Watanzania ni wasahaulifu au wana mioyoni ya kipekee?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Kwa matukio yaliyowahi kuibuka na kusababisha hasira kwa wengi, lakini baada ya muda hali ikawa kimya, inaweza ikawa ni ishara kuwa Watanzania ni watu wa kipekee sana. Ama ni wasahaulifu au wana mioyo ya kipekee ya kusamehe au kupuuzia mambo.

Nitatoa mifano michache.

Serikali ilipoamua kuwahamisha Wamasai wa Ngorongoro toka kwenye ardhi yao ya asili, watu wengi walipaza sauti wakiitaka Serikali ibadilishe huo mpango.

Kulikoni mbona hilo halizungumziwi tena? Wamasai wameshapatiwa haki yao?
 
Tanzania ilipoingia mkataba na DP WORLD dhidi ya bandari za Tanganyika, watu hawakukaa kimya. Walidai marekebisho yafanyike au mkataba usitishwe. Hata wengine walienda mbali zaidi kwa kutaka kuandamana bila mafanikio.

Madai ya wananchi yalisikilizwa? Mbona hatujapewa mrejesho?
 
Kipindi fulani, mmoja wa Wakuu wa wilaya alirekodiwa akiwarubuni madiwani wa Upinzani ili wajiunge na Chama Tawala kwa staili ya kuunga mkono juhudi.

Pamoja na ushahidi huo kuwasilisha TAKUKURU kwa mbwembwe, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa juu ya mtuhumiwa. Badala yake, DC aliyedaiwa kufanya hilo alitoka hadharani na kudai kuwa kungali na hela ya kuendelea na manunuzi kwa wote waliokuwa tayari kuvikimbia vyama vyao.

Si wananchi, wala wanasiasa, wala TAKUKURU au hata mwajiri wake walioweza kumkemea hata kwa maneno matupu.

Wanasiasa wa Upinzani walipiga kelele lakini baada ya muda, hilo nalo likasahaulika.
 
Kwa matukio yaliyowahi kuibuka na kusababisha hasira kwa wengi, lakini baada ya muda hali ikawa kimya, inaweza ikawa ni ishara kuwa Watanzania ni watu wa kipekee sana. Ama ni wasahaulifu au wana mioyo ya kipekee ya kusamehe au kupuuzia mambo.

Nitatoa mifano michache.

Serikali ilipoamua kuwahamisha Wamasai wa Ngoro Ngoro toka kwenye ardhi yao ya asili, watu wengi walipaza sauti wakiitaka Serikali ibadilishe huo mpango.

Kulikoni mbona hilo halizungumziwi tena? Wamasai wameshapatiwa haki yao?
sio watu wengi bana,
ni wanaharakati vibaraka wachache sana wanaofadhiliwa na kurubuniwa kwa vipande vya fedha na mabwenyenye ya magharibu kujaribu kuvuruga amani na utulivu wa waTZ, na kujaribu kuwahadaa na kuwachochea waTanzania wenye shughuli zao muhimu na mipango yao ya kujipatia vipato, eti waamini mahali fulani Tz kuna uomevu au uvunjifu wa haki za binadamu hali ya kua si kweli...

waTanzania ni waerevu sana, waungwana na wako chonjo mno.
Wanajua na kufahamu kikamilifu kwamba, kwenye maisha kuna changamoto na mabadiliko yasiyoepukika na kwahivyo kunahitaji hekima na busara kuyakabili na kuyatatua na sio kuchochewa na kuamini kirahisi tu upotoshaji wa wanaharakati ambao hata kuishi kwao kunategemea ufadhili wa mabwenyenye na wanapoishi pia si humu nchini tena ni ghambo na inafahamika wazi...
 
Mzee Lowassa alipokuwa "active" kisiasa, alishambuliwa sana na Wana CCM na vyama vya Upinzani wakimhusisha na ufisadi.

Baada ya "kupumzika" Siasa, hakuna kelele tena. Wananchi nao hawawahoji akina Nape au akina Lema wathibitishe kama kweli Lowassa alikuwa fisadi au aliwatisha kisiasa. Lowassa hazungumziwi tena. Watu wameshasahau yote aliyokuwa akituhumiwa.
 
Mkuu, tatizo ni maagano yaliyowekwa juu ya uwepo wa mwenge wa uhuru kupitia mizimu, ili upate kuangaza nje ya mipaka ya Tanzania.
 
Mmoja wa wanaisia aliwaahidi watu wa Kigoma kama si Ujiji kuwa wakati wa utawala wake, angepafanya Kigoma/Ujiji kuwa kama Dubai.

Nilifika Ujiji mwaka Jana. Ni pazuri, lakini hapafananii hata Kigamboni, sembuse Dubai. Inaonekana mheshimiwa alimaliza kipindi chake bila kutimiza ahadi yake.

Sijawasikia watu wa Kigoma na Watanzania kwa ujumla wakiisulubu Serikali yao kwa kuwahadaa watu wa Kigoma. Yumkini, hata hiyo ahadi ilishasahaulika!
 
Watanzania ni watu wa kipekee sana, wana mioyo ya kipekee ya kusamehe au kupuuzia mambo.
Watanzania ni watu poa sana, ni watu wa upendo sana, ni watu wa kuridhika sana, ni watu wa shukrani sana, ni watu wa ku forgives and forgets, hata uwafanyie nini, wanasamehe na kusahau, ule muda wa mitano tena ukiwadia, wanakuwa wamesamehe na kusahau kila kitu hivyo wanachukua, wanaweka, waa!. Mitano tena!
P
 
Mzee Lowassa alipokuwa "active" kisiasa, alishambuliwa sana na Wana CCM na vyama vya Upinzani wakimhusisha na ufisadi.

Baada ya "kupumzika" Siasa, hakuna kelele tena. Wananchi nao hawawahoji akina Nape au akina Lema wathibitishe kama kweli Lowassa alikuwa fisadi au aliwatisha kisiasa. Lowassa hazungumziwi tena. Watu wameshasahau yote aliyokuwa akituhumiwa.
friend,
this is politics,
hakuna jambo geni wala jipya unless ni mgeni au si mwanasiasa...
 
Kuna kituko kingine kinachoendelea mpaka sasa.

Inasemekana, wabunge 19 wa viti maalum wanaodaiwa kutokea CHADEMA hawakupata ridhaa ya vyama vyao kuvikalia hivyo viti. Pamoja na CHADEMA kuwakana, Serikali kupitia Spika wa Bunge imeendelea kuwategemeza bungeni kinyume na Chama walichojinasibu nacho, jambo ambalo ni kinyume kabisa na Katiba ya Tanzania.

Najaribu kufikiri tu! Hilo lingewezekana kwa jirani zetu Wakenya?

Watanzania wenyewe hawajali hata kidogo, na pengine hawajui hata kuwa ni Kodi zao ndizo zinazotumika kuwalipa mishahara hao watu wanaodaiwa kuvunja Katiba ya nchi yao.
 
Kwa matukio yaliyowahi kuibuka na kusababisha hasira kwa wengi, lakini baada ya muda hali ikawa kimya, inaweza ikawa ni ishara kuwa Watanzania ni watu wa kipekee sana. Ama ni wasahaulifu au wana mioyo ya kipekee ya kusamehe au kupuuzia mambo.

Nitatoa mifano michache.

Serikali ilipoamua kuwahamisha Wamasai wa Ngoro Ngoro toka kwenye ardhi yao ya asili, watu wengi walipaza sauti wakiitaka Serikali ibadilishe huo mpango.

Kulikoni mbona hilo halizungumziwi tena? Wamasai wameshapatiwa haki yao?
Wewe unashangaa hilo. Kuna mwamba aliwapa umeme, maji, akihakikisha mnasikilizwa, elimu bure, kupingwa rushwa.

Wengi walifanya sherere alipokufa. Watanzania hawajui hata mtu anayosimamia maslahi yao.
 
Kuna kituko kingine kinachoendelea mpaka sasa.

Inasemekana, wabunge 19 wa viti maalum wanaodaiwa kutokea CHADEMA hawakupata ridhaa ya vyama vyao kuvikalia hivyo viti. Pamoja na CHADEMA kuwakana, Serikali kupitia Spika wa Bunge imeendelea kuwategemeza bungeni kinyume na Chama walichojinasibu nacho, jambo ambalo ni kinyume kabisa na Katiba ya Tanzania.

Najaribu kufikiri tu! Hilo lingewezekana kwa jirani zetu Wakenya?

Watanzania wenyewe hawajali hata kidogo, na pengine hawajui hata kuwa ni Kodi zao ndizo zinazotumika kuwalipa mishahara hao watu wanaodaiwa kuvunja Katiba ya nchi yao.
Asilimia90 ya wale wamama wabunge wa covid19 ni wake na wachumba za viongozi wa Chadema, unadhani kuna nia ya dhati ya kuwaengua chadema?

Hivo ni kweli mwanaume kamili unawexa kupambana kwa nguvu zako zote kuharibu kazi ya mke wako?
 
Wengi walifanya sherere alipokufa. Watanzania hawajui hata mtu anayosimamia maslahi yao.
Umeshawahi kusikia tena mtu katekwa? Umewahi kusikia tena maiti zimeokotwa zikiwa ndani ya viroba? Umeshasikia tena malalamiko ya wafanya biashara kuchukuliwa fedhakwny akaunti zao? Umewahi kusikia tena jambazi kateuliwa rc/dc?
 
Umeshawahi kusikia mamiliomo biashara zao zimekufa sababu ya umeme? Migogoro ya kifamilia?
 
sio watu wengi bana,
ni wanaharakati vibaraka wachache sana wanaofadhiliwa na kurubuniwa kwa vipande vya fedha na mabwenyenye ya magharibu kujaribu kuvuruga amani na utulivu wa waTZ, na kujaribu kuwahadaa na kuwachochea waTanzania wenye shughuli zao muhimu na mipango yao ya kujipatia vipato, eti waamini mahali fulani Tz kuna uomevu au uvunjifu wa haki za binadamu hali ya kua si kweli...

waTanzania ni waerevu sana, waungwana na wako chonjo mno.
Wanajua na kufahamu kikamilifu kwamba, kwenye maisha kuna changamoto na mabadiliko yasiyoepukika na kwahivyo kunahitaji hekima na busara kuyakabili na kuyatatua na sio kuchochewa na kuamini kirahisi tu upotoshaji wa wanaharakati ambao hata kuishi kwao kunategemea ufadhili wa mabwenyenye na wanapoishi pia si humu nchini tena ni ghambo na inafahamika wazi...

👉🌈🥱
 
Kwa matukio yaliyowahi kuibuka na kusababisha hasira kwa wengi, lakini baada ya muda hali ikawa kimya, inaweza ikawa ni ishara kuwa Watanzania ni watu wa kipekee sana. Ama ni wasahaulifu au wana mioyo ya kipekee ya kusamehe au kupuuzia mambo.

Nitatoa mifano michache.

Serikali ilipoamua kuwahamisha Wamasai wa Ngoro Ngoro toka kwenye ardhi yao ya asili, watu wengi walipaza sauti wakiitaka Serikali ibadilishe huo mpango.

Kulikoni mbona hilo halizungumziwi tena? Wamasai wameshapatiwa haki yao?
Bhulyanhulu wasukuma walihamishwa dhahabu ichimbwe,wamasai siyo special, hawana haki yoyote,ardhi ni Mali ya serikali na rais ndiye mtunzaji mkuu
 
Back
Top Bottom