Nimeamini Tanzania yangu kuna watu wana hela

mipango99

JF-Expert Member
Aug 20, 2022
264
355
Naam habarini wakulungwa mabaharia.

Nihivi nilikuwa nasimuliwa kunawatu nchi hii wanaishi kuliko mfalme ..ntataja niliowaona

1: Kuna kipindi nilivyo kuwa chuga nilifanikiwa kwenda kufanya kazi kwa mchaga flani pande za njiro.

Meneja wa precision Air tawi la Tz, asee hiyo nyumba ulinzi uliopo noma, nyumba imetulia imejitenga flani hivi nje kumependeza nilikaa nusu saa lakini niliona. Ni kama nimeongeza miaka 2 ya kuishi, watu wanakula maisha bwana usipime.

Ya 2: Huko chuga niliingia kwenye nyumba ya jamaa mmoja kipindi hiyo chuga ebwanaee yule jomba sjui ni 'freemason' nyumba nzima imewekwa zuli jekundu kama lile la ikulu vyumba vyote kila. kwenyekona kuna flat skrn zile za touch bei yake uspime. Nje kunagari benz×3 imepata pacha hyo ilikuwa mpya lakini kaicha inachakalia hapo kuuliza hana mda wakupeleka gerej.

Nimekaa dakika mbili napiga kazi hata sjamaliza naskiaaa toooka kijana achahyo kaz shika hela yako. Naondoka nawai ndege sahv naelekea mwanza nkirud nitakutafuta ..Nkicheki nshavuta jiwe 5 nikatimka moyoni nasema kuna watu wanahela.

Ya 3: Nikiwa chuga kuna waziri mmoja mstaafu awamu ya Kikwete tulienda kupiga kazi kwake ebwana kunawatu wanahela ndani

Kuna mabwawa manne
yenye aina mbalimbali za samaki, nyumba 3 kali, mandari kali ,yaani haichoshikutazama :sema nlicho mkubali huyu wazir yupo simpo sana baada ya kumaliza kazi day1

Akavuta K Vant kubwa mbili tukawa tunakunywa taratibu stori zake sasa. Anasema kijana zangu mikipindi hicho nipo China ghorofa refu zaidi dunian niko chumba chajuu sjui 800 huko 900 nikama niko nje yadunia nimekaa miezi 6, mara anasema minikiwa nimeboeka nampigia padri nan sjui aniandalie nyumba huko moshi kwenye makaz yao kisha Naenda kutuliza akili huku nakula mvinyo wa Jerusalem.

Anasema sehemu hiyo ndochimbo analolipenda kunafanya akili irelax.baada ya K Vant kuisha stor nazo zikaishia hapo na waziri flani.

Niliingia nimepauka nikatoka na meremeta.

Unaweza na wewe kuongezea uliwahi kutana na mtu mwenye pesa hadi uka shangaa.

Thank you.
 
Kwa nilivyo isoma story yako siku ukifika Dar mitaa hii utajua hujui huku ndiko matajiri walipo sasa, huko unapo pataja ni chamtoto tu, siku ukifika Dar temebelea mitaa hii na mrejesho ulete.

1. Masaki
2. Oysterbay
3. Mbezi Beach
4. Tegeta Madale,Masaiti,Nyuki
5. Bahari Beach
6. Ununio
7. Mbweni
8. Tegeta "A"

Kwa ujumla kwa Dar, wilaya ya Kinondoni ni ya moto sana kwa makazi na location kali za kuishi halafu zina fuata zingine kama Kigamboni n.k
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom