Nimeamini TANESCO inatumika kisiasa

Nimeamini TANESCO inatumika kisiasa

Mkatiwe tu ninyi kwa nini? Huku nilipo umeme mda wote upo hata walivyokua kwenye matengenezo tunawashukuru Tanesco kwa kutokata umeme kabisa.
Ndiyo maana unaipenda CCM mkuu sisi malofa ni shida tupu na ndo maana tunaichukia CCM inatutesa sana. tarehe 25/10 lazima tulipize kisasi.
 
Nipo Morogoro Kilosa umeme bado matatzo jana umekatika kutwa nzima na leo nako kama jana unakatika saa 12 asubuh unarud had saa 5 sasa cjajua hyo gesi ni kwa ajil ya magogoni na lumumba ama vp
 
Hizo posho mnazopewa huko ccm mnadhani the same thing is happening huku ukawa........typical gamba

Weka usahidi kuthibitisha hilo kijana kama huna we endelea kula posho za ukawa zilizokuweka hapo ulipo.
LUKU



Cost TZS 14,041.97
Service Charge TZS 11,040.00
VAT 18% TZS 4,514.75
EWURA 1% TZS 250.82
REA 3% TZS 752.46
TOTAL TZS 30,600.00
Cheki makato hayo halafu mnasema mnatoa huduma.Subirini tarehe 25/10 mtatutambua
 
Wasalaam Wadau wa JF na GT wote.

Ninapoandika Uzi huu kwasasa Hatuna Umeme hapa Tulipo, tatizo hili hapa kwetu #Kilosa halijaanza wiki iliopita Tarehe 07/09/2015 wakati Tanesco wakitangaza Kujaribu mitambo ya Gesi.

Huku kwetu Tatizo la kukatika Umeme kwa Masaa 16 mpk 18 kwa siku limeanza Tangu mwezi wa Saba (07) Mwanzoni, ni takribani Miezi mitatu sasa hatuna umeme wa Uhakika na Bila Taarifa yeyote kutoka katika Shirika hili la Ugavi wa UMEME.

Wiki iliopita TANESCO walipotangaza mgao utakoma Tarehe 14/09/2015 tulijipa moyo basi nasi tumepona, UMEME uliendelea kukatika, Likaja Tangazo Umeme wa uhakika unapatikana sasa Ijumaa tarehe 18/09/2015 tukaisubiri Iyo jana umeme pia ukakatika kwa masaa 13.

Leo tena nnapoandika sasa Umeme umekatika saa 01:53 asubuhi hii na kurudi bila shaka ni mpk saa 4 usiku.

Sasa naomba TANESCO watuambie kuna nini kinaendelea mgao huu miezi mitatu mfululizo?

Najiuliza kwanini Mgao bila taarifa?

Hapa mimi kama mimi nimeshapata Hasara ya zaidi ya mil 4 tangu mgao Uanze Mkoa wa Morogoro, ikiwepo wilaya ya kilosa. Na kuna taarifa, sio hapa MOROGORO tu, maeneo mengi nchini YALIOPO PEMBEZONI yana mgao mkali sana wa masaa kati ya 16-24

Najiuliza Pia waandishi wa habari mpo wapi Kuutetea Umma ulioko pembezoni ya miji mikubwa kwa mateso haya?

Yan mnaandika tu mgao wa UMEME wakikosa umeme wakazi wa Dar es salaam. Kwann? Au hamjui haya?

Nadhan Tunahtaji kufikiri pamoja. TANESCO tangazeni mgao Tujue, tujipange tununue Majenereta. Mna turudisha nyuma kimaendelo na maisha yamekuwa ghali maradufu.

Mashine za unga zinasaga usiku wa manane, Wachoma mageti hawalali wanakesha kumalizia tenda za watu. Samaki wangu wa mil 3 waliozea kwenye freezer 😡 nikifika hapo. Huwa natamani kufanya lolote. (hasira sana). Maana nakaribia kufiliska.

Eeh Mungu Nisaidie!
NOTE: umeme huu una katika kila siku iendayo Kwa Mungu. Na hatujui hatima yetu

Tafadhali Moderator msiunganishe uzi huu, unahtaji Majibu yakina sana, hasara tunayopata kwa mgao huu ni kubwa kuliko propaganda zinazofanya na Tanesco.
 
Last edited by a moderator:
Daaaaah mkuu sie wa Kilosa Morogoro ndio tunapata shida kuliko wilaya zote Tanzania yani umeme ni majanga
 
Inawezekana tanesco wana kalenda yao tofauti. ... maana huju nilipo wamekata alfajiri na jana walirudisha saa sita usiku.
 
Aisee mm nina hasira na hawa tanesko mpaka nashindwa kuongea ni upuuzi na ujinga uvivu wa kufikiri walio nao hawa watu pumbavu kabisa km ni matengenezo waanze kufanya saa nne usiku sio mchana watu wanatafuta maisha hii nchi ya kipumbavu sana hii
 
eti wanasingizia wanaunagnisha gesiii. kama mitaambo ya gessi inabadilishwa kwa miezi mitatu, so shows how incompetence we are!!!
 
Mimi nipo kijichi umeme umekatika toka Jana saa10 jioni mpaka sasa hakuna umeme
 
Watanzania tunaishi kwa mazoea ndio maana hawa jamaa wanatuchezea watakavyo na hawachukuliwi hatua yeyote.
 
juzi tulitangaziwa kwamba siku ya jana ijumaa, tatizo la kukatika kwa umeme, litakuwa mwisho, kutokana na kukamilika kwa uingizwaji wa mfumo wa ges kwenye mitamo ya kuzalisha umeme.

Chakushangaza leo saa 12 alfajiri tayari wameshachukua umeme wao. Sasa tunajiuliza ihi shida ya mgao wa umeme mbona inafichwa?

Maana sisi mgao huu ulianza tangu mwezi wa sita. Kilichotushangaza ni pale tanesco ilipokuja kusema hati mgao utakuwa wa siku 7 ?

Embu hapa Tanesco wawe wa kweli au hakuna pesa za uendeshaji wa mitambo ya kufua umeme? Watuambie ukweli.

Au ni agizo kutoka juu kipindi hiki cha kampeni kuzima umeme kwa maslai ya watawala kudhoofisha upatikanaji wa habari za wapinzani?

Katika nchi za wenzetu kipindi cha kampeni. Ni kipindi muhimu sana kwa taifa. Vyombo vya habari vinakuwa LIVE kila wagombea wanapokwenda ili kuwapa fursa wananchi kuwasikiliza wagombea ili mwisho wa siku wamchague kiongozi bora.

Mfano mzuri ni kwajirani zetu kwenya vyombo vya uma viliwajibika kwa wananchi kuhakikisha vinawapa habari za kila mgombea kila anapokwenda tofauti na hapa kwetu vyombo vya uma vimekuwa haviko huru.

Tuache mchezo uhu wa kutumika kisiasa ingekuwa nchi za wenzetu tayari vyombo hivi vingekuwa vimeshapelekwa mahakamani kwa kuwanyima wananchi haki yao kikatiba ya kupata huduma na habari.
 
Na usishangae kabla ya uchaguzi bei ya umeme ikapungua.
 
Watanzania tunaishi kwa mazoea ndio maana hawa jamaa wanatuchezea watakavyo na hawachukuliwi hatua yeyote.

Nadhani kuna haja ya kuwa tunaenda mahakamani kudai fidia kwa Hasara tunazoingia, haiwezekani kila siku tubebe hasara za Tanesco, kodi tunatoa, mita zetu zina chajiwa service charge, service my ass!

Watanzania lazima tuseme tumechoka, Umasikini huu tunajitakia. Tuchukue hatua
 
Back
Top Bottom