Nimeamini TANESCO inatumika kisiasa

Nimeamini TANESCO inatumika kisiasa

mmeuaminisha uma wa watanzania kwamba mgao umeisha.mbona jioni hii mmetukatia umeme na tuliacha kuchaji taa zetu tukijua mgao umeisha kumbe ZILONGWA MBALI ZITENDWA MBALI.
 
Kila mtu anapenda umeme uwepo,Kama huna weledi na jambo ni bora ukauliza badala ya kila jambo kuihusisha ccm, suala la uwashaji wa mitambo ni suala la kitaalam mbali na MW zinazotakiwa pia kuna suala la capacity ya pressure inayotakiwa kuweza kuendesha mitambo ya kufua umeme
 
walahi siku hizi tanesco wamekua na ahadi za kukupa tamaa kama siasa za jimbo la uchaguzi unapewa tamaa ya karibuni mambo mazuri siku zinaenda hali ile ile.
wamekuwa waongo kama UKAWA
 
Nina zaidi ya mwezi hapa nilipo kanda ya ziwa sijaona taarifa ya habari ya saa mbili usiku. Kila siku umeme unashinda ila ikifika saa moja na robo wakati wa taarifa ya habari ya Channel 10 ambayo pia huchelewa kuonyesha habari za kampein wanakata umeme, kwa hiyo huwa nawahi kuangalia taarifa ya ITV saa 12 asubuhi.

Sasa wameanza mtindo wa kukata umeme wakati wa kusomwa taarifa hiyo na wanarudisha umeme mara taarifa inapokwisha .

Je, kwa ratiba hiyo TANESCO haitumiki kisiasa ?!

CCM kwa mtindo huu tegemeeni kukosa kura zaidi kuliko, kwani mnatia hasira sana.

Mkuu ni kuwaadhibu tu ccm
 
LUKU



Cost TZS 14,041.97
Service Charge TZS 11,040.00
VAT 18% TZS 4,514.75
EWURA 1% TZS 250.82
REA 3% TZS 752.46
TOTAL TZS 30,600.00
Cheki makato hayo halafu mnasema mnatoa huduma.Subirini tarehe 25/10 mtatutambua

Nikuwaiga chini mkuu hawafai kabisa
 
Tufahamisheni gesi bado inaingia mbona bado mgao uko pale pale Jamani msitudanganye kwa sababu ya kumbeba mgombea wenu mlitoka mbele ya vyombo vya habari mkatangaza umeme wa uhakika na kusema Uganda Kenya Malawi wanamgao je Tanzania? Mara mtauza umeme nje ya Nchi na kusambaza gesi nchi nzima mnatudanganya.
 
Jana Mhe. Waziri wa Nishati na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco waliwadhihirishia Watanzania kuwa sasa matatizo ya umeme sasa BASI baada ya kuwasha mmoja ya mashine inayoleta gesi kutoka Mtwara. Tulifurahi sana jana lakini cha ajabu hapa Mwanza saa 11.50 za asubuhi walizima umeme na umeme umerudi saa moja jioni ya leo. Tunauliza, Je yale majigambo ya jana yalikuwa yana maana gani?. Sisi ni watu wazima, msiwe mnatudanganya na ieleweke hata umeme wa gesi ukianza kura ni ya LOWASSA.
 
hiyo mitambo inadungwa usiku pia maana umeme unakatika had usiku wa manane
 
Tukuyu, kyela na busokelo kila inapofika sa 18 wanakata na hurudisha kesho yake, huu mwezi tatu toka waanze
 
hii Nch ni ya hovyo sana. wasomi wanatumiwa na wana siasa kama makapi
 
Nakufuatilia sana bw Mramba, hujatuambia kuwa kuna mgawo wa umeme, watudanganya kama watoto. Suala si kufunga mitambo ya gesi-hilo zaidi ya miezi sita sasa, kawaambie wajukuu wako! Tunajua kuwa kuna upungufu kutokana na songosongo kusimama -na hili ulisema mwenyewe. na Megawats alizokuwa anazalisha seth snigh nao ni upungufu ref. escrow. Haya sasa sema kuna MGAWO MPAKA MKAMILISHE kuingiza gesi ya Mtwara.
Mkiendelea kudanganya nitaingia hapo ofisini tupigane!
 
Back
Top Bottom