Nimeamini....Wenye Hekima Hulipwa Umri!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,720
Nelson Mandela anatimiza miaka 20 (11/02/2010)tangu aachiliwe kutoka katika Gereza alikotumiakia kwa mia ka 27!

Picha ya chumba(cell) cha Mandela akiwa Robben Island.

Hapo chumbani kuna vifaa 4 tu;
-Pa kulala, kitanda?/Kirago?
-Stuli ndogo
-Debe
-Sahani na kikombe!

Je, unalinganishaje umri alio nao huyu mzee hadi sasa(miaka karibu 91), na mateso haya aliyoyapata kwamiaka hiyo yote?

-Je Huenda mateso yale yalimkomaza mwili sana na akawa fit?

-Au kukaa bila kufanya kazi kwa muda mwingi kunasababisha mtu aishi zaidi, maana mwili unakuwa haukutumika?

-Ni nini siri ya umri mwingi wa mzee huyu?

Eee Mungu mbariki mzee huyu mwenye heshima na hekima, aishi miongo kadha mingine!
 
uvumilivu ndio msingi ya hayo maswali yote dia,alivumilia na kamwe hakukata tamaa
 
maisha marefu na mafupi yote ni zawadi na mapenzi yake Mungu.

kumbuka si wote wapigao mbio sana hupata taji.......................
 
uvumilivu ndio msingi ya hayo maswali yote dia,alivumilia na kamwe hakukata tamaa
Pearl, unamaanisha ukiwa mvumilivu sana utajaliwa umri?
Je uvumilie hasa mambo yepi?
 
Nelson Mandela anatimiza miaka 20 (11/02/2010)tangu aachiliwe kutoka katika Gereza alikotumiakia kwa mia ka 27!

Picha ya chumba(cell) cha Mandela akiwa Robben Island.

Hapo chumbani kuna vifaa 4 tu;
-Pa kulala, kitanda?/Kirago?
-Stuli ndogo
-Debe
-Sahani na kikombe!

Je, unalinganishaje umri alio nao huyu mzee hadi sasa(miaka karibu 91), na mateso haya aliyoyapata kwamiaka hiyo yote?

-Je Huenda mateso yale yalimkomaza mwili sana na akawa fit?

-Au kukaa bila kufanya kazi kwa muda mwingi kunasababisha mtu aishi zaidi, maana mwili unakuwa haukutumika?

-Ni nini siri ya umri mwingi wa mzee huyu?

Eee Mungu mbariki mzee huyu mwenye heshima na hekima, aishi miongo kadha mingine!
hapo kwenye red nafikiri walikua wanafanya kazi ngumu mda mwingi mkuu sahihisho tu.
 
Pearl, unamaanisha ukiwa mvumilivu sana utajaliwa umri?
Je uvumilie hasa mambo yepi?

Ni zawadi tu kama alivyosema AK, kwani kuna watu hawakuona hata birthday yao ya kwanza na huwezi kupata maelezo kwa nini imekuwa hivyo. Pia kuna watu wameishi hadi wakachoka na hakuna sababu kwa nini. Kama unamwamini Mungu basi utaelewa kwa nini nasema hivyo. Kwa wale wasioamini wataongelea biology na probability! Kwa vyovyote vile hakuna sababu inaweza kuhalalisha kwa nini mtu mwingine afe mapema ukiacha matatizo yetu ya dunia ya kumi mbili!
 
maisha marefu na mafupi yote ni zawadi na mapenzi yake Mungu.

kumbuka si wote wapigao mbio sana hupata taji.......................

AK kwa mara ya kwanza sioni sabau ya kutokukuunga mkono!!! maisha kweli ni tunu tu ya Mwenyezi Mungu!!!
 
mambo ya kuvumilia ni mengi,kwasababu usipofumilia hata hapa JF kuna watu wanakwaza sana usipovumilia unaweza kufa kwa pressure wenzako wakaendelea kuishi,alikutana na watu tofauti tofauti,makwazo ya kila aina,mateso etc but alivumilia na kuwa na nia moja na naamini ktk yote hayo alimtanduliza Mungu.
 
Mandela hapo ndo alipolala,maskini babu wa watu pamoja na mateso ila alivyotoka jela hakuwafukuza wazungu.Mungu mpe maisha marefu Nelson Mandela
 
AK kwa mara ya kwanza sioni sabau ya kutokukuunga mkono!!! maisha kweli ni tunu tu ya Mwenyezi Mungu!!!

asante mpendwa kwa kuniunga mkono. mbona wengi tu siku hizi wameishavumbua hazina kubwa ya hekima niliyojaaliwa? tatizo mwanzoni atu walikuwa wanasoma maoni yangu bila kuyatafakari!

any way thanks and God bless you
 
bold yako haionyeshi mkuu, labda ungepaka rangi!:D
yah nimeweka rangi,naikubali hoja yako kama ulivyosema kwakweli maana naona pia kama watu wenye hekima mara nyingi huishi muda mrefu sana wala si uongo,tatizo ninachojiuliza sasa ni je tutaendelea kupata watu wenye hekima kama hawa na wengineo tena?maana naona kadri siku zinavyokwenda maadili yanazidi kuponyoka kwa kasi kubwa;mfano tu rejea hapohapo south na kwa rafiki mkubwa wa mandela
prezidaa jacob zuma mambo yake.
 
Mandela hapo ndo alipolala,maskini babu wa watu pamoja na mateso ila alivyotoka jela hakuwafukuza wazungu.Mungu mpe maisha marefu Nelson Mandela

Kweli Mama, inauma sana kwamba binadamu mwenzetu aliishi hapo kwa kipindi kirefu namna hiyo. Umri ambao wenzangu wa huku pwana mtu anazaliwa na kukaribia kupata mjukuu!

Lakini kitu cha kufurahisha ni kuwa kipindi alichoishi baada ya jela kitakuwa kimelipa machungu yake yote na kufuta machozi yake pia. Nilisikitika sana kwamba mtu aliyelia naye (Winie) hawakuweza kufurahia maisha pamoja. Kwa vyovoyte vili, imelipa sana bila kujali alianzaje na kupitia wapi!
 
asante mpendwa kwa kuniunga mkono. mbona wengi tu siku hizi wameishavumbua hazina kubwa ya hekima niliyojaaliwa? tatizo mwanzoni atu walikuwa wanasoma maoni yangu bila kuyatafakari!

any way thanks and God bless you

Sasa sisi tusemeje? Nilidhani washangiliaji ndio wanaiofahamu vizuri mechi. Kumbe hata wachezaji wamo?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom