamke eti kama haiwezi lugha kaenda huko Norway kufanya nini! Kwa kweli huyo dada roho ilimuuma karibia ajinyonge. Je tunaweza kumsaadia vipi huyu bibie katika swala hili maana yaelekea mume ameshamuona mzigo sasa, ambayo imempelekea hata tendo la ndoa kuwa gumu kwake. Asanteni.

By the time anakubali kuolewa nadhani alishapiga feasibility study ya maisha yake ya ndoa na akaona kuwa ni viable deal kwenda kuishi Norway. Sasa kwa sababu ashayavulia nguo hana budi kuyaoga.
Mungu amtie wepesi wa kuelewa lugha.
Hili ni fundisho kwa mabinti wote wa kibantu wanaong'ang'ania ndoa za ughaibuni kwa ajili ya kutafuta uslope kwenye maisha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom