Nimechanganyikwa jamani msaada! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimechanganyikwa jamani msaada!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by 007/Mrs.bond, May 27, 2009.

 1. 007/Mrs.bond

  007/Mrs.bond Member

  #1
  May 27, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Za leo wandugu wapendwa,

  Napenda kuuliza swali tafadhali, hivi mwanamme anaishi Norway,ameamua kuoa mwanamke toka mfano kwetu Tanzania na kumpeleka huko wakaanze maisha pamoja. Then huyo bibie akaanza kusoma hiyo lugha ili aweze kupata kazi...lugha imegoma akamueleza mumewe hali halisi ili kama nikutafuta kazi nchi nyingine iwe hivyo. Huyo baba baada ya kuelezewa hayo akawa mkali nakutoa maneno ya kejeli kwa huyo mwanamke eti kama haiwezi lugha kaenda huko Norway kufanya nini! Kwa kweli huyo dada roho ilimuuma karibia ajinyonge. Je tunaweza kumsaadia vipi huyu bibie katika swala hili maana yaelekea mume ameshamuona mzigo sasa, ambayo imempelekea hata tendo la ndoa kuwa gumu kwake. Asanteni.
   
 2. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mrs Bond;

  Huyo dada amekata tamaa mapema sana na sijui ni kwa nini. Huwezi ukahama Nchi eti kwa sababu huijui lugha ya wenyeji hasa katika dunia hii ya Utandawazi. Watu wanajifunza Kichina itakuwa Kinorway?

  Nina dada Yangu aliolewa na Mdanish na wakahamia huko Mwaka 1999. Haikumchukua zaidi ya Mwaka kujifunza Ki-Danish na leo hii anaongea kama lugha yake ya Kwanza.

  Mshauri asikate tamaa, ajitahidi tu. Hakuna kisichowezekana!
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  May 28, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Huyo mume naye mshamba tu atamwambiaje laaziz wake maneno ya kashfa badala ya kumuinkareji!! Wanaume wengine bwana.........

  Mama hiyo iwe changamoto ajifunze kwa bidii na amweleweshe huyo mume maana ya mke ni nini!! Kumleta ulaya isiwe chanzo cha kumnyanyasa ama!!
   
 4. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Jiulize maswali kadhaa:
  Je kujiua kutatoa solution gani katika maisha yangu?
  Ni lazima kuishi na huyu mwanaume?
  Solution ni tafuta maisha yako mwenyewe dada. People will always disappoint u!
  Wanawake mnataka haki sawa. kujitafutia maisha yako binafsi ni moja ya haki sawa mtakazo.
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyo mwanaume amesha onja mambo yetu yaleeeeeeeeeeeeee.
  Kama vp nae ampe au amuonjeshe aone kama atabadilika au lah.
   
 6. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  we naye utashindwaje kujifunza kugha, hata kama mimi nakupiga chini huna maana kabisa - unapewa opportunity unaanza kulia lia, bora ujinyonge kwa kweli.,
   
 7. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ukitaka tamu utaonja shubiri, si aliona kiswahili sio dili akaona bora ajizungu kilugha sasa analalamika nini! Ajifunze tu kwa nguvu zote, akiendelea na kuona kwake aibu eti cwezi oh hoo! Atatemeshwa mzigo, tuje 2sage lami pamoja huku bongo asidilei mwambie, na ka mko karibu jtahidi kumpa moyo, au ka vp?...... Enh! Si mwanakwenu huyo why apate tabu kwa bepari hali upoo!
   
 8. Offish

  Offish Senior Member

  #8
  May 28, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mwambie uamzi anaotaka kuuchukua haufai na ni wa aibu kabisa kwake, kwako na wengine wote walio karibu naye; asiwe mtu wa kukata tamaa kwani kushindwa kuzungumza lugha fulani wala mume sio mwisho wa dunia yake. Bado ana fursa kibao za mafanikio kama kweli hiyo 'ready-made' iliyo mbele yake imemshinda. Mafanikio sio lazima ayapate Ulaya, hata aklirudi anaweza kuwin kuliko huko aliko
   
 9. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwani amesema anataka kujiua?
  ni lazima kuishi na huyo mwanaume kwa sababu ni mume wake na anampenda.
  ndo anatafuta maisha hivyo kwa kujifunza lugha then atafute kazi na yeye awe na pesa yake.

  Kilichotakiwa ni huyo mwanaume kumtia moyo ajifunze kwa bidii atazoea tu, na dada naye ajitahidi wakati mwingine kichwa kinakataa lakini atajua polepole, na mbona hujatuuambia amejifunza muda gani?
  inaweza ikawa ni wiki miezi mitatu tu kwa lugha ya watu ni mdogo sana.atajua tu bwana hayo huyo bwana kashampata mwingine anatafuta sababu maana wanaume?
   
 10. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hajamwambia nataka hayo mambo amemwambia ajifunze lugha.
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mambo gani_?
   
 12. D

  Dina JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2009
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mmh jamani, mwambie mdada akaze msuli, mbona anakata tamaa mapema?
   
 13. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  achague kati ya haya:
  1. Kukakamaa ajifunze lugha mpaka kieleweke
  2. Arudi bongo maana huko hataweza kama lugha haipandi na anahitaji kazi
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Binafsi kulazimishana kujifunza lugha za kikoloni ni zaidi ya utumwa.
   
 15. D

  Dina JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2009
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mmh jamani, mwambie mdada akaze msuli ajifunze lugha, mbona anakata tamaa mapema? Siku zote penye nia pana njia...
   
 16. D

  Dina JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2009
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kama ni utumwa, basi arudi nyumbani alikojua kiswahili bila kufundishwa!
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Inategemea mdau kama anapenda utumwa au la..lakini my personal standing ni kukataa utumwa.
   
 18. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #18
  May 28, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Title: Nimechanganykwa jamani msaada............. Is it about yourself?

  Kama ni wewe mwenyewe pole sana dada yangu kaza moyo chunguza kama huyo mume anakupenda kiukwelii au la (kwangu mtu akupendaye akikukashifu kwa ajili ya kitu kidogo kama hiki cha wewe kumweleza udhaifu wako) hainiingii akilini.

  Mwambie jinsi jibu lake lilivyokuathiri maana umesema hadi tendo la ndoa linakuwa gumu kwako. Ni heri akajua damage aliyoisababisha kwa majibu yake yasokuwa na utu. Kujifunza kitu kunategemea interest ya mtu na uwezo wake wa kuelewa sasa kama inakuwa ngumu kwa wewe kuelewa ni vema akalielewa hilo na kutafuta njia ya kukusaidia (ikiwa ni pamoja na kukufundisha yeye kwa upendo kwa sababu inaelekea yeye tayari ameshamaster lugha hiyo).
   
 19. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #19
  May 28, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Huyo Mwanaume anaishi nae ni Mtanzania?
   
 20. M

  Misana Member

  #20
  May 28, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dada. mwambie mambo ya lugha hayataki haraka na asi-give up mapema namna hiyo. kuna msemo unasema - what you think is impossible is always possible. Aendelee kijifunza taratibu and i believe within 6 months to 1 year atajikuja anaongea mpaka matusi yote ya ki-norge. Asionyeshe kushindwa. Naye huyo mume wake anatakiwa pia akirudi nyumbani ajaribu kumsaidia maana yeye tayari anakijua, hat kumwita tu "njoo" "tulia" kula" every day watajikuta wanakiongea kuliko kichaga huku kwetu. Ila asijinyonge ni bora ajirudie zake huku kwenye mabomu ya Mbagala.
   
Loading...