Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
NIMEBAINI WATANZANIA NI VINARA(SUPERPOWER) WA MAMBO HAYA;

Anaandika Robert Heriel.

Kwa wasomi wa somo la Historia watakubaliana nami kuwa hapa Duniani kuna mataifa ni superpower na yapo yalikuwa hivyo. Mpaka sasa taifa la Marekani ndio superpower wa Dunia yetu huku taifa la Uchina likimpa changamoto ya kutaka kupindua meza. Mataifa mengine yaliyowahi kuwa superpower ni pamoja na Uingereza, Ujerumani, ufaransa, Uturuki, Roma, Ashuru, Misri, Uyunani, umedi na uajemi.

Ili taifa liwe superpower linapaswa liwe linaongoza kiuchumi, kiteknolojia, kiushawishi duniani wa Masuala ya diplomasia na Siasa, kiutamaduni, kiviwanda, kijeshi miongoni mwa mambo mengine.

Mwaka huu sitaki kuwachosha Kwa maandishi mengi.
Leo nataka kuitangaza Tanzania na wananchi wake kuwa ni vinara katika mambo Yafuatayo;

1. UNAFIKI
Taifa letu sijui lijivunie au lione haya Kwa kuongoza Kwa kuwa na watu wanafiki.
Jamani! Sisi ni wanafiki na katika hilo tunalimudu na hakuna taifa lolote linaloweza kukatiza na kutushinda katika hilo.

Unafik unaanzia kwenye malezi Kwa Baba na Mama huko, kisha shuleni baadaye mtaani na huho serikalini.
Huko kwenye dini ndio usiseme. Ni unafiki mtupu.

Vijiweni ukikaa ni unafiki mtupu! Kusengenyana na kujadili maisha ya watu. Ukiondoka unasemwa A to Z. Nawe wakiondoka unawasema. Watanzania ni nadra Sana kumchana mtu makavu. Wengi wanaunafki hivyo wanashindwa kum-face mtu na kumchana.

Maofisini huko ndio usisem. Unafiki! Unafiki mtupu! Usiombe ukawa Kiongozi hasa wa ngazi za juu Kama Rais au nafasi yoyote ya juu. Utanafikiwa wewe mpaka ukome. Utasifiwa na kutukuzwa mpaka useme yeleuwiiii!
Subiri uachie ngazi ndio utajua maharage ni mboga na bamia ni gundi.

Unafik! Unafiki mtupu! Tumebobea kwenye unafiki. Ukipata vipesa kidogo watu watakushobokea na kukutukuza Kama mungu mtu.

Ukitaka ujue Dalili nyingine ya mtu mnafiki ni ku-fake life. Watanzania wanaile Dhana kuwa Utanashati huficha umasikini 😀😀 yaani unafiki unafiki tu. Yaani mtu Avae vizuri ili aonekane anapesa kumbe Hana😀 huoni hilo ni tatizo. Huo ndio unafiki wenyewe. Ku-fake life ndio unafiki wa kiwango cha juu kabisa.

Mtanzania akija kuomba umkopeshe au kuomba kazi atakavyokuigizia utasema mtu si ndio huyu. Kumbe Unafiki mtupu. Ngoja apate anachokitaka hutaamini na macho yako. Ni ushenzi mtupu.

Ndio maana niliandikaga mahali fulani kusema usisaidia Masikini Acha Wafe.

Ogopa mtu anayejiliza Liza, ogopa mtu anayejitilisha huruma huruma hasa akiwa mtanzania mwenzako ni Unafik mtupuuu!

2. Uvivu na Kupenda vya Bure
Sisi Watanzania jamani tuache kuonekana haya tuseme ukweli. Sisi ni wavivu hasa. Wengi wetu ni watu wapenda vitu rahisi. Kupenda vya Bure.

Ndio maana hatuachi na hatuchoki kulalamika. Yaani tunalalamika na hiyo ni moja ya sifa ya mtu mvivu WA KAZI na kufikiri.

Watanzania wengi wetu tunapenda mambo ya bure bure, kufanyiwa fanyiwa kila kitu. Kutafuniwa na kumezewa kila kitu.

Watanzania wengi wetu hatuna ule uwezo wa kufanya kazi masaa nane mfululizo kila siku wengi tukijitahidi Sana ni masaa manne Kam sio matatu tena chini ya uangalizi mkali Sana.

Mtanzania bila kumsimamia tena usimamizi mkali nakuhakikishia hakuna kazi itafanyika. KAZI YA siku mbili itafanywa wiki mbili Kama sio tatu. Nenda maofisini huko ukakae benchi ishu ya Lisaa limoja usishangae likakumalizia siku nzima Kama sio siku mbili mpaka tatu.

Ukitaka ujue Watanzania wengi ni wavivu na wapenda bure bure angalia unaweza ukapita mtaani huko unashangaa mtu mwenye nguvu kabisa akikuomba ati Mia mbili au nauli. Loooh.

Angalia unakuta kwenye familia ya watu Saba mpaka nane. Sio ajabu anategemewa mtu mmoja au wawili. Wengine kazi kupika na Kula na kulala alafu ni watu wazima kabisa wenye umri wa kujitegemea. Ukiwauliza wanakuambia hakuna kazi. Ukimtafutia kazi anakuambia Mshahara Mdogo wakati shule halijaenda, elimu duni.

Haya hata Kama shule umeenda ndio uone Bora kulishwa na kunyonya nguvu za wenzako kisa hutaki kazi zenye mishahara midogo. Bora kipi? Kufanya kazi yenye Mshahara mdogo au kujiajiri vibiashara mshenzi ili ujilishe na kujitegemea mwenye kuliko ukalishe ndevu Kwa watu.

Uvivu mtupu! Mtupu! Kupenda Ganda la ndizo kuteleza.

3. Roho Mbaya
Watanzania wengi wanapenda kusikia habari mbaya Kwa wenzao. Yaani akisikia mwenzake kafukuzwa kazi wengi wetu wanashangilia. Kwa nje wanakuambia pole lakini ukiondoka watakavyokusema na kushangilia.

Watanzania wengi ukitaka uwabambe wakushangilie ukiwa kiongozi fanya tumbua za mara Kwa mara. Washushe wenye vyeo au wafukuze kabisa, utashangiliwa wewe Kwa shangwe kuu. Lakini muongeze mtu Cheo uone Kama watashangilia Kama utakavyomtumbua. Watapiga makofi tuu ya kuzugia.

Watanzania wengi hawapendi kuona unafurahia maisha na Mkeo/mumeo au watoto wako. Kufurahia kwako maisha na Mkeo watasema mnaringa, mnajishaua na watawapigia Hadi Dua ili muachane. Watanzania wengi ukiwapa watoto wako zawadi nzuri watakuambia unawadekeza😀😀 yaani tunachekesha kweli.

Usije mpendezesha Mkeo utazua tafrani Kwa Ndugu zako. Ati unamhudumia Mkeo kuliko ndugu zako utafikiri wao hawana mikono, hawana waume 😀😀. Roho Mbaya tuu

Wao wanachopenda uteseke ikiwezekana ufe kabisa. Huwezi amini siku ukifa watu wengi watafurahi na kusema tuone sasa mke wako ataishi vipi si alikuwa anaringa. Wao maisha mazuri huyaita kuringa na umasikini na kuishi kifukara ndio unyenyekevu 😀😀.

Roho Mbaya tu. KAZI kuuliza maswali yasiyona maana yoyote kwao. Mathalani; vipi maisha? Unaishi wapi? Vipi Shemeji hasumbui? Vipi hujajenga tuu? Hujaoa au hujaolewa tuu umri unaenda? Umri ukienda ni wako Kama sio umbea.

Alafu wanaouliza maswali haya ndio hao HAO wasambaza umbea. Hawajawahi kukusaidia Kwa lolote zaidi ya kujifanya na maswali Yao kana kwamba wanajali kumbe unafiki mtupu.

4. MAJUNGU
Watanzania wengi wetu kutokan na unafiki na uvivu tunashikilia nafasi ya Kwanza kwenye majungu.
Tunajua kuyapika na kuyapakua. Unajua majungu yanapendelewa Kwa sehemu kubwa na watu wavivu wasio na kazi za kufanya.

Kujadili maisha ya watu. Utasikia yaani mke wake Malaya, sijui mbaya, sijui blah blah! Alafu wanajadili mambo ambayo wao wenyewe yamewashinda.

Utasikia jamaa pesa zake ni zandagu, za freemason na watatunga na hadithi za uongo na Kweli hapo ku-justify Hali zao kuwa Bora wao walivyo kuliko wenye Utajiri wa ndumba.

Majungu ndoani
Majungu maofisini
Majungu kwenye makanisa na misikiti na nyumba za Ibada.
Majungu mpaka kwenye Misiba.

Kwa Kupenda vya Bure, jitu halijachanga chochote lakini kwenye Misiba ndio linakuwa na mdomo kusema chakula sio kizuri mara kidogo. Utafikiri msibani watu wameenda kula.

Watu Kama hawa ni vile wanachekewa Ila Kwa watu Kama Mimi huwaga siwavumilii iwe mi kwenye Misiba au Harusi wanapaswa wapewa black n white.

Tunapaswa kubadilika. Na ili tubadilike tunapaswa kuambiana ukweli na kukomesha tabia hizi za hovyo.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Point zote ni konki!

Na zote hizo ziko mitaa ya ufipa pale!

Machadema ndio tabia zao hizo!
 
Leo umeichambua vizuri kabisa mienendo na sifa za wana CHADEMA.
wako radhi kwa lolote dhidi ya mwanachama mwenzao kisa maslahi.

Mfano ni BAVICHA na wale wabunge 19 imekuwa nongwa hata salamu wanapitana kama mabubu.
 
Back
Top Bottom