Jambo pekee nitakalojifunza Vita ya UKRAINE na URUSI linaendana na funzo la viongozi wa TANZANIA kwa wananchi pia kwa majirani zako we msoma uzi

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Vita ya UKRAINE na URUSI imetawala katika vyombo kadhaa vya habari!!

Nina Funzo kubwa kwamba
USIJIWEKE WAZI KWA KILA JAMBO, KWANINI?

Urusi kutokuwa wazi sana na taarifa zake sahihi kutojulikana Kwa Magharibi
Kumesababisha asiingiliwe mipango yake mapema , kwasasa hakuna hasa anayejua Kama kweli nguvu tuliyokuwa tunaambiwa ya Urusi ni yenyewe Au kuna chumvi inaongezwa? Leo hii tunaona tulivyotarajia kwamba atamshambulia na kufika Kiev Kwa Muda mfupi sana Lakin ikawa ndivyo sivyo imechukua Muda mrefu sana sana kufika huko na Kwa hasara kubwa na bado akagonga Mwamba, Hii inaonesha kwamba Kumbe uwenda hana Uwezo tulioambiwa, ila wenye akili Timamu bado tunashtuka kwamba uwenda si kwamba katumia nguvu Zote anajilinda na kuhadaa ulimwengu kwamba aonekane ni MAKONDA asiye na cheo ? Yaan Joka Kibisa?

Ila wengine wanasema uwenda kaishiwa ndo maana anatangaza tenda a kupata wa kumsapot kwenye mapigano,

Kaenda china Kwa Siri bwana Shoigu kuomba msaada na msaada wenyewe ni wa kufanya biashara yake ishamiri wakati vita ikiendelea maana Ameonekana hana ujanja wa kufany biashara huku vita ikichapwa, Uchina wanaonekana wamekubali ila Kwa siri sana , na hii inafanya Nguvu ya UKIMYA NA SIRI kuendelea kutesa magharibi.

Pamoja na kwamba wamemspy na kujua Mipango ila CHUPI ya Urusi imegoma kuwaonesha Unyweleo hata mmoja wa Siri kama walivyo wanawake wa Arusha, imekuwa ngumu sana kama Chupa na mchwa! Lakin wao wanajifariji kwamba kutuna Kwa CHUPI ya Mwanamke ndo kunaashiria urefu wa Unyweleo wa ndani, hivo wanajua Nyembe zipi zitimike, ila wasiwasi unabaki kwamba wenda si Unyweleo bali ni Maumbile ya KIMISI ****

Umuhimu wa Ku toweka mambo wazi katika kumtesa mpinzani wako!

KWA UPANDE WA UKRAINE
Hakuna aliyetegemea Kama Atakomaa Hivi , Zelensky Kwa Putin amekuwa kama KASONGO kwenye Suruali ya anayekutana na hawala baadaye! Kutokujua hasa Taarifa zote za Maandalizi yake kumefanya UKRAINE imtese pia Putin mpaka akapanik, tunavyoongea hapa wameshakufa viongozi wa juu 9 wa Jeshi la Urusi , TUNZA SIRI JARIBU KUWA MKIMYA KWA MAMBO YAKO

MASOMO MENGINE
Imedhihirika kuwa tulikuwa hatujui. Tukiamua tunaweza kujua sasa. Tusidanganyike. Vita vya Urusi na Ukraine si vita vya Urusi na Ukraine bali ni vita kati ya Urusi kwa upande mmoja dhidi ya Marekani pamoja na Ulaya kwa upande wa pili. Kama kulikuwa na kiwingu cha kutoelewa mashindano yaliyopo duniani, sasa ndiyo wakati wa kuelewa. sisi wa Afrika tunacheza mdumange, a usingizi wa pono huku vijana wetu wa ki bet kwenye vita utadhani ni jambo Jena wakati wakubwa wana yao ya kugombea “usupa pawa” wa ulimwengu.

Sisi ni “mashuhuda tu na wa Kwenda kushadadia ” tu!
Vita hii ilivyoanza itufunze mambo Saba yafuatayo:
Wababe wako wawili duniani, sisi ni watoto na vita vyetu ni vya kitoto, Zaidi zaid vita yetu bado ni kupigania nani aingie Ikulu na nani awe waziri usimkaribishe adui “kupiga chabo” nyumba ya mkubwa, ukioolewa usimwache bwana wako wa kwanza kwenda kwa wa pili tena aliye adui wa unayetalikiana naye utabondwa* na hatimaye Waafrika tuache utoto tufunguke macho.

Najieleza.
Mosi, wababe wako wawili duniani, Urusi na Marekani tu. Vita viliyoanza majuzi vinatuambia kwamba duniani wababe wako wawili. Ni Urusi na Marekani, wao ndio ndovu wenyewe. Wengine hata NATO na nchi za Kiarabu ni kama simba tu mbugani. Ni kama chui tu. Ni kama mbwamwitu tu. Ni kama fisi tu. Ni kama mbweha tu. Wanatutisha tu wadogo zaidi, lakini kimsingi hawana ubavu ya pekee.

Wababe wawili wapo nyuma ya pazia. Wanagombea “unbigibraza” ulimwenguni. Wanagombea “usupapawa” ulimwenguni. Urusi inagombea kutamba duniani. Ni jogoo anayetaka atawale zizi na majike yote. Marekani naye anataka vivyo hivyo. Kila mmoja anaishi kwa kumwogopa na kutilia mashaka nyendo za mwenzake. Wanaviziana. Wanachunguzana.

Majogoo wanapigana kwa ajili ya kuzidaka nchi maskini. Urusi inataka majike wote (nchi kama zetu hizi, nchi lala hoi) na Marekani vivyo hivyo. Kumbe kazi ni kwetu kumkubali jogoo gani. Ashakum si matusi, sina lugha nzuri zaidi ya hii. Ukimkubalia Urusi, usimkubalie Marekani. Ukifanya hivyo tu utabondwa. Ukraine imenasa katika mkasa huu. Ashakum si matusi, wandugu, Ukraine ilikuwa chini ya Urusi, sasa “imetongozwa” na Marekani wakisaidiwa na wapambe wao nchi za Ulaya (na umoja wao wa ulinzi NATO), eti iachane na Urusi iolewe nyumba ya jirani, yaani na hasimu. Sasa inapigwa kwa sababu ya uchangudoa wake wa kisiasa. Hilo ndilo la kujifunza. Nakwambia ukimwona mtoto mwenzio anakatwa kwenzi na nguvu na kaka mkubwa, uliza kisa ufyate mkia.

Pili, sisi ni watoto na vita vyetu ni vya kitoto. Ugomvi wa Urusi na Marekani na magomvi ya sisi Waafrika ni magomvi yenye viwango viwili tofauti. Wao ni wa viwango vikubwa, wakati magomvi yetu ni ya viwango vya kitoto.
Urusi na Marekani zinagombea kuutawala ulimwengu, maana yake siyo dunia tu, wakati sisi tunavyogombea ni vitu vya hali ya chini kabisa. Wao wana mashindano makubwa kabisa hadi huko kwenye anga za juu, si tu kwa “satellites”, bali pia kwa roboti zao wanazotuma huko anga za juu. Urusi ina Roscosmos, Marekani ina NASA kuendesha mashindano ya anga za juu. Hata International Space Station (ISS) inayomilikiwa kwa pamoja na Marekani, Urusi, Japani, Canada na Mamlaka ya mambo ya Anga ya Ulaya, imegawanywa sehemu mbili. Ipo sehemu ya Marekani na ipo sehemu ya Urusi. Wao hawalali zizi moja.

Zamani walishindana kwenda mwezini, siku hizi si mali kitu. Siku hizi wanashindana kutuma roboti kwenye magimbe (sayari) za mbali: Mars, Jupiter, Venus na kadhalika. Marekani wametuma “curiosity skycrane” na “Preseverance” huko Mars, wametuma Juno huko Jupiter na kadhalika. Marekani inapofanya hivyo, Urusi hutuma roboti za familia ya Soyuz. Unaona wanavyogombea? Wanagombea vingine vyenye hadhi zaidi, wakati sisi tunagombana na mende, mijusi, bundi, popo, panya, paka na kadhalika eti kwamba ni mapepo wanaotumwa majumbani kwetu usiku na wachawi. Hivyo dhalili ndivyo tunavyokemea na kukosea usingizi; sisi kweli watoto. Yaani wakati sisi tunajilisha hadithi hewa za kuruka kwa fisi, nyungo, mbweha, “vipembe”, watu wana mashindano ya vyombo vya kweli angani.

Afadhali Waarabu wamejiwezea kutuma chombo kinachoitwa Amal (maana yake Matumaini) na Wachina wametuma chombo kinachoitwa Tianwen I (maana yake Njaa kwa Ukweli wa Mambo ya Angani). Sisi tupo tu na “bongo fleva” na sala za kukemea viumbe vya Mungu tulivyoambiwa tuvitawale (Mwa 1:26-28) na “wachawi” ambao si lolote isipokuwa chui wa makaratasi tu.

Pata picha yenye kukera hii. Eti sisi siku hizi hizi tunagombana na kuwakata mapanga na mashoka wazazi na bibi zetu eti kwa sababu wana macho mekundu na vibiongo nao wanaturoga tusiolewe au eti tusipate ajira, kweli sisi ni watoto. Wengine wetu tunagombana kwa sababu baadhi ni warefu na wengine ni wafupi, kama ilivyotokea Rwanda mwaka 1959 na 1994, kweli sisi ni watoto.

Wengine tunagombana kwa sababu baadhi ni Wakristo na wengine ni Waislamu na tunauana ili Mungu atupe pepo, kweli sisi ni watoto. Pepo gani tutaipata kwa kuchinjana? Hivi kuna baba yeyote ambaye atampa zawadi mtu aliyemuulia mtoto wake hata akiwa ni mwizi? Hivi Mungu ni mbaya tofauti baba binadamu? Hivi yeye aliyekataza kuua wanadamu anazawadiaje pepo wauaji?

Maswali niliyouliza jijibu mwenyewe. Acha tuendelee na hoja zetu. Ni hivi, kusudi kujipanga kwa ugomvi wao mkubwa na wa jadi, Urusi na Marekani wana silaha za hatari ambazo kwa sasa wamefichana. Ikifumuka vita ya kweli watafichuliana nasi tutaziona. Wana ndege za kivita za hatari. Kwa sasa ni siri zao. Wana mabomu ya kila nguvu, siyo tu mabomu ya atomiki bali pia makali zaidi yale yanayoitwa ya haidrojeni. Yaani staajabu hapo. Wakati wao wana silaha za ajabu, sisi tuna AK 47, ndege za kivita za zamani kama vile Mig 25, maroketi launcha ya kutupwa kwa mikono, nyengo, mikuki, mapanga na “vibonga.” Nacheka, jinsi tulivyobaki nyuma hivyo!

Ni hivi, ukitaka mfano, linganisha ugomvi wa Urusi na Marekani na majogoo wanaogombea majike, na magomvi yetu linganisha na magomvi ya vifaranga wanaomgombea senene aliyekatisha kati yao. Au linganisha ugomvi wa mawaziri wanaogombea umaarufu nchini na ugomvi wa watoto darasani wanaogombea kalamu yenye mfuto. Kifupi, ni magomvi ya viwango viwili tofauti sana. Magomvi ya kwetu ni ya kitoto sana. Nadhani nimewajuza jambo la msingi la pili.

Basi, tuwaache wapigane, hatuwezi kuwaamua wala kuwaingilia. Urusi imesema, atakayeingilia ugomvi wao, ataoneshwa cha mtema kuni kilichomtoa kanga manyoya. Katika onyo hili tunajulishwa kwamba msituni wenyewe ni ndovu, na si vinginevyo. Simba, mbwamwitu, fisi, tumbusi na kadhalika hawawezi kuingilia ugomvi wao ingawa wasipopigana ndovu wao huonekana kama wakali vile.

Tatu, kamwe usimkaribishe adui “kupiga chabo” nyumba ya mkubwa. Marekani inataka ikae Ukraine, kwa jina la NATO, iipige chabo Urusi. Urusi haitaki jambo hili na kamwe haitaruhusu. Urusi iliwahi kutaka kukaa nyumba za karibu na Marekani iipige chabo Marekani. Matokeo yake, wote waliojaribu kuikaribisha Urusi jirani ili iipige chabo Marekani walishapata tabu za mwaka. Cuba, Chile na kadhalika zimepata taabu kwa majaribio hayo. Ukitaka nenda ukawaulize wakusimulie.

Kwa upande wa Urusi, Afghastan, Syria, Iraki, Chechenia, Georgia, Crimea zimeshakiona cha moto na sasa hivi ndiyo tunasikia na kuiona Ukraine inavyonyeshewa mabomu. Kisa nyuma ya pazia ni kidogo tu. Marekani wanataka kuipiga chabo Urusi, wakitokea nyumba ya jirani, Ukraine. Urusi haikubali kuwa na adui upenuni au katika nyumba ya pili jirani. Ndipo Urusi ilishaiambia Ukraine isiikaribishe Marekani hapo hata kama inakuja kwa gia ya NATO. Urusi inajua NATO ni kisingizio tu. Kumbe, Ukraine ilishaonywa isifanye hivyo, isikie, sasa ndiyo inakiona cha moto.

Maana yake nini jambo hili? Maana yake ni fundisho kwa nchi zetu zote ndogo ndogo. Ukiikaribisha Marekani, ujue utageuka adui wa Urusi na kinyume chake ni kweli vile vile.

Jeuri ya Marekani ya kutaka “kuzipiga chabo” nchi wanazoziogopa hata China inajua, ndiyo maana China lazima itakuwa pamoja na Urusi. Kinachoendelea huko China, ashakum si matusi, ni kwamba Marekani “inaitongoza” Taiwani pale pale jirani. Marekani inataka ikae Taiwani kusudi “iipige chabo” China. Ndiyo maana, kwa shauri hili, Taiwani inatakiwa isuke au inyoe, ichague kubaki na China au iwakaribishe Marekani ikione cha moto.

Nne, ukioolewa usimwache bwana wako wa kwanza utabondwa, tena kwa mabomu yenye mabawa. Mataifa madogo madogo siye ni kama vijike vinavyogombewa na “mabwana”. Lakini nadhani hatujitambui vizuri. Ukraine haikuwa makini na ukweli huu. Ukraine si nchi ya ajabu, ni kama sisi tu. Ni maarufu kwa kulima mahindi na ngano tu, si zaidi. Sisi kama tuna dhahabu, almasi, urani, mafuta na gesi, tukikubali kuwapa Marekani, siku tutakapogeuka na kuwapa Urusi, tutakiona cha moto na kinyume chake kitakuwa kweli vile vile.

Siku ile sisi tutakapokuwa machangudoa wa kisiasa, mabwana watapigana kwenye ardhi yetu nasi tutaathirika vibaya. Kifupi, ni nchi yetu itakayotifuliwa, kuchomwa moto na kugeuzwa majivu. Kwa nini? Sasa sababu tunaijua: Wapiganapo fahali wawili ni nyasi zinazoumia. Ukweli wa jambo hili tutaushuhudia hivi karibu kama Urusi haitaamua kuacha kuicharaza Ukraine. Yaani siyo tu Ukraine itakayoumizwa ila hata nchi zetu. Nchi zetu zitapata shida ya ughali wa maisha kwa bei za gesi na mafuta zitakazochafuka na wale waliokuwa wanategemea kununua na kuuza kwa mabwana hao kutobaki tena kama kwanza.

Tano, tuache utoto tufunguke macho. Hili ni jambo lingine la kujifunza kutokana na vita inayoonekana kwa nje kama ya Urusi na Ukraine. Ni kwamba wengine tujipange, hasa nchi zetu za Kiafrika. Tushughulikie mambo mazito yenye maslahi kwetu, tuachane kutiana ulofa kwa mafundisho ya kijinga kama ya laana, mizimu, mapepo, majini na kadhalika.

Tuangalie ugomvi wa wababe, tujifunze kitu. Utasikia eti sisi tumelaaniwa kwa sababu wazee wetu waliiba mahindi. Tazama sasa wanaoiba vitu vyetu vikubwa: dhahabu, almasi, mafuta, gesi, urani na kadhalika wanapigana.

Watapigana na kuachana na wala hakuna atakayelaaniwa kwa dhambi hiyo. Utasikia eti nchi yetu imelaaniwa kwa sababu ya babu zetu kupigana kwenye vikao vya mbege, lubisi, wanzuki, kangala na gongo, wababe watapigana mbele yetu hata wakitaka wanaweza kuanzisha vita vya tatu vya dunia na kutuhusisha sote lakini hawatalaaniwa.

Basi, tuache kulofazana na kupeana akili ya Kinjikitile, badala yake tufungue macho. Maovu yanayotendeka duniani, kwa Mungu ni dhambi binafsi wala hayatengui miguu ya wanadamu wasioshiriki. Ubora na utu binafsi wa kila mwanadamu unabaki pale pale maana anayekula zabibu mbichi ndiye anayeumwa meno ganzi na si vinginevyo (Eze 18:1-32, Yer 31:29-30). Tafadhali tusieleze matatizo yetu kama laana kutokana na matendo ya wazee wetu. Tuwaache wazee wetu wapumzike kwa amani.

Sita, na mwisho, tujiweke tayari vyombo vya habari vya Marekani na Ulaya: CNN, VOA, Al Jazeera, BBC, DW na kadhalika kutudanganya. Wandugu, akili ya kuambiwa tuchanganye na yetu. Vitatudanganya ili Waafrika tuvutwe upande wa Marekani na Ulaya. Ndivyo ilivyotokea wakati wa vita vya Iraki na vita vya Siria.

Ndivyo tulivyodanganywa kwamba Patrick Lumumba wa Kongo, Kwame Nkurumah wa Ghana, Robert Mugabe wa Zimbabwe na kadhalika ni wabaya wakati haikuwa hivyo. Jambo hili linatokea kwa sababu, kwa bahati mbaya sana, vyombo vyetu vya habari havina uwezo wa kukusanya habari vyenyewe. Huwa vinatazama CNN, BBC, VOA, DW na kadhalika, kukopi na kisha kurudia habari hizo kwetu. Lakini vyombo vyetu vya habari husahau ukweli kwamba kila mwamba ngoma, ngozi huvutia kwake!

Tumwombe Mungu tusifikishwe kwenye vita kuu ya tatu ya dunia. Lakini uwezekano si mkubwa sana kwa sababu Marekani ni jogoo asiyetaka vita vipiganiwe kwenye ardhi yake isipokuwa ardhi za wengine tu.

Atasita kuvianzisha kwa sababu Urusi ina silaha zinazoweza kutua New York, Los Angeles, Atlanta na Chicago pia. Tusipofanya Kushtuka kuwa usitegemee wakubwa maskini Ukraine itataabika peke yake. Ni kama mke wa mtu aliyeshawishiwa na mwanaume fulani, wakati mumewe huyo mke atakapokuwa anampiga yule mwanaume anajificha konani.

Saba Funzo Kubwa ni kwamba Viongozi wetu wa Afrika hawana akili kubwa ya kuweza kujikwamua wao , na ukiangalia wengi wamepata kisingizio cha ugumu wa maisha ambao ulikuwapo kabla hata ya vita hii, cha kushangaza nchi zinazopigana vita zina mipango mikakati ya kuzuia mfumko wa bei ila sisi zetu wamekaa kusema hii vita hii ina madhara

Britanicca
 
Vita ni unity , mkiwa na umoja kamili hata kama mna silaha dhaifu kiasi gani , ushindi ni hakika , Ila mkitofautiana mitazamo tuu hata kama mna silaha nzito namna gani lazima mpigwe , Urusi Kwa sasa umoja wa kitaifa umepungua Kwa percentage kama 30 hv ,
 
Umeona mnaoangalia CNN, BBC, Al JaZEERA..

Fuatilien RT ambayo imeondolewa kwenye vingamuzi vyote duniani ili mdanganywe kama hivi..

Ukrane hawana umoja ,wale wanaoongea Kirusi wameungana na majeshi ya Urusi na Generali wao jana kairudisha Donbass yote..

Urusi kuna viongozi wa upinzani wanaopinga hiyo vita ndiyo walikuwa Wanahamasisah wanachama wao, leo mmoja amekamatwa kwenye uwanja wa ndege akitaka kukimbia..

Mitaa ya mingi Moscow imewekwa herufi Z na raia wanavaa tisheti zizoandikwa hivyo kuunga mkono majeshi ya Urusi yaliyopo huko..
 
Vita hazina formula..
Kama ulitegemea iishe ndani ya muda mfupi na ikawa ndivyo sivyo,si jambo la kushangaza..
Marekani aliingia Afghanistan 2001 Taleban ikiwa madarakani..Kakaa zaidi ya miaka 20.. Katoka Afghanistan kaiacha Taleban madarakani..
Kwa logic,Taleban hakutakiwa kuwepo kwenye uso wa dlDunia.

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
CNN, VOA, Al Jazeera, BBC, DW na kadhalika kutudanganya. Wandugu, akili ya kuambiwa tuchanganye na yetu. Vitatudanganya ili Waafrika tuvutwe upande wa Marekani na Ulaya. Ndivyo ilivyotokea wakati wa vita vya Iraki na vita vya Siria.
Mkuu,
Kwani kambi ya wakomunisti na wajamaa kama Urusi, China, Korea kaskazini, nk hawana vyombo vya habari?
Kama vipo, nani kavizuia kutangaza 'kweli' ?
Na je, vyombo vyao havitangazi uongo na kufanya propaganda kama TBC ya Tanzania?!!!
 
nyie si mmevipiga pini visionekane kwenye nyenzo zenu (you tube,google search n.k) kuwa vitahabarisha ukweli

kama kweli ndg yenu ( ukraine)hali kichapo kwanini mmevifungia?!!
 
😂😂
Hivi hujasikia kule Russia wananchi wa kawaida hawajui kinachojiri kwa majirani zao Ukraine, kwa sabb ya ukiritimba wa uongo na propaganda za vyombo vyao vya habari RT, TASS, nk kwa maelekezo ya Putin/Kremlin?

Halafu, nani kazuia 'supa pawa' TEAM Putin kupiga pini vyombo vya habari vya magharibi?
 
Usichokijua:
Kama isingekuwa operation mrusi angetumia siku 3 tu maana angeua hadi sisimizi.

Putin muungwana sana. Hataki kuua raia hata wanajeshi wa Ukraine hakutaka kuwaua. Ndio maana anatoa humanitarian corridors.

Wangekuwa wamagharibi unajua wanavyoua ovyo hadi njiwa pori.

Wasoviet wana huruma sana kwa raia
 
Mkuu wewe si umeishi Urussi tena kwa kazi maalumu hadi shemeji yetu anatokea pande hizo, hata wewe hujui Warusi wakoje.

Sasa hiyo kazi maalumu ulikuwa unafanyaje?
 
Mkuu idawa sisemi mimi kuijua Urusi nasema Marekani kuwajua Urusi,

Mimi kazi zangu si za Hawa CIA wala FBI hapana ni za vinchi vyetu Hivi ombaomba KAZI MAALUMU

Tuangazie Marekani mama akizindua Filamu sasa

Britanicca
 
Vita ya UKRAINE na URUSI imetawala katika vyombo kadhaa vya habari!!

Nina Funzo kubwa kwamba
USIJIWEKE WAZI KWA KILA JAMBO, KWANINI?

Urusi kutokuwa wazi sana na taarifa zake sahihi kutojulikana Kwa Magharibi
Kumesababisha asiingiliwe mipango yake mapema , kwasasa hakuna hasa anayejua Kama kweli nguvu tuliyokuwa tunaambiwa ya Urusi ni yenyewe Au kuna chumvi inaongezwa? Leo hii tunaona tulivyotarajia kwamba atamshambulia na kufika Kiev Kwa Muda mfupi sana Lakin ikawa ndivyo sivyo imechukua Muda mrefu sana sana kufika huko na Kwa hasara kubwa na bado akagonga Mwamba, Hii inaonesha kwamba Kumbe uwenda hana Uwezo tulioambiwa, ila wenye akili Timamu bado tunashtuka kwamba uwenda si kwamba katumia nguvu Zote anajilinda na kuhadaa ulimwengu kwamba aonekane ni MAKONDA asiye na cheo ? Yaan Joka Kibisa?

Ila wengine wanasema uwenda kaishiwa ndo maana anatangaza tenda a kupata wa kumsapot kwenye mapigano,

Kaenda china Kwa Siri bwana Shoigu kuomba msaada na msaada wenyewe ni wa kufanya biashara yake ishamiri wakati vita ikiendelea maana Ameonekana hana ujanja wa kufany biashara huku vita ikichapwa, Uchina wanaonekana wamekubali ila Kwa siri sana , na hii inafanya Nguvu ya UKIMYA NA SIRI kuendelea kutesa magharibi.

Pamoja na kwamba wamemspy na kujua Mipango ila CHUPI ya Urusi imegoma kuwaonesha Unyweleo hata mmoja wa Siri kama walivyo wanawake wa Arusha, imekuwa ngumu sana kama Chupa na mchwa! Lakin wao wanajifariji kwamba kutuna Kwa CHUPI ya Mwanamke ndo kunaashiria urefu wa Unyweleo wa ndani, hivo wanajua Nyembe zipi zitimike, ila wasiwasi unabaki kwamba wenda si Unyweleo bali ni Maumbile ya KIMISI ****

Umuhimu wa Ku toweka mambo wazi katika kumtesa mpinzani wako!

KWA UPANDE WA UKRAINE
Hakuna aliyetegemea Kama Atakomaa Hivi , Zelensky Kwa Putin amekuwa kama KASONGO kwenye Suruali ya anayekutana na hawala baadaye! Kutokujua hasa Taarifa zote za Maandalizi yake kumefanya UKRAINE imtese pia Putin mpaka akapanik, tunavyoongea hapa wameshakufa viongozi wa juu 9 wa Jeshi la Urusi , TUNZA SIRI JARIBU KUWA MKIMYA KWA MAMBO YAKO

MASOMO MENGINE
Imedhihirika kuwa tulikuwa hatujui. Tukiamua tunaweza kujua sasa. Tusidanganyike. Vita vya Urusi na Ukraine si vita vya Urusi na Ukraine bali ni vita kati ya Urusi kwa upande mmoja dhidi ya Marekani pamoja na Ulaya kwa upande wa pili. Kama kulikuwa na kiwingu cha kutoelewa mashindano yaliyopo duniani, sasa ndiyo wakati wa kuelewa. sisi wa Afrika tunacheza mdumange, a usingizi wa pono huku vijana wetu wa ki bet kwenye vita utadhani ni jambo Jena wakati wakubwa wana yao ya kugombea “usupa pawa” wa ulimwengu.

Sisi ni “mashuhuda tu na wa Kwenda kushadadia ” tu!
Vita hii ilivyoanza itufunze mambo Saba yafuatayo:
Wababe wako wawili duniani, sisi ni watoto na vita vyetu ni vya kitoto, Zaidi zaid vita yetu bado ni kupigania nani aingie Ikulu na nani awe waziri usimkaribishe adui “kupiga chabo” nyumba ya mkubwa, ukioolewa usimwache bwana wako wa kwanza kwenda kwa wa pili tena aliye adui wa unayetalikiana naye utabondwa* na hatimaye Waafrika tuache utoto tufunguke macho.

Najieleza.
Mosi, wababe wako wawili duniani, Urusi na Marekani tu. Vita viliyoanza majuzi vinatuambia kwamba duniani wababe wako wawili. Ni Urusi na Marekani, wao ndio ndovu wenyewe. Wengine hata NATO na nchi za Kiarabu ni kama simba tu mbugani. Ni kama chui tu. Ni kama mbwamwitu tu. Ni kama fisi tu. Ni kama mbweha tu. Wanatutisha tu wadogo zaidi, lakini kimsingi hawana ubavu ya pekee.

Wababe wawili wapo nyuma ya pazia. Wanagombea “unbigibraza” ulimwenguni. Wanagombea “usupapawa” ulimwenguni. Urusi inagombea kutamba duniani. Ni jogoo anayetaka atawale zizi na majike yote. Marekani naye anataka vivyo hivyo. Kila mmoja anaishi kwa kumwogopa na kutilia mashaka nyendo za mwenzake. Wanaviziana. Wanachunguzana.

Majogoo wanapigana kwa ajili ya kuzidaka nchi maskini. Urusi inataka majike wote (nchi kama zetu hizi, nchi lala hoi) na Marekani vivyo hivyo. Kumbe kazi ni kwetu kumkubali jogoo gani. Ashakum si matusi, sina lugha nzuri zaidi ya hii. Ukimkubalia Urusi, usimkubalie Marekani. Ukifanya hivyo tu utabondwa. Ukraine imenasa katika mkasa huu. Ashakum si matusi, wandugu, Ukraine ilikuwa chini ya Urusi, sasa “imetongozwa” na Marekani wakisaidiwa na wapambe wao nchi za Ulaya (na umoja wao wa ulinzi NATO), eti iachane na Urusi iolewe nyumba ya jirani, yaani na hasimu. Sasa inapigwa kwa sababu ya uchangudoa wake wa kisiasa. Hilo ndilo la kujifunza. Nakwambia ukimwona mtoto mwenzio anakatwa kwenzi na nguvu na kaka mkubwa, uliza kisa ufyate mkia.

Pili, sisi ni watoto na vita vyetu ni vya kitoto. Ugomvi wa Urusi na Marekani na magomvi ya sisi Waafrika ni magomvi yenye viwango viwili tofauti. Wao ni wa viwango vikubwa, wakati magomvi yetu ni ya viwango vya kitoto.
Urusi na Marekani zinagombea kuutawala ulimwengu, maana yake siyo dunia tu, wakati sisi tunavyogombea ni vitu vya hali ya chini kabisa. Wao wana mashindano makubwa kabisa hadi huko kwenye anga za juu, si tu kwa “satellites”, bali pia kwa roboti zao wanazotuma huko anga za juu. Urusi ina Roscosmos, Marekani ina NASA kuendesha mashindano ya anga za juu. Hata International Space Station (ISS) inayomilikiwa kwa pamoja na Marekani, Urusi, Japani, Canada na Mamlaka ya mambo ya Anga ya Ulaya, imegawanywa sehemu mbili. Ipo sehemu ya Marekani na ipo sehemu ya Urusi. Wao hawalali zizi moja.

Zamani walishindana kwenda mwezini, siku hizi si mali kitu. Siku hizi wanashindana kutuma roboti kwenye magimbe (sayari) za mbali: Mars, Jupiter, Venus na kadhalika. Marekani wametuma “curiosity skycrane” na “Preseverance” huko Mars, wametuma Juno huko Jupiter na kadhalika. Marekani inapofanya hivyo, Urusi hutuma roboti za familia ya Soyuz. Unaona wanavyogombea? Wanagombea vingine vyenye hadhi zaidi, wakati sisi tunagombana na mende, mijusi, bundi, popo, panya, paka na kadhalika eti kwamba ni mapepo wanaotumwa majumbani kwetu usiku na wachawi. Hivyo dhalili ndivyo tunavyokemea na kukosea usingizi; sisi kweli watoto. Yaani wakati sisi tunajilisha hadithi hewa za kuruka kwa fisi, nyungo, mbweha, “vipembe”, watu wana mashindano ya vyombo vya kweli angani.

Afadhali Waarabu wamejiwezea kutuma chombo kinachoitwa Amal (maana yake Matumaini) na Wachina wametuma chombo kinachoitwa Tianwen I (maana yake Njaa kwa Ukweli wa Mambo ya Angani). Sisi tupo tu na “bongo fleva” na sala za kukemea viumbe vya Mungu tulivyoambiwa tuvitawale (Mwa 1:26-28) na “wachawi” ambao si lolote isipokuwa chui wa makaratasi tu.

Pata picha yenye kukera hii. Eti sisi siku hizi hizi tunagombana na kuwakata mapanga na mashoka wazazi na bibi zetu eti kwa sababu wana macho mekundu na vibiongo nao wanaturoga tusiolewe au eti tusipate ajira, kweli sisi ni watoto. Wengine wetu tunagombana kwa sababu baadhi ni warefu na wengine ni wafupi, kama ilivyotokea Rwanda mwaka 1959 na 1994, kweli sisi ni watoto.

Wengine tunagombana kwa sababu baadhi ni Wakristo na wengine ni Waislamu na tunauana ili Mungu atupe pepo, kweli sisi ni watoto. Pepo gani tutaipata kwa kuchinjana? Hivi kuna baba yeyote ambaye atampa zawadi mtu aliyemuulia mtoto wake hata akiwa ni mwizi? Hivi Mungu ni mbaya tofauti baba binadamu? Hivi yeye aliyekataza kuua wanadamu anazawadiaje pepo wauaji?

Maswali niliyouliza jijibu mwenyewe. Acha tuendelee na hoja zetu. Ni hivi, kusudi kujipanga kwa ugomvi wao mkubwa na wa jadi, Urusi na Marekani wana silaha za hatari ambazo kwa sasa wamefichana. Ikifumuka vita ya kweli watafichuliana nasi tutaziona. Wana ndege za kivita za hatari. Kwa sasa ni siri zao. Wana mabomu ya kila nguvu, siyo tu mabomu ya atomiki bali pia makali zaidi yale yanayoitwa ya haidrojeni. Yaani staajabu hapo. Wakati wao wana silaha za ajabu, sisi tuna AK 47, ndege za kivita za zamani kama vile Mig 25, maroketi launcha ya kutupwa kwa mikono, nyengo, mikuki, mapanga na “vibonga.” Nacheka, jinsi tulivyobaki nyuma hivyo!

Ni hivi, ukitaka mfano, linganisha ugomvi wa Urusi na Marekani na majogoo wanaogombea majike, na magomvi yetu linganisha na magomvi ya vifaranga wanaomgombea senene aliyekatisha kati yao. Au linganisha ugomvi wa mawaziri wanaogombea umaarufu nchini na ugomvi wa watoto darasani wanaogombea kalamu yenye mfuto. Kifupi, ni magomvi ya viwango viwili tofauti sana. Magomvi ya kwetu ni ya kitoto sana. Nadhani nimewajuza jambo la msingi la pili.

Basi, tuwaache wapigane, hatuwezi kuwaamua wala kuwaingilia. Urusi imesema, atakayeingilia ugomvi wao, ataoneshwa cha mtema kuni kilichomtoa kanga manyoya. Katika onyo hili tunajulishwa kwamba msituni wenyewe ni ndovu, na si vinginevyo. Simba, mbwamwitu, fisi, tumbusi na kadhalika hawawezi kuingilia ugomvi wao ingawa wasipopigana ndovu wao huonekana kama wakali vile.

Tatu, kamwe usimkaribishe adui “kupiga chabo” nyumba ya mkubwa. Marekani inataka ikae Ukraine, kwa jina la NATO, iipige chabo Urusi. Urusi haitaki jambo hili na kamwe haitaruhusu. Urusi iliwahi kutaka kukaa nyumba za karibu na Marekani iipige chabo Marekani. Matokeo yake, wote waliojaribu kuikaribisha Urusi jirani ili iipige chabo Marekani walishapata tabu za mwaka. Cuba, Chile na kadhalika zimepata taabu kwa majaribio hayo. Ukitaka nenda ukawaulize wakusimulie.

Kwa upande wa Urusi, Afghastan, Syria, Iraki, Chechenia, Georgia, Crimea zimeshakiona cha moto na sasa hivi ndiyo tunasikia na kuiona Ukraine inavyonyeshewa mabomu. Kisa nyuma ya pazia ni kidogo tu. Marekani wanataka kuipiga chabo Urusi, wakitokea nyumba ya jirani, Ukraine. Urusi haikubali kuwa na adui upenuni au katika nyumba ya pili jirani. Ndipo Urusi ilishaiambia Ukraine isiikaribishe Marekani hapo hata kama inakuja kwa gia ya NATO. Urusi inajua NATO ni kisingizio tu. Kumbe, Ukraine ilishaonywa isifanye hivyo, isikie, sasa ndiyo inakiona cha moto.

Maana yake nini jambo hili? Maana yake ni fundisho kwa nchi zetu zote ndogo ndogo. Ukiikaribisha Marekani, ujue utageuka adui wa Urusi na kinyume chake ni kweli vile vile.

Jeuri ya Marekani ya kutaka “kuzipiga chabo” nchi wanazoziogopa hata China inajua, ndiyo maana China lazima itakuwa pamoja na Urusi. Kinachoendelea huko China, ashakum si matusi, ni kwamba Marekani “inaitongoza” Taiwani pale pale jirani. Marekani inataka ikae Taiwani kusudi “iipige chabo” China. Ndiyo maana, kwa shauri hili, Taiwani inatakiwa isuke au inyoe, ichague kubaki na China au iwakaribishe Marekani ikione cha moto.

Nne, ukioolewa usimwache bwana wako wa kwanza utabondwa, tena kwa mabomu yenye mabawa. Mataifa madogo madogo siye ni kama vijike vinavyogombewa na “mabwana”. Lakini nadhani hatujitambui vizuri. Ukraine haikuwa makini na ukweli huu. Ukraine si nchi ya ajabu, ni kama sisi tu. Ni maarufu kwa kulima mahindi na ngano tu, si zaidi. Sisi kama tuna dhahabu, almasi, urani, mafuta na gesi, tukikubali kuwapa Marekani, siku tutakapogeuka na kuwapa Urusi, tutakiona cha moto na kinyume chake kitakuwa kweli vile vile.

Siku ile sisi tutakapokuwa machangudoa wa kisiasa, mabwana watapigana kwenye ardhi yetu nasi tutaathirika vibaya. Kifupi, ni nchi yetu itakayotifuliwa, kuchomwa moto na kugeuzwa majivu. Kwa nini? Sasa sababu tunaijua: Wapiganapo fahali wawili ni nyasi zinazoumia. Ukweli wa jambo hili tutaushuhudia hivi karibu kama Urusi haitaamua kuacha kuicharaza Ukraine. Yaani siyo tu Ukraine itakayoumizwa ila hata nchi zetu. Nchi zetu zitapata shida ya ughali wa maisha kwa bei za gesi na mafuta zitakazochafuka na wale waliokuwa wanategemea kununua na kuuza kwa mabwana hao kutobaki tena kama kwanza.

Tano, tuache utoto tufunguke macho. Hili ni jambo lingine la kujifunza kutokana na vita inayoonekana kwa nje kama ya Urusi na Ukraine. Ni kwamba wengine tujipange, hasa nchi zetu za Kiafrika. Tushughulikie mambo mazito yenye maslahi kwetu, tuachane kutiana ulofa kwa mafundisho ya kijinga kama ya laana, mizimu, mapepo, majini na kadhalika.

Tuangalie ugomvi wa wababe, tujifunze kitu. Utasikia eti sisi tumelaaniwa kwa sababu wazee wetu waliiba mahindi. Tazama sasa wanaoiba vitu vyetu vikubwa: dhahabu, almasi, mafuta, gesi, urani na kadhalika wanapigana.

Watapigana na kuachana na wala hakuna atakayelaaniwa kwa dhambi hiyo. Utasikia eti nchi yetu imelaaniwa kwa sababu ya babu zetu kupigana kwenye vikao vya mbege, lubisi, wanzuki, kangala na gongo, wababe watapigana mbele yetu hata wakitaka wanaweza kuanzisha vita vya tatu vya dunia na kutuhusisha sote lakini hawatalaaniwa.

Basi, tuache kulofazana na kupeana akili ya Kinjikitile, badala yake tufungue macho. Maovu yanayotendeka duniani, kwa Mungu ni dhambi binafsi wala hayatengui miguu ya wanadamu wasioshiriki. Ubora na utu binafsi wa kila mwanadamu unabaki pale pale maana anayekula zabibu mbichi ndiye anayeumwa meno ganzi na si vinginevyo (Eze 18:1-32, Yer 31:29-30). Tafadhali tusieleze matatizo yetu kama laana kutokana na matendo ya wazee wetu. Tuwaache wazee wetu wapumzike kwa amani.

Sita, na mwisho, tujiweke tayari vyombo vya habari vya Marekani na Ulaya: CNN, VOA, Al Jazeera, BBC, DW na kadhalika kutudanganya. Wandugu, akili ya kuambiwa tuchanganye na yetu. Vitatudanganya ili Waafrika tuvutwe upande wa Marekani na Ulaya. Ndivyo ilivyotokea wakati wa vita vya Iraki na vita vya Siria.

Ndivyo tulivyodanganywa kwamba Patrick Lumumba wa Kongo, Kwame Nkurumah wa Ghana, Robert Mugabe wa Zimbabwe na kadhalika ni wabaya wakati haikuwa hivyo. Jambo hili linatokea kwa sababu, kwa bahati mbaya sana, vyombo vyetu vya habari havina uwezo wa kukusanya habari vyenyewe. Huwa vinatazama CNN, BBC, VOA, DW na kadhalika, kukopi na kisha kurudia habari hizo kwetu. Lakini vyombo vyetu vya habari husahau ukweli kwamba kila mwamba ngoma, ngozi huvutia kwake!

Tumwombe Mungu tusifikishwe kwenye vita kuu ya tatu ya dunia. Lakini uwezekano si mkubwa sana kwa sababu Marekani ni jogoo asiyetaka vita vipiganiwe kwenye ardhi yake isipokuwa ardhi za wengine tu.

Atasita kuvianzisha kwa sababu Urusi ina silaha zinazoweza kutua New York, Los Angeles, Atlanta na Chicago pia. Tusipofanya Kushtuka kuwa usitegemee wakubwa maskini Ukraine itataabika peke yake. Ni kama mke wa mtu aliyeshawishiwa na mwanaume fulani, wakati mumewe huyo mke atakapokuwa anampiga yule mwanaume anajificha konani.

Saba Funzo Kubwa ni kwamba Viongozi wetu wa Afrika hawana akili kubwa ya kuweza kujikwamua wao , na ukiangalia wengi wamepata kisingizio cha ugumu wa maisha ambao ulikuwapo kabla hata ya vita hii, cha kushangaza nchi zinazopigana vita zina mipango mikakati ya kuzuia mfumko wa bei ila sisi zetu wamekaa kusema hii vita hii ina madhara

Britanicca
Mkuu bado msimamo wako ni huu? Mataifa makubwa 54 yanatoa silaha. Ushauri, mamluki lakini pumzi ya moto wameiona?

Vikwazo vya kiuchumi na kijeshi zaidi ya 13,000 hakuna nchi yeyote duniani imewahi kuwekewa vikwazo vingi hivyo bado imeweza kuendelea kupigana na uchumi umekuwa?

Hebu fikiria Israel huu mwezi4 sasa eneo sawa na wilaya ya kigamboni. Wameshindwa kupambana na hamasi badalà yake wanaua raia tu. Tupe tafsiri yake na ulinganishe na Urusi vs Ukraine
 
Back
Top Bottom