Nimeamini Tanzania yangu kuna watu wana hela

Halafu kuamka na matongo tongo usoni ni kutokana na maisha yetu na vitanda tunavyolalia.


Jamani ile nyumba sijawahi amka nina matongo tongo machoni yani kama Mandonga vile, Nikiamka kama sikua nimelala, Na nikilala kama Nimeamka yaniii.

Wajomba tutafteni pesa Tutafteni pesa.. watu wana maisha bwana.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ni family Friend wetu,akamwambia maza Likizo naomba walete watoto kwangu.

ilikua likizo ya pasaka "wiki 1" tu tukafika ukiachama na uzuri wa lile jumba ambalo macho yalishalizoea..

ukiachana na thamani za ile nyumba ambayo macho yalishazizoea,kisanga kilichoniacha mdomo wazi ni CHAKULA.

Picha linaanza usiku dinner naona jikoni ugali unasongwa,wali unapkwa,Pilau linapkwa,Ndizi zinapkwa,Achana na manyama manyama na vitoweo vingine.

Fresh nkasema labda kuna wageni, Mida ya kula imefika kwenda mezani Meza refu hiyo hapa na kuleee ina futi zisizopungua 10 urefu wake.

Ukijisevia unasimama unapta hotpot moja moja, Mjomba hiyo siku nilihisi ntajinyea.

Nilikula si mchezo,halafu sasa watu uliza tulikua wangap Mimi na dogo 2 house girls (ambao sikuwaona mezani kabisa) wao wanalia huko huko jikoni.

so uktoa wageni sisi kuna maza house (tunamwita aunt) asie hata na undugu na sisi (ila ana pesa) ndio mana akawa aunt etu.

jumlisha na bro mwingine Jumla mtu nne tu pale dining ila bufeeee ni la watu wasiopungua 8 na wote wanakula na kusaza.

Hiyo haijaishia hapo,tumekula tumeshiba,Asubuhi Chai mezani mimi huyooo wahi jikoni kupasha Kiporo, si nikakutwa napasha pilau na wali ili nikanywee chai..

Bwana weee house girl waligombezwa ile siku sijapata ona, kisa eti ni kwann hawakumwaga viporo wanaacha watto tunataka kuvila viporo, jamani jaman nikamwambia Aunt kiporo kitamuu, Aunt akaniambia weee hebu kakae seblen dada atawapkia Pilau na Wali mnywe chai.

Kachukue juice upunguze njaa ngojea dada akapke plau.

Basi dada wakaambiwa chap chap watupkie plau na wali la kunywea chai, Viporo vishamwagwa hapo.

ki ukweli ile nyumba sijawahi isahau mpaka na kesho..

Halafu kuamka na matongo tongo usoni ni kutokana na maisha yetu na vitanda tunavyolalia.

Jamani ile nyumba sijawahi amka nina matongo tongo machoni yani kama Mandonga vile, Nikiamka kama sikua nimelala, Na nikilala kama Nimeamka yaniii.

Wajomba tutafteni pesa Tutafteni pesa.. watu wana maisha bwana.
Hahahahahahah daahhh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom